Najisikia peponi kuwa na magufuli-mwakyembe

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,135
17,124
Asema ni kiongozi makini, mwenye msimamo, asiyekubali kuyumbishwa

Mwakyem(5).jpg

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison MwakyembeNaibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema amefurahishwa sana na uteuzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete na hasa kutokana na kumpangia wizara moja na Dk. John Magufuli, ambaye alisema ni kiongozi makini na mwenye misimamo asiyekubali kuyumbishwa katika utekelezaji wa kazi za umma.
Aliyasema hayo katika mahojiano maalum na NIPASHE kwa simu muda mfupi baada ya kuapishwa juzi na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dk. Mwakyembe alisema anajisikia vizuri sana kufanya kazi na Dk. Magufuli katika Wizara ya Ujenzi itakayoshughulikia ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege kwa kuwa ni kiongozi makini na mwenye misimamo sana hasa katika suala la utekelezaji wa kazi za miradi ya maendeleo.
“Najisikia vizuri sana tena mno kufanya kazi na Magufuli kwani ni mchapa kazi ambaye pia tumeshibana sana, pia ni kiongozi ambaye ana msimamo katika kutumikia umma ambao unaeleweka kwamba hapendi kuyumbishwa,” alisema.
Dk. Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela, alisema ameupokea uteuzi wa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi kama changamoto kwake kwani kiongozi yeyote makini anapopewa jukumu kubwa kama la uwaziri inakuwa ni changamoto ambayo anatakiwa kuhakikisha anatimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Kuhusu ufisadi, alisema kimsingi, kwa kuwa suala la kupiga vita ufisadi na rushwa limetungiwa sheria kwa maana hiyo ndani ya serikali litaendelea kupigiwa kelele ili kuwepo na matumizi sahihi ya fedha za umma.
Dk. Mwakyembe alianza kupata umaarufu kutokana na kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa utoaji wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura iliyopewa Kampuni ya Richmond Development LLC ya Hauston Marekani.
Kampuni hiyo ilipewa zabuni mwaka 2006 ya kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura wakati nchi ilipokabiliwa na ukame uliosababisha kukauka kwa mabwawa ya kuzalisha umeme.
Baada ya hapo, zilizuka tuhuma kwamba kampuni hiyo ilikuwa ya kitapeli na kwamba haikuwa na uwezo wa kufua umeme.
Tuhuma hizo ndizo zilizosababisha Bunge kuunda kamati hiyo ya uchunguzi iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe na kufanya uchunguzi ndani na nje ya nchi.
Dk. Mwakyembe akiwa mwenyekiti wa kamati hiyo, aliwasilisha taarifa ya uchunguzi huo bungeni Februari 7, mwaka 2008 huku kamati yake ikibainisha kwamba Richmond ilipewa zabuni hiyo kwa upendeleo na kwamba ilikuwa kampuni ya mfukoni.
Kamati hiyo ilipendekeza maofisa wa serikali waliohusika katika mchakato huo wawajibike kutokana na uzembe ulioisababishia serikali hasara ya kuilipa Richmond mamilioni ya fedha bila kuzalisha umeme.
Kampuni hiyo ililipwa Sh. bilioni 200 ambapo kila siku kwa miaka miwili Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilikuwa likiilipa Richmond Sh. milioni 152 hata kama haikuzalisha umeme.
Aidha, kamati hiyo ilimshauri aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ambaye alisimamia mchakato huo apime.
Siku iliyofuata yaani Februari 8, Lowassa na mawaziri wawili, Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Dk. Ibrahim Msabaha (Afrika Mashariki), walijiuzulu kutokana na kuguswa kwa kashfa hiyo.
Tangu hapo, watu wamekuwa wakimuita kuwa ni kamanda wa kupambana na ufisadi pamoja na wabunge wengine kadhaa wa Bunge la Tisa na wengine wamerejea katika Bunge la Kumi.
Walikuwa makamanda wa kupambana na ufisadi kutokana na kupigia kelele kashfa mbalimbali ambazo zimeiandama serikali katika miaka ya karibuni kama Richmond, Epa, Kiwira, Ticts, TRL kwa kutaja baadhi.
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,618
2,123
Kweli ushukuru mungu bse ungeweza pangwa wizara moja na Mustafa,Kawambwa etc sidhani kama angekuwa na amani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom