Najaribu kuwaza endapo Lowassa ataikosa nafasi ya kuiwakilisha CCM!

Kifai

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
816
172
Nimekaa na kujiuliza mambo yafuatayo
1) Kwanini huyu jamaa katumia gharama kubwa sana kuandaa hii shughuli yake leo
2) Hivi ikitokea hajachaguliwa kuiwakilisha CCM ni nini kitatokea ndani ya CCM?
3) Hivi Lowassa akipewa hii nchi kutakuwa na uhakika wa kuwakemea mafisadi wa nchi hii?

Ni hayo tu
 
Nimekaa nakujiuliza mambo yafuatayo
1) kwanini huyu jamaa katumia gharama kubwa sana kuandaa hii shughuli yake leo
2) hivi ikitokea hajachaguliwa kuiwakilisha ccm ni nini kitatokea ndani ya ccm??
3) hivi lowassa akipewa hii nchi kutakuwa na uhakika wa kuwakemea mafisadi wa nchi hii?
Ni hayo tuu

Usiseme Endapo Bali Jua Kuwa Hatopitishwa Na Leo Ndiyo Amejichanganya Mwenyewe Ktk Hotuba Yake Kuonyesha Wazi Kuwa Ana Chuki Na Uongozi Wa Mkwere Na Hotuba Yake Nzima Kwa Muda Mfupi Tu Huu Anamdhalilisha Hivyo Ninavyomjua Mkwere Lowassa AKIUPATA URAIS Kristo Atakuja KUTUCHUKUA.
 
Usiseme Endapo Bali Jua Kuwa Hatopitishwa Na Leo Ndiyo Amejichanganya Mwenyewe Ktk Hotuba Yake Kuonyesha Wazi Kuwa Ana Chuki Na Uongozi Wa Mkwere Na Hotuba Yake Nzima Kwa Muda Mfupi Tu Huu Anamdhalilisha Hivyo Ninavyomjua Mkwere Lowassa AKIUPATA URAIS Kristo Atakuja KUTUCHUKUA.
sioni ni jinsi gani ccm hawatompitisha lowasa kuna watu wakiwa kwenye team yako ushindi ni wako na jamaa watu wote muhimu anao ongezea na pesa na media.
 
Du,sijui hii nchi Tumerogwa na nani?
maana unaweza ukakosa hata ya akiri ndogo ya kuwaza kuwa kuwa huyu mtu hii gharama anayoitumia kuutafuta urais atairudisha vipi kama akiienda ikuru,na yy aliipata wapi huu utajiri wote ngali yuko kwenye siasa na serikali miaka yote ya maisha yake.
jamani tuwe smart katika kuwaza kulikokujitengenezea bomu wenyewe.
 
Unajua kuna ufisadi na uadilifu sasa kibaya zaidi hapo upande mmoja huo una nguvu kubwa hasa ya pesa na ushawishi...yaani tupo hatarini sana...na endapo sasa upande wa pesa ukishinda ndio tumekwisha maana yale makashfa yote yalopita itaonekana wale wote watuhumiwa ni wasafi na wote walovalia bango watajuta..tutamkumbuka nyerere...hakika
 
Watu wa nchi hii bongo zetu zimedumaa. Tunashindwaje kuona na hata kusikia kuhusu njia hii ya kuusaka uongozi wa nchi kwa gharama kubwa hivi? Hata wakimpitisha mtaani tutamkataa kwa namna yoyote. Nchi hii haitaongozwa na fisadi tena. Kuleni pesa uongozi hapewi. Watanzania hawapo tayari kuongozwa na wagonjwa. Na tuyaepuke ya nigeria kumchagua rais mgonjwa.
 
Nimeshakuambia Lowassa Hawi Rais Wa Tanzania Na Ili Uamini Hili Subiria July 12 2015 Ndipo Utayaamini Haya Niyanenayo Kwako.

Lowassa anajifurahisha tu na kujipa matumaini katika safari yake ya matumaini. Pia anauhadaa umma wa Tanzania kwa kununua umati ili aonekana anakubalika!

Hizo ni mbio za sakafuni......., ajiandae kwa mshangao mkuu!
 
naomba kujua sitta alichokisema.

"Amesema ufisadi sio kitu cha kawaida some time huwa kinatengenezwa ili kumchafua mtu maana kwenye ufisadi hata chadema wapo na huwezi kumbadilisha fisadi hivyo hata mm nashawishika kufuata upande mmoja wenye nguvu"
 
Lowassa anajifurahisha tu na kujipa matumaini katika safari yake ya matumaini. Pia anauhadaa umma wa Tanzania kwa kununua umati ili aonekana anakubalika!

Hizo ni mbio za sakafuni......., ajiandae kwa mshangao mkuu!

huwezi kuwalipa watu wote wale na hata ukipewa hela huwezi kushangilia kama huna mapenzi na mtu husika yaani hata upewe shingapi huwezi kulazimisha mtu akupende
 
Ndimu nitapata wapi jamani niwape watu wenye chuki, wanao tafuta rahisi maskini kuongoza nchi, tutabaki na statement zile zile, nchi ni maskini, mwache atufundishe mbinu za kupata utajiri na sio mbinu za kubaki kuwa maskini. Mtazamo tu jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom