Najitolea Maisha yangu kwa ajili ya WatanZania- Raisi Magufuli!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Ni lini mara ya mwisho uliwahi kusikia Raisi wa nchi akiongea maneno mazito na yanayoingia ndani ya mishipa kama hayo? Kwamba ameamua kujitolea maisha yake kwa ajili yetu kwa kweli naweza kusema Raisi Magufuli ni Superhuman kwani amekwenda hatua ya mbele zaidi ya binadamu wa kawaida, ameweka ubinafsi pembeni kwa ajili yetu, nakumbuka maneno ya Mlm.Nyerere aliyewahi kusema ,,tunataka Raisi ambaye matatizo na umaskini wa Mtanzania unamuuma na hiyo ndiyo iwe sababu ya yeye kuamua kugombea Uraisi"!

Sasa ukimwangalia fisadi Lowasa unaweza kusema kwamba matatizo na umaskini wa MtanZania unamuuma? Ingekuwa hivyo angemuibia huyu Mtanzania masikini na kuzidi kumdidimiza kwenye dimbwi la umaskini?
 
ulimi hana mfupa - matokeo ndio yatasema sio maneno. kila mtanzania ana wajibika hata kutoa maisha yake -ila siku unasikia watu wameuwawa wakiwa kazini hapo pia ametoa maisha yao kwa Tanzania.
 
Hahahahah hivi Lowassa naye anawawazia hivi kama nyinyi mfanyavyo?
 
Anahatarisha maisha ya watendaji wake wasio na ulinzi kwa sababu anapanda mbegu ya mawazo ya kuwadhuru kwa utekelezaji wao.

Yeye Magufuli ana ulinzi wa kijeshi na kikachero masaa 24 mpaka siku anastaafu na kufa.

Hawezi kusema amejitolea maisha yake. Waliojitolea maisha yao ni kama Afisa Misitu Arusha aliyeuawa, sio Rais anaetembea na misafara ya walinzi wenye silaha za kivita. Anadhani wananchi wote hawaelewi populist rhetoric.
 
kwa ivo mnataka kutuambia kwamba walinzi wake ndiyo wanataka kumuua au yeye ndiyo hawaamini kwamba wanauwezo wa kumlinda dhidi ya wanaotaka kumuua?

Hiyo sentensi inaweza kuwa na maana na tafsiri nyingi kulingana na jinsi kila mtu anavyoona na maadamu yeye mwenyewe Raisi Magufuli hakufafanua alichomaanisha basi kila mtu atakuja na tafsiri yake, binafsi nimeelewa kwamba ameamua kujitolea muda wake, Elimu yake, ujuzi wake, uzoefu hekima zake, na hata kama ikiwezekana kupoteza baadhi ya marafiki kwa ajili ya kuwatumikia wananchi basi na iwe hivyo kwa ajili ya watu wa WatanZania lkn hiyo ni tafsiri yangu na kama nilivyosema kila mtu anaweza kuwa na yake!
 
Let us avoid these idle talks about our leaders. Choose your topic wisely and do not drag somebody's name into a discussion without a clear reason. For example, in this thread, how does lowasa's name come in?
 
wewe kweli haujaelewa chochote.

swissme
 
Let us avoid these idle talks about our leaders. Choose your topic wisely and do not drag somebody's name into a discussion without a clear reason. For example, in this thread, how does lowasa's name come in?

Kwani, kuna tatizo gani mimi kulitaja na kulijadili jina la fisadi Lowasa?
 
Hee kuna muda mwingine nashindwa kuwaelewa ,kwani Hapo Ikulu alienda kucheza bao ?? Na amejitolea maisha yake dhidi ya akina nani ?? Kama sio wanaomzunguka
 
Kichwa cha habari kinakubetray, inaonekana haukutaka kumwongelea Magufuli bali ulikuwa unatafuta sababu ya kutaja jina la Lowasa.

Nina uhuru wa kuandika na kupangilia ninachoandika ninavyotaka kama vile wewe ulivyokuwa na uhuru wa kusoma au kutokusoma ninachoandika!
 
Ww ni lafa ,Usipomtaja Lowassa hupati usingizi?subiri tutakutana 2020 ndo utamjua ni nani?
 
Back
Top Bottom