G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Hii ni kauli ambayo aliitoa kwenye bunge la bajeti linaloendelea siku chache zilizopita.Wengi tuliichukulia kauli ile kuwa ni ya aina yake hasa kwa jinsi ilivyowasilishwa.Wapo baadhi waliyoipuuza na kuiacha ipite.
Hivi ni nini kilichojificha kwenye uwaziri wa Prof. Mark Mwandosya hadi tunaambiwa "hujafa hujaumbika?" Mwandosya ni waziri pekee asiye na wizara niliyewahi kusikia duniani! Ama kweli "hujafa hujaumbika"
Wakati mawaziri wengine wanapanga bajeti za kuwatumikia wananchi kwa kutumia kodi zetu, yeye Mwandosya anapanga bajeti ya kula, kunywa na kutembea kwa kutumia kodi zetu watanzania.Ndiyo, ana haki ya kupanga bajeti! Si ni waziri? Mimi najiuliza sana mpaka napata hasira! Ni kwa nini Kikwete alimteua waziri anayetumia kodi za watanzania kujipangia bajeti ya kutumia yeye mwenyewe?
Kweli Kikwete kwa hili nilijikuta nazidi kumtafakari ni rais wa aina yake! Kuna nini kati ya Kikwete na Mwandosya hadi tunaambiwa kuwa hujafa hujaumbika? Ni fadhila gani na kwa jambo lipi zinazolipwa? Kuna mambo kama watanzania tunayachukulia kawaida lakini yanatupatia taswira ya ajabu sana duniani!
Ina maana kwa kauli ya Celina Kombani Kikwete anamuumba Mwandosya kwa kumpa uwaziri, shangingi na bajeti huku kukiwa hamna analofanya kama waziri kwa ajili ya watanzania? Hizi ni kodi zetu na mimi ni miongoni mwa walipa kodi nina haki ya kulalamika! Tuangalie matatizo lukuki yanayotukabili huku kukiwa na mawaziri wasio na wizara wanaopangiwa bajeti na kupewa mashangingi, walinzi na hadhi zote kama waziri!
Ama kweli "hujafa hujaumbika" Mimi mlala hoi nani ataniumba?
Pumzika kwa amani baba wa taifa la Tanzania...uliyakemea haya kwa uzalendo wa hali ya juu!