Najaribu kutafuta uhusiano kati ya shughuli za CCM na matatizo ya wananchi

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,857
7,846
Na Thadei Ole Mushi.

Wakati Wananchi wa nyanda za Juu Kusini wakiozesha mahindi, Mwenezi wetu yupo Pale Lumumba anaandaa kipindi cha Kwenda kufundisha kuhusu Itikadi.

Wakati Zabibu zikiozea Shambani kule Dodoma, katibu wetu yupo Ofisini na Mtolea wanapanga namna ya kutumia Fedha za Mlalahoi kwenye Chaguzi ambazo hazina maana kabisa kwa wananchi hivi ndivyo anavyobana matumizi ya Serikali.

Wakati Vijana wakihangaika asubuhi na jioni Kutafuta Ajira watu wanasaini Posho za Kufundishana Itikadi za Chama kila kukicha.

Nataka kusema nini?

CCM tunabahati ya kubadisha safu za Uongozi lakini hatubadilishi namna ya kufikiria.

Binafsi sioni mantiki au Impact ya Madarasa ya Itikadi na mabonanza yanayoendeshwa na idara ya Uenezi wa Chama.

Sioni Mantiki au impact ya Sera yetu ya hamia kwetu na Gombea tena.

Kiutafiti tunasema hakuna uhusiano wowote kati ya matatizo ya wananchi na mambo yanayofanywa na viongozi wa chama. Ccm inaishi sayari nyingine na Wananchi wapo sayari nyingine.

Muda huu tunaopoteza na mambo kama haya ni bora tungeutumia kudeal na matatizo ya wananchi yaani kuyasemea kwa sauti ili Serikali ichukue hatua.

CCM inapaswa kuwa mdomo wa wananchi, sauti ya wanyonge. CCM inapaswa kuwa kinara wa kukataa sheria Kandamizi kwa wananchi.

Ile CCM iliyokuwa na uwezo wa Kuisimamia Serikali ipo wapi? Kwa sasa Serikali yetu inasimamiwa na watu individual kama kina Fatma na Zitto.

Uwezo wa CCM umepotea moja kwa moja katika kusimamia mambo ya msingi na Maslahi ya Wananchi.Wamemezwa na Serikali kabisa, hawana ubavu wa kukemea.

Ole Mushi.
0712702602
 
CCM imepoteza mvuto inatakiwa kuondolewa kwa namna moja au nyingine
 
CCM sio viongozi wa ngazi za taifa.

Tatizo la myopic approach ni kudhani CCM ni viongozi wa kitaifa ambao wanaonekana kwenye TV na vyombo vya habari.

Halafu CCM inaisimamia serikali kupitia vikao halali vya chama na sio matamko kwenye mitandao.

Kupiga kelele kwenye mitandao ya kijamii sio tiketi inayoonyesha unaisimamia serikali bali ni kutafuta umaarufu ambao hauna vigezo vya fikra tunduizi.

Hili ndilo tatizo la kuishi maisha ya kwenye mitandao.

Eti Fatma Karume na Zitto ndio wamebaki kuisimamia serikali. Hili pia ni tusi kwa CHADEMA kwa sababu ndicho chama chenye serikali kivuli/mbadala

Inawezekama mleta mada hajui hata maana ya kuisimamia serikali.

Eti uwezo wa CCM umepotea? CCM ipi hiyo? Ile ambayo ulikuwa ukivaa sare zake unazomewa mitaani? Huyu mleta mada nadhani ana kumbukumbu kama za kuku!

Tanzania kuna vituko!
 
Hakuna mwenye shangwe na Ccm nanyi hilo mnalijua shida ni kujitoa ufahamu kwamba inapendwa kwa kutumia policeccm watanzania wanajua mna uwezo wa kutumia hata vifaru kuangamiza atakaewazomea na awamu ya tano inajibu kwa mtutu na si kwa hoja kama wewe ulivyoshindwa kujibu kwa hoja bali kwa vijembe
 
Back
Top Bottom