Najitayarisha kujiunga na Chama cha Upinzani cha CCM punde baada ya mwakani

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Nikiwa naanza kufungasha ,sasa najitayarisha kuelekea Chama kinachoelekea kuwa kipya katika kambi ya Upinzani hapo mwakani punde tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Nia ni kuhamia CCM na kuhamasisha upinzani ,upinzani dhidi ya vyaChama Tawala kitakachotokana na UKAWA .Sababu kuu hupenda sana kuwepo upande wa upinzani na si vinginevyo.

Nitapambana na serikali hiyo hata kama inaongoza nchi sawasawa ,mpaka waelewe kuwa uongozi si lelemama na ni zamu yao kubeba lawama hata za kutunga au za uongo.

Wapenda maendeleo wote wa nchi hii msilemae na UKAWA njia ni moja tu ,tujiunge na CCM pindi tu kitapojiunga na upinzani hapo 2016.
 
Hivi kweli unadhani ccm wanaweza wakaleta upinzani wa kweli? Hapana aiseee why? Kwasababu wao kinachowaunganisha sio dhamira ya kuitetea nchi bali maslahi yao binafsi. Kwahio kamwe hawawezi kuwa pamoja kama wasivyokiwa wamoja sasa hivi....
 
Kitabomoka kama KANU Kenya na kwa kuwa hakitakuwa na msaada tena kwao watajitoa wengi tu na kujaribu kujipenyeza kwenye system mpya.. Najua wapo wanachama wenye mapenzi ya kweli na ccm lakini kwa sasa wamewekwa kando na mafisadi waliokiteka chama.. Hawa ndo watakaokichukua chama chao baadae baada ya mafisadi kuondoka..
 
Nikiwa naanza kufungasha ,sasa najitayarisha kuelekea Chama kinachoelekea kuwa kipya katika kambi ya Upinzani hapo mwakani punde tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Nia ni kuhamia CCM na kuhamasisha upinzani ,upinzani dhidi ya vyaChama Tawala kitakachotokana na UKAWA .Sababu kuu hupenda sana kuwepo upande wa upinzani na si vinginevyo.

Nitapambana na serikali hiyo hata kama inaongoza nchi sawasawa ,mpaka waelewe kuwa uongozi si lelemama na ni zamu yao kubeba lawama hata za kutunga au za uongo.

Wapenda maendeleo wote wa nchi hii msilemae na UKAWA njia ni moja tu ,tujiunge na CCM pindi tu kitapojiunga na upinzani hapo 2016.

Sidhani kama kitakuwepo pindi kitakapotoka madarakani, 1992 wakati wakusajili vyama CCM hawakujisajili kama chama. Na hakuna ushahidi wa kuonyesha CCm kimesajiliwa katika vyama vya Siasa Tanzania. Mwiba CCM kinaishi kwa ubabe wa Viongozi wake lakini hakijasajiliwa, pindi kitakapo toka madarakani ndio mwisho wa hicho chama, kinaweza kufutwa au kiombe upya usajili
 
Lol mapya haya
 
Lol mapya haya

Sio mepya hiyo ni hakika ,kama kumupa mtihani MSajili wa Vyama vya siasa Tanzania basi muulize suali hilo na sio akupe jibu la mkato ,akutolee formu ya kuomba usajili na kusajiliwa kwa CCM anaweza akakuambia muhusika wa kujibu suala hilo sio yeye. Au akakukatia simu ,CCM haikusajiliwa .
 
Mkuu Mwiba utajiunga ili ukiimarishe au..?

Kama unavyoelewa CCM inaanguka mwakani na UONGOZI wa TANZANIA kuhamishiwa Chama kingine kwa hesabu hizo inamaanisha CCM watakuwa bench ya upinzani dhidi ya Chama Kiongozi wa Taifa la Tanzania ,upinzani ni sehemu nzuri kuwatetea wananchi walala hoi ,CCM itakuwa inatetea wananchi.
 
Wakati huo Lowassa atakuwa kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni.

Umeona ,ila Lowasa ninaemfahamu harudi tena kwenye siasa ,ubunge hagombei alivyoniambia ,akishanyolewa kwenye CNEC ya CCM nae anarudi kijijini kuchunga ng'ombe na umri wake tutamsaidia kumpigia kampeni 2019 kugombea uenyekiti wa mtaa ,yaani wapinzani tutajipanga vizuri sana ,chama kitakachoongoza upinzani kitakuwa CCM kwa sababu kina uzoefu wa siasa za Tanzania ni lazima serikali ya UKAWA itakayokuwa madarakani wakati huo maji wayaite mee.

Ukiangalia tutakuwa na wasemaji mahiri akina Nape ,Mzee wa Ziara Kinana ,wazee wa busara akina Sita,Wasira Mwanamke wa shoka Tibaijuka yaani upinzani utatimia kwelikweli UKAWA hatuwapi nafasi zaidi ya mwaka mmoja tu au miwili serikali yao tunaipiga na chini.Hata wananchi wataupenda upinzani yaani ndani kuna ccm ,mimi naenda huko ,Je wewe kwanini usijiunge na kambi ya ccm ?
 
Yaani ndugu, wataka kuwa UPINZANImuda woote? Tunakutakia heri.. Ila jiuliza UNIP ya Kaunda huko Zambia iko wapi?
 
Nikiwa naanza kufungasha ,sasa najitayarisha kuelekea Chama kinachoelekea kuwa kipya katika kambi ya Upinzani hapo mwakani punde tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Nia ni kuhamia CCM na kuhamasisha upinzani ,upinzani dhidi ya vyaChama Tawala kitakachotokana na UKAWA .Sababu kuu hupenda sana kuwepo upande wa upinzani na si vinginevyo.

Nitapambana na serikali hiyo hata kama inaongoza nchi sawasawa ,mpaka waelewe kuwa uongozi si lelemama na ni zamu yao kubeba lawama hata za kutunga au za uongo.

Wapenda maendeleo wote wa nchi hii msilemae na UKAWA njia ni moja tu ,tujiunge na CCM pindi tu kitapojiunga na upinzani hapo 2016.

Kwa ujumla CCM imeshinda kwa asilimia 80, unajua hilo mkuu?
 
Wewe umemsikia Nape anavyopiga dongo ,madai yake yanaonyesha kuwa uchaguzi haukuwa wa haki na mizengwe imetumika ,japo anashangiria ushindi ,ila kilicho ndani ameshitushwa na kushindwa ambako ni kukubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.

Kusema CCM imeshinda kwa asilimia 80 hilo ni tatizo la CCM sio upinzani ,inawezekana kabisa hiyo asilimia 80 inawapiga kuwa milioni tano na asilimia 20 inawapiga kura milioni nane unafikiri kwa akili yako nani mpendwa na nani mshindi ?
ndio nikasema punde tu baada ya 2015 naelekea CCM ili nibaki paleplae upinnzani ,kuwatetea wananchi na zuluma za utawala wa UKAWA utakaokuwa madarakani.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom