Naishi na Mwanaume, tatizo nikimgusia suala la ndoa anadai nisubiri hayuko tayari kwa sasa

Pisi kali

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,106
2,000
Ni kweli hakuna haja ya kuoa maana utaoaje wakati hata kabla ya kuoa unapata kila kitu kama mtu alieko kweny ndoa wadada mnapokubali kutoa pambuchi tena wengine mpka mnahamia kwa mabwana zenu mnatufanya tuone umuhimu na ulazima wa kuoa maana kama napata kila kitu kama aliea sasa kuna haja gani ya kuoa!!?? Kwa hiyo unajikuta unakuchukua huyu mnakaa wee akija shituka mnaachana unachukua mwingine hivo hivo mpaka na watoto unapata.

Kwa dini zingine ni sawa Ila kwa waislam ni DHAMBI “tunaambiwa tusiikaribie zinaa” sasa unavyofanya hivyo unafaidika duniani tu kwa tamaa za mwili Ila akhera kuna dhambi zako zinakusubiria, Kwahiyo hivi hanikomoi mm bali tunapata wote dhambi! Na dini anaijua vizuri haswa
 

munisijo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
1,077
2,000
Labda nikuibie siri moja kubwa sana ya sisi wanaume ambayo kwenye kikao chetu tumekatazwa asilani tusiitoe - Ipo hivi, kwa wanaume wote tulio oa, huwa hatuoi kwa hiyari yetu, yaani I mean huwa hatutaki kuoa, siku zote tuna tamanigi tuendelee kula tu maisha

Tatizo huwa linatokea pale tu ambapo ''tunafika bei'' sasa, aiseeeeeeee huwa hatusikiagi la muda, Mama, Baba, Kabila, rangi, uzuri wa mtu, historia ya zamani wala dini ... yaaani hata kama uliolewaga, sisi tunaoa tena na ndoa inadumu au kama upo na mwenyewe una mwita ''my wako'' tunaleta fitna mbaya na tunakuoa fasta sana

Sasa ''usipofika bei'' best, tuna visingizio kama vyote yaaaaani

Uwe na siku njema
 

Goldnessa

Member
Apr 30, 2021
63
150
Kosa la kiufundi ulilofanya bibie ni kuanza kuishi na huyo mwanaume kabla ujaolewa.Hizi sogea tukae zina maumivu makubwa sana mbeleni wanaofanikiwa kuvuka salama ni wachache.

Chondechonde angalia usifanywe shamba darasa.Alafu umesema mwanaume anataka watoto ila kwa dini yenu watoto kabla ya ndoa si ndo wanaitwa watoto haramu? Je hilo suala mmelizingumza na mwenza wako?au ndo mahaba nipofue?
 

ngongoti2000

JF-Expert Member
Nov 20, 2017
1,907
2,000
Habari zenu wanaJF

Waislam wenzangu A’alaykum (eid inanukia)

Niko na mtu tuna miaka mitatu hadi sasa tumepitia changamoto nyingi furaha na huzuni, kiukweli ni mtu ambaye hajawahi kuniacha hata hatua moja.

Swala lililonileta kwenu.

Huyu mtu ni muislam mwenzangu hamna changamoto zingine zozote isipokua kwenye swala la sisi kuhalalisha anakua mgumu mno (ndoa) ukimwambia tu basi tuhalalishe ni yuko muwazi yeye kwasasa hataki.

Huduma zote anatoa kuanzia matumizi (pesa) na huduma za chumbani hajaoa, tunaishi wote. Shida ni hiyo tu hataki tuhalalishe ndugu zangu nifanyaje na kuachana nae siwezi japokua mwenyewe alinambia kama naona ananichelewesha basi anipe space ndani ya muda flani ikiwa bado sijaipata hiyo ndoa turudiane.

Hata funga yangu naona haiswihi kabisa maana tunaishi wote then tunafunga eti. Kwenye kila kitu mnakubaliana ila swala la ndoa hapo hataki anasema nivumilie.

Simuelewi! Au ana miiko Niko hoves nimechoka kuzini

Hata mimi nisingekuoa kama unahamia kwangu kiholela holela kama wewe.......kitakachotokea mara nyingi ni surprise kwako kwamba ataoa mwanamke anayefaa kuwa mke siyo wewe mburula
 

Nuzulati

JF-Expert Member
Nov 25, 2020
2,358
2,000
Sasa hasara kwa Nani?? Mi yangu yananiendea na hiyo miaka 3 nikiona bado nitafanya ustaarabu mwingine maana ndio kwanza nitakua na 28yrsm
Una utoto mwingi kwenye maelezo yako umesema unatarajia kuwa mama na ulibahatika kuwa na mtoto bahati mbaya amefariki,kwa maelezo yako mengine utamvumilia huyo mtarajiwa kwa miaka3 endapo mtabarikiwa kuwa na watoto then na wewe jamaa ameshikiria msimamo wake kwa hiyo utaondoka ukiwa una years unaiyona ndogo mwenyewe .
 

Pisi kali

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,106
2,000
Kosa la kiufundi ulilofanya bibie ni kuanza kuishi na huyo mwanaume kabla ujaolewa.Hizi sogea tukae zina maumivu makubwa sana mbeleni wanaofanikiwa kuvuka salama ni wachache.Chondechonde angalia usifanywe shamba darasa.Alafu umesema mwanaume anataka watoto ila kwa dini yenu watoto kabla ya ndoa si ndo wanaitwa watoto haramu? Je hilo suala mmelizingumza na mwenza wako?au ndo mahaba nipofue?

Ukisoma comments nimelizungumzia mbona

Tunaongea anasema bado nivumilie nisiwe naharaka ndoa zipo
 

Kiraka

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
3,278
2,000
Hakupendi huyo ndio maana yupo tayari kukuachia muda utafute mwingine wa kukuoa. Lengo kuu la mahusiano hua ni mwisho wawili wapendanao wawe pamoja na kuanzisha familia.....Ukimpenda mtu kwa dhati kabisa muda wote unatamani umchukue/oe awe wako daima sasa kama mtu yupo tayari kukuachilia utafute wa kukuoa jua hakupendi. Yupo zake hapo kutimiza haja zake tena inawezekana hizo haja zake unazomtimizia ameshakina.

Wake up mate, Does this ain't ring a bell to you??
Nadhani hili ni jibu sahihi.
 

Pisi kali

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,106
2,000
Una utoto mwingi kwenye maelezo yako umesema unatarajia kuwa mama na ulibahatika kuwa na mtoto bahati mbaya amefariki,kwa maelezo yako mengine utamvumilia huyo mtarajiwa kwa miaka3 endapo mtabarikiwa kuwa na watoto then na wewe jamaa ameshikiria msimamo wake kwa hiyo utaondoka ukiwa una years unaiyona ndogo mwenyewe .

Sikupingi mtazamo wako umeniona na utoto mwingi..
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,725
2,000
Kama ni suala la dini unapata dhambi ambazo umeamua kuzifanya bila toba yoyote ukijua unazini mda wote
Pamoja na mwezi wa toba bado umo tu (una roho ngumu)
Ila sikuhumu Bali ndio ukweli

Turudi kwenye mahusiano ni kwamba umesema yeye ni 99.9 ila unaogopa kumuacha ukienda kupata asiekupa hiyo 99%
Hapo napo una udhaifu sana kwenye imani yako kwani hakuna anaejua ya kesho na maisha yako hupangi wewe

Huyo anakutumia kama taulo tu mpaka lichakae
Kwa udhaifu wako inabidi akuchezeshe mziki wake
Ila umejiwekea viashiria vingi vya kuendelea kuishi nae na sidhani kama comments hizi zitakubadilisha maana unategemea na mtoto wa zinaa pia
 

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,544
2,000
Hayo unayofundishwa ndiyo yatakufanya nikuoe Wala endelea kujazwa Mimi nakuzoom tu...

Nimekujengea Nyumba, nimekununulia gari, nimekufungulia biashara unataka Nini zaidi..

Show nakupa ya ukweli bado huridhiki haya endelea na mauzi yako.. majuto siku Zote Ni Mjukuu na tambua unaye washirikisha wanakuonea wivu ndiyo Maana maushauri mengi Ni ya kukubunjia Mahusiano..

Ok umenipa miaka miwili Mimi bado life start at age of 40...
Think twice
 

ni ngumu

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
4,114
2,000
Kimaisha yuko vizuri tu na mimi wala sio tegemezi kwake kila mtu anakazi zake (tunasaidiana)

Usahihi (hapo anajua yeye sasa maybe ameona mimi sio sahihi kwake)

Umri ana 35 mimi niko na 25yrs, naona hapo kwenye utayari wa kuoa kwake yeye mwenzangu bado

Kuishi pamoja, alinikuta najitegemea na yeye alikua anajitegemea, mawazo yake akasema tutafute nyumba kubwa tuishi pamoja hatukua na muda mrefu tangu tuanze mahusiano almost a month tu hivj, so kuanzia hapo hadi sasa tunaishi pamoja mkoa x


Kuzungumzia ndoa
Nimeacha

Ila as wapenzi ni kitu ambacho naona kinaniumiza na yeye ukitaka akose raha basi zungumzia kuhusu ndoa siku nzima atashinda hana furaha kwahiyo kauli yangu ya mwisho nilimwambia sitozungumzia tena kuhusu ndoa ye mwenyewe akiona sasa yuko tayari sawa

Ila ndani kwa ndani naumia sana, kuna leo na kesho hatuijui kesho yetu na bado tunazaa binafsi sipendi lakini sasa sina uwezo wa kulizuia hilo sitaki hata sherehe nimemwambia tuhalalishe tu hata watoto wae wa ndani ya ndoa na tuwe tumekamilisha angalau nusu ya dini inavyotaka

Kuna sababu ndogo ndogo pia
1.Historia yake na wanawake sio nzuri
2.Ana aibu
3.Hapendi kujichanganya na yupo kivyake vyake na maisha yake
4.Hapendi complications

Mkigombana uwaga unaongea kauli gani?Ushwahi msaliti hata kama unahisi hajui?

Kuna kosa kubwa ulifanya nalo ni kukubali kuishi nae nyumba moja kabla hajakuoa mapema sana naelewa inawezekana unalifanya hivyo sababu ya mapenzi lakini kadri ambavyo ni rahisi mtu kupata huduma zote za kijinsia basi ni kazi kwake kuwaza kujiingiza kwenye ndoa hasa km ana vitabia vya hapo juu.Its normal kabisa

By the way km Mna amani na furaha just be happy tu na fanya wajibu wako kwake.Usijiumize kichwa sana

Mi nitakupa mfano hai mwanamke niliyemuoa mimi nilidumu nae kwenye mahusiano kwa miaka 7.Alipokuw ananiuliza km nitamuoa mi nikimwambia wazi bado sijawaza kuoa na siwezi kukuhidi nitakuoa ila nakupenda ndo mana tumedumu mok sasa.Sometimes nilikuwa nampa kavu usinipangie,sikutaka kuoa sababu nilikuwa sijisikia kuoa na sipo tyr.Pesa nilikuwa nayo na mwanamke sahihi alikuwepo yeye ili nilikuwa sijisikii kuoa na sitaki kuambiwa kuhusu ndoa in fact hata mimi nilimwambia ukiona huwezi katafute ndoa ila usiniambie habari za ndoa.Siku moja isiyo na jina niliwaza kuoa haikuchukua miezi 3 nikalipa mali na haikupita miezi mitatu nikaoa.Mama angu mzazi alijua masihara sasa kwanini nilioa ni kwasababu niliona ni mda sahihi wa kuoa.Na kipindi namuoa mke wangu alikuwa kaacha kabisa kuniambia nimuoe niliamua mwenyewe kwa akili zangu timamu.

Usilazimishe ndoa hata usiwaze kama ipo ipo tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom