Najiandaa kwenda kumpigia kura Tundu Lissu umbali wa km 200

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,856
2,953
Licha ya umbali wa nilipojiandikishia kupiga kura na sheria za NEC kumtaka kila mtu kupigia kura pale alipojiandikishia tu.

Basi mimi Gluk nimeshaandaa safari ya kwenda kupiga kula umbali wa KM 200
Maana naamini kura yangu moja inaweza kuwaondoa watanzania katika hiki kifungo cha zaidi ya miaka 60 chini ya utawala huu usiojari utu, haki na uhuru.

Hii ni mara yangu ya pili kupiga kura, ila naimani kuwa kura yangu ya mwaka huu ni kura muhimu zaidi ya kura yangu ya miaka 5 iliyopita.
Mimi, uko wangu mzima, marafiki zangu 5271 ambao tunaunda Group la Telegram

Wote kwa umoja wetu wote tumekubaliana kuwa 28 kura zetu zote ni kwa ndugu yetu, kipenzi chetu na mbeba maono. Ndugu Tundu Antipas Lissu

Freedom is coming.
 
Mimi siko mbali Sana na kituo changu.

Isipokua nimewahamasisha majirani zangu wote ambao Ni waelewa tuamke asubuhi na mapema tukawe wa kwanza kabisa kuhakikisha Hakuna kura feki zinaingizwa halafu tunapiga kura Kisha tunatafuta baa ya karibu tunakunywa supu na Pepsi tu,hatunywi bia maana tunaogopa kulewa halafu jioni tushindwe kulinda kura, kufuatilia matokeo, kulinda ushindi na kushangilia ushindi kwa nguvu zote.
Bia tutaanza kunywa baada ya Chuma kutangazwa.

Nimeweka Oda ya mbuzi wanne kwa ajili ya sherehe ya Uhuru wa Haki.
 
Nyinyi wafuasi wa Lissu mnamatatizo gani kwenye vichwa vyenu?
mbona kama mmerukwa na akili?
hivi mtaweka tiki kwa usahihi kabisa bila kuharibu kura kwenye karatasi?
mbona kama mmepagawa hivi?
 
Wewe hata usafiri km 50,000 ni juu yako ,maana hata wana wa izrael walisafiri miaka arobaini kwenda kaanani lakini wengi wao hawakufiki.

Lissu kamwe hawezi kuwa rais wa Tanzania, ni sawa na kulazimisha mbingu na ardhi zikutane.

Mimi Nita safiri 0 km kumpigia kura JPM na lazima atashinda uchaguzi huu.
 
sorry

napaa na ungo nipate pia kutoa ulinzi kwenye anga la kituo cha shule ya Sekondari
 
Yaani nipoteze muda kwenda kumpigia kura msaliti wa Nchi anayerudi ubeligiji November

Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
 
Back
Top Bottom