NAJITOLEA kumfanyia rais WANGU KIKWETE kampeni ashinde tena URAIS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NAJITOLEA kumfanyia rais WANGU KIKWETE kampeni ashinde tena URAIS

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by cheusimangala, Apr 22, 2010.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nampenda sana rais wa nchi yangu prezdaaa Kikwete,hata kama watu wanamponda lakini mimi naona kuwa baba wa watu anajitahidi,hata Obama kuna aliyoahidi lkn bado hajatekeleza!
  watu ni wavivu wakujitafutia maendeleo wanadhani rais akisema maisha bora kwa kila mtanzania basi atawagawia ugali wa bure kila siku,maisha bora ni pamoja na sisi wenyewe kumuunga na kumtia moyo rais wetu kwa kujituma kutafuta maendeleo yetu binafsi.
  naombeni mnifundishe mbinu mbalimbali zakuwashawishi watanzania kumchagua tena PREZDAAA KIKWETE ashinde ktk uchaguzi ujao kwani nina imani kabisa yeye ndio kiongozi tunayemuhitaji!C.C.M hoyeeeee!
  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
  thank you!
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  wtf going on here!
   
 3. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Hatutakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, KIDUMU CHAMA CHA JAMII (CCJ):target:
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,111
  Likes Received: 24,173
  Trophy Points: 280
  Mi nimeona hapo tu.....

  Hakyanani hata yeye akiona avatar yako naye atakupenda!
   
 5. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,956
  Likes Received: 21,117
  Trophy Points: 280
  Obama ana muda gani tangu awe rais na Kikwete ana muda gani tangu awe rais?
  Kuhusu kumuunga mkono Kikwete ni haki yako kikatiba.
   
 6. m

  marymar Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nampa big up our prezidah kwani ni hodari sana na hata mungu alisema jisaidie nami nitakusaidia sio kwa vile maisha bora kwa kila mtanzania ndo tujibweteke. haipendeziiiii
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  u guyz r jokers of highest caliber..lol

  sasa kaa rais haleti maendeleo kwa watu wake kuna faida gani ya kuwa zigo la rais na maswahiba wake..si bora nchi iuzwe kila mtu ajue lwake?
   
 8. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Rais wangu hana muda mchafu wakubabaika na kiavatar kama hiki wakati mama salma ni the real beuty tena anayejua kupiga pamba!
  kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI bila thithiem amani yetu itakuwa mashakani na tutakaopata shida ni sisi kina mama na watoto!
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  same here

  haya mengine 'mapito' tu!!!!

  I wish I could not leave to see upuuzi ukijirudia tena mwaka huu uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!

  'am not a politician but only a friend of politics............'
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  jamani kwani chama gani kiliingia madarakani damu ikamwagika??

  wat makes you think so bibie??
   
 11. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ngoja nikaendelee kujitafutia life bora nitarudi tuendelee jioni shosti wangu!
   
 12. k

  kero Member

  #12
  Apr 22, 2010
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa naona umaamua kujichimbia kaburi.
  Lo mtanzania huyu kafichwa gizani, hajui hata anahitaji nini kutoka kwa Raisi wake, Siku ukimpata Raisi utajua nini ulinyimwa ka haki yako ya msingi.
  Hapawezi kukawa na mtu anayeiitwa raisi and then watu wanaishi ka wanyama wa mbuga za Serengeti. "Survival for the fittest"

  A president has a big role to play we mtoto wa Tanzania, it is over 45 years lakini hauna any kind of life social welfare, unashiriki kujinyima kwa kukubali ujinga kwamba sisi nchi yetu ni masikini, sio kweli, Ni viongozi vichwa maji- will remain to be the reason why hata wewe haujitambui.
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  First term ni kupanda mlima..........second kushuka.....sijui itakuwaje......manake second terms za Mwinyi na Mkapa duh
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naomba mahakama iruhusu mgombea binafsi ili nimsapoti Kikwete kama mgombea binafsi lakini chini ya CCM siko tayari kumkampenia.
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  naona cheusi unatafuta ubunge ukishamaliza biashara zako za box...
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hawa ndio wapiga kura 2010........................... And we keep wondering why we r not moving forward!!!!?!
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Nadhani kama wengi wasemavyo, ni kama umefurahishwa na tabasamu lake na sura labda lakini kwa utendaji, bora jeshi lipindue litutawale tu!
   
 18. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Baba yangu mshirikina
  Nasema, baba yangu ni mshirikina.
  Mbona unaguna? Mimi nimeshasema, baba yangu ni mshirikina. Ninazo sababu za kusema hivyo kwani nina kila sababu za kuamini hivyo (baba yangu ni mshirikina).
  Visa vya baba kuwa mshirikina vinaanzia pale alipokuwa akimfukuzia mama. Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani kuna wengi waliokuwa wakimtaka mama na sisi tulitakiwa tuseme ni nani anafaa kuwa baba yetu. Mimi nikiwa mmoja wa wanafamilia nilifuatilia kwa karibu mno ni nani anafaa kuwa baba. Kila mmoja alikuwa na mbwembwe zake, mmoja alijifunga mbawa akawa anaruka juu na kutua, na mwingine alisema ana-uelewa mkubwa kwenye mambo ya uchumi kwa hiyo atatulea vema na kutuletea maendeleo kwenye familia yetu. Na wengine ambao kwa kweli nilishindwa hata kufuatilia nyendo zao, nao walikuwa na yao.

  Vituko vya baba tuliyempokea ni vingi vingi mno, kimoja ni kudondoka mbele zetu wakati akitushawishi sisi watoto tumruhusu kuwa baba wa familia. Baadae alidai kuwa ilitokana na jitihada zake za kutuombea ili tuwe na maisha bora. Kuna watu walituambia nyie huyo anayetaka kuwa baba yenu ni mshirikina, lakini sisi tukakataa na baadae tukakubali kuwa yeye ndo awe baba yetu.
  Siku moja akiwa nyumbani kwa kaka yetu mmoja aliyekuwa na kasherehe kake, baba huyu wa kufikia yalimpata yaleyale ya kudondoka na kupoteza fahamu. Vipimo vilionyesha kuwa hana tatizo isipokuwa ni uchovu tu wa kazi nyingi.
  Baada ya tukio hilo mimi nilianza kujikumbusha yaliyojiri huko nyuma na nikakumbuka yale ambayo watu walikuwa wakituonya juu ya mababa watarajiwa.

  Nikiwa katika tafakari mara likatokea zogo kubwa kati ya watu wa imani na jamaa mmoja maarufu huku mtaani kwetu (anaitwa Hayahaya). Huyu Hayahaya aliwapiga mkwara watu watakaojitokeza kumpinga baba mlezi wetu wa sasa kuwa watakufa ghafla. Baada ya mkwara huo mtu mmoja wa imani akamwamba Hayahaya kuwa afute kauli yake la sivyo yeye atakufa ghafla. Na hapo nikamuona Hayahaya akigeuka mbogo na kumuambia mtu wa imani kuwa yeye si mtoto, na kumuomba kama anataka kujua kazi zake basi aende kwenye kibanda chetu anamoishi baba ndo atajua kazi zake. Mi kwa mara ya kwanza nilidhani ni utani lakini baadae nikaja kugundua kuwa jamaa hakuwa anatania kwa kuwa anajua anachokifanya kibandani kwetu. Nilitegemea baba atakasirika na kumuonya Hayahaya juu ya kauli yake lakini nikaona kimya.

  Atamkaripiaje mtu aliyemuwezesha yeye kuingia kwenye kibanda chetu na kuwa baba yetu? Inawezekanaje baba akae kimya juu ya kauli ya kukidhalilisha kibanda chetu?

  Ndo maana nasema baba yangu ni mshirikina!!!
   
 19. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Namna nzuri ya kumpigia kampeni raisi wako.

  Waambie wana JF amefanya yapi katika kipindi hiki cha miaka mitano inayoisha katika kumwondoa babu,baba, Bibi, Mama yako aliyeko kwenye umasikini mwingi kijijini.

  Wambie watu wa mtwara na hata DSM kwanini ahadi ya kumaliza barabara ya Mtwara Dar kwa kiwango cha lami ifikapo 2008 haikutimia mpaka leo wakati pesa zipo.
  Waambie JF ni kwanini ana muda mwingi sana kwenye mambo ya kirafiki kama kuhudhuria misiba, kuwatembelea hospitali, kwenda kwenye harusi nk, wakati hana muda wa kutosha kuwauliza watendaji wake mambo nuhimu kama vile jibu la tatizo la foleni jijini, kinachokwamisha ujenzi wa daraja la kigamboni, kwanini uwanja wa kilimanjaro ukodishwe kwa hela chache sana wakati uko kwenye hub ya utaalii nchini. Kwanini kuvunja mkataba na RITES inatuchukua miaka wakati dalili zote za kampuni hiyo kushindwa kuendesha shirika letu ziko wazi. nk nk.

  Wambie watanzania sababu za kumfanya Raisi mpaka sasa hajchukua au kumwajibisha yeyote kutokana na kitendo cha watendaji kuchomeka vipengele vingine kwenye sheria aliyoisaini kwa mbwembwe mbele ya dunia halafu inaonekana ni feki.

  Waambie wafanyakazi wa Tanzania ni kwa nini marupurupu ya wabunge na viongozi wa kisiasa ni makubwa kuliko mishahara ya wanataaluma katika fani mbalimbali mfano madaktari, waalimu, wafanayakazi wa afya, marubani, mahakimu na majaji nk, nk.

  Waambie watanzania sababu za mgao wa umeme wakati kuna mitambo ya kuzalisha umeme iliyotakiwa kutaifishwa na serikali kwa mujibu wa sheria za nchi iko kwenye aridhi yetu haizalishi umeme.

  Ukifanya haya na mengine mengi tu, utakuwa umempigia kampeni kali sana na hata akipata hakuna atakayekuwa anamlaumu tena raisi wako.
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  sasa huu ushirikina umeingiaje hapa????????????
   
Loading...