Naishukuru TCRA kwa kunizimia simu

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Nadhani nitakuwa wa kwanza kabisa kuishukuru mamlaka hii ya mawasiliano, TCRA kwa kunizimia simu aina ya GALACE SQ japo niliijua kuwa ni feki tangu watangaze kuzima, hivyo nilijiandaa kisaikolojia. Ni takribani wiki 2 sasa tangu izimwe.

Mtanishangaa kwanini naishukuru Mamlaka ila kiukweli, ningeendelea kuitumia sidhani kama mwaka huu ungeisha haijaniua. Ilikuwa napata maumivu makali ya kichwa, huku kikigonga gonga, na nilikuwa nikitumia vidonge nikidhani ni maumivu ya kawaida ila tangu imezimwa kichwa kimeanza kutulia taratibu hadi sasa kimetulia, JAPO SINA UHAKIKA KAMA NI KUTOKANA NA TATIZO HILO, KAMA NDO LIMEISHA AMA NDO LIMESHAATHIRI UBONGO WANGU.

Ninahisi kabisa tatizo ni hiyo simu kwani ilikuwa kadiri navyoongea, ndipo kichwa huuma na kugonga, ila nikitumia simu ambayo siyo feki sikuwa napata tatizo.

Nadhani kuna wengine baada ya kuzimiwa pia walishuhudia badiliko fulani chanya, basi waungane nami tuwashukuru TCRA.
 
Hahahha,aisee nimecheka mpaka basi uzii huuuuu
Hongera kwa kujitambua na kujali afya yako mkuu.
Pia zilikwa zinapunguza Adroid(Nguvu za kiume)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom