Najitokeza kugombea Ubunge jimbo la Mafia 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Najitokeza kugombea Ubunge jimbo la Mafia 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Malaria Sugu, Jul 10, 2009.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jina langu. MzeewaHhoja
  Elimu yangu. Inatosha kupitishwa.
  Kadi yangu. nishailipia kama kijana
  itikadi yangu. maendeleo
  Chama Changu. C

  Nilitembelea kisiwani Mfia hivi karibuni. Nilianzia Dar hadi Nyamisat na Kushuka Bandari ya hatari ilipo kilindoni. ni sfari yenye machofu ktk karne hii ya sayansi na teknlojia. ni safari ya kuliwa na Mbu na ya kucheza na maisha.
  ni safari iliojaa hatari hasa baada ya usafiri wa huko kutumia vijdau viduchu huku vikiondoka usiku wa manane huku vikjaa watoto wa Changa
  nilitembelea utende huku mvua ikinyesha njia ilijaa matope na huku gari ikikwama kila wakati.
  niiltembelea Kirongwe na huko magari hayapiti isipokuwa muyabebe .ni njia ilojaa matope.
  nilitembelea Jimbo, mlali, Banja, jojo, Kifinge, Baleni na Ngome ambapo naamini Mbunge Hajafika huko kote nikitizama maendeleo na sio kupiga kampeni. huko kote wakulima wanaytumia vijembe vya mkono na hakuan tireketa katika kipindi hichi cha Kilimo KWANZA.
  Nilitembelea skuli sekondAr ya Kirongwe na Kitomondo kwa kweli hamna walimu hasa wa masomo ya Sayansi na kwakweli wansoma kwa shida Huku wakitumia Vibatari.
  Nishati ya umeme ni ya kubahatisha na kijisehemu tu ndicho chenye kupata huduma hiyo ya shida ktk kisiwa cha Kilndoni. Kuhsu mabomba ya maji hayo usiseme. hakuna maji salama na hakuna mpangowa kuwapatia, l Kirongwe wala baleni au Dongo kama wnaweza kupata huduam hii kwa 200 ijayo
  Kuhusu uvuvi mhe, mzee hapo tena wananchi wanafukuzwa kama punda na wawekezaji a. kuhus bandari mzee usiseme. Wnajengewa uwanja wa ndege kwa ajili ya mafisadi wenda kuchukua raslimani
  za watu wa huko. wananchi wanalalama mbunge kahamia DAR jIJI LA MARAHA
  Najitokeza kugombea Ubunge kwa Chama Cha C , nitampinga mbunge wa sasa na naamini kwa kisiwa kivyokuwa nitapata kwa 90%. nitakuwa mtu safi na nitakiimarisha kisiwa kukitoa kwenye giza lilopo
   
 2. K

  Kyaruzi Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbunge mwenyewe ndio wewe?, si ukajifunze kwanza kuandika, kupanga paragraph na kuanza na helufi kubwa kwenye majina ya sehemu.

  Kinyume cha hapo watu wa Mafia watakuwa wame ruka maji na kukanyaga mkojo! wenyewe kule mnaita "makojo"
   
 3. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mzee hata wewe kiswahili hukijui. umeona wapi neno helufi. sema herufi. umesoma chhoni nini
   
 4. L

  LUKULUKU Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee umenena. mimi leo nimerudi katika kushiriki ktk wale maiti nimeona Jimbo lilovyokuwa naskika CASPEAN WANAKULA PESA za wananchi na bara bara haijengwi. inawezekana mafisadi wameivamia Mafia . kagombee Ubunge uwaokoe wenzetu. lkn usiwageuke baadae , nakupa kura yangu kabla sijaipiga
   
 5. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Andika kwa kiswahili ili kila mtu akuelewe hapa jamvini.
   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubunge wa JF twaweza kukupa lakini wa Jimbo inabidi uwe na watu wako huko na upange na lugha fasaha ya kuwaconvice- chama C ndio CCM?
   
 7. K

  Kyaruzi Member

  #7
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walau mimi sigombei ubunge infact hata uenyekiti wa Kitongoji si qualify!
   
 8. E

  Eddie JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Baba yako kawa Mbunge Mafia miaka 20 mbona hakujenga hizo barabara, shule, vituo vya afya na Bandari? Mbona alikuwa anakaa Makumbusho tu Mafia anakuja wakati wa uchaguzi?

  Ikiwa mzee wako kashindwa kuku somesha mpaka unashindwa kuandika utaweza kuwa Mbunge kweli ww? Mafia sio sultanate ile muwe mna rithishana tu.

  Tunakusubri kwa hamu sana njoo
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kumbe ndio maana ya zile thread nyingine!!!!
   
 10. mbuvu

  mbuvu Member

  #10
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakuunga mkono ukagombee na hivi kuna fununu mbunge wa huko anaishi dar.
   
 11. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Yaani kutembelea tu tayari umeshapata hamu ya kugombea! Wewe jamaa si ndiye yule mwenye thread zile za kidini dini? Wakazi wa Mafia siwajui sana, ila wakikupa ubunge, nitakuwa na mashaka na akili zao. Kwa nini usisubiri hizo siku 14 uwe Kadhi?
   
 12. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #12
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sio lazima uwe Mbunge ndio uwakomboe watu wa Mafai,otherrwise una lako jambo, Mi najua msaada unaweza kuutoa hata hapo ulipo na ukaupa mwongozo makini watu wakafanikiwa, sidhani kama Mapadri na Masheikh wana direct contact na Mungu na sie waumini hatumfikii Muumba mpak tupitie kwao.! BADILI FIKRA ZAKO.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Watu mnatafutana ubaya tu miye simo. Mbona wengine walioenda Mafia hivi majuzi na wenyewe hawataki kugombea huko na wameyaona hayo hayo tena wana "sababu" kubwa zaidi ya kugombea huko?
   
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mdau nini kimekusukuma kuona kwamba mzee wa hoja ni Omar Kimbau?
   
 15. m

  msabato masalia Senior Member

  #15
  Jul 10, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Muheshimiwa Spika,watu washaanza kuningilia.Mafisadi wananitafuta.Hivi BASATA wanaonaje hili la HATI miliki ya Ubunge? Mwanakijiji hatuwezipitisha muswada wa hili ili kuokoa uvunjifu wa amani?Kama wananchi wa B'mulo walivyosema CCM pitisheni sheria itakayosema CCM daima mkichagua wapinzani hakuna maendeleo.Mtikila alikuwa msuluhishi wa hili kwa mgombea binafsi.
   
 16. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani kutembelea tu tayari umeshapata hamu ya kugombea! Wewe jamaa si ndiye yule mwenye thread zile za kidini dini? Wakazi wa Mafia siwajui sana, ila wakikupa ubunge, nitakuwa na mashaka na akili zao. Kwa nini usisubiri hizo siku 14 uwe Kadhi?
  Niombe radhi kijana, WEWE udini kwako unapopiganiwa uslam tu?
   
 17. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Niombe radhi kijana, WEWE udini kwako unapopiganiwa uslam tu?
   
Loading...