Elections 2010 NAJITOLEA kumfanyia rais WANGU KIKWETE kampeni ashinde tena URAIS

Rais wangu hana muda mchafu wakubabaika na kiavatar kama hiki wakati mama salma ni the real beuty tena anayejua kupiga pamba!
kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI bila thithiem amani yetu itakuwa mashakani na tutakaopata shida ni sisi kina mama na watoto!

Acha uwongo weye!!! huna hata aibu ya kusema uwongo!!! Nenda ukafanye kampeni labda utakumbukwa upewe ukuu wa wilaya kama siyo ubalozi. Nchi imejaa ufisadi lakini huoni hayo ya akina mama kushare kitanda wakati wanajifungua, wanafunzi kukaa chini, nchi kukosa maendeleo yote hayo huyaoni!!!! Wizi wa mabilioni na hakuna aliyekamtwa hadi leo, yote hayo huyaoni!!!! Naona kumbe uwongo ni jadi yako.
 
cm kaamua kufanya joke tu sidhani kama yuko siriaz!! hahahaaaaa kama tunatumia asilimia kubwa ya muda wetu kwenye emails and the like yeye mbona anachekelea tu hakemei na kukomesha...hawezi??? anyway asante kwa kichekesho mana unatuongezea afya ya moyo na ubongo!!
 
hahahahaha....unajua bwana, shida zinatofautiana ndo mana wazee wa zamani walisema kitanda usicholalia huwezi jua kunguni wake...kwa sisi wala hoi,maji ya kuotea usiku,ukiondoka asubuhi unakariri unit za luku,matusi ya kondakta kwa kuwa umepungukiwa 50,kushindia maji ya kunywa kwa kusingia unafanya diet kumbe ukata...na huku tunasikia taifa linapoteze mabilioni ya fedha kutokana na ujasusi wa kimtandao,viongozi wanajinunulia mashangingi, migodi ikitwaliwa kwa hila na watu wachache wakineemeka nayo,mafisadi hawafikishwi kwa pilato.....sidhani ka tutakuwa na mtazamo na sawa kama wako CHEUSIMANGALA......ila nin amini ungebahatika kuishi maisha tunayoishi sisi huku chini.....CHEUSI MANGALA UNGEBADILI MWENDO HUO!!!!!!

Sayonara!!!
 
nimewahi kusema huko nyuma na leo narudia.........
huyu Kikwete hata afanye utumbo gani.wanawake huwaambiii kitu kwa Kikwete....
jamaa utasema ana dawa.

Mkuu, huyu jamaa ana dawa. Zamani tulikuwa tunasema ana ngekewa sana na viumbe hawa.

Cheusimangala kila la kheri ati..... kwani ni haki yako!!
 
Ukisikia jamaa andai anataka kumkampenia baba yetu jua anapata Chochote kitu au Kaahidiwa Ubunge wa Viti maalumu
 
Nampenda sana rais wa nchi yangu prezdaaa Kikwete,hata kama watu wanamponda lakini mimi naona kuwa baba wa watu anajitahidi,hata Obama kuna aliyoahidi lkn bado hajatekeleza!
watu ni wavivu wakujitafutia maendeleo wanadhani rais akisema maisha bora kwa kila mtanzania basi atawagawia ugali wa bure kila siku,maisha bora ni pamoja na sisi wenyewe kumuunga na kumtia moyo rais wetu kwa kujituma kutafuta maendeleo yetu binafsi.
naombeni mnifundishe mbinu mbalimbali zakuwashawishi watanzania kumchagua tena PREZDAAA KIKWETE ashinde ktk uchaguzi ujao kwani nina imani kabisa yeye ndio kiongozi tunayemuhitaji!C.C.M hoyeeeee!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
thank you!
Yanatoka moyoni hayo au kiunoni maana mkulu naye mambo yake si haba katika mitaa ya KATI pale....
Enewei endelea naamini unaweza kuambulia ukuu wa wilaya samwhere nchini hapa hapa
 
Back
Top Bottom