Naishi na mke ambaye sina mapenzi nae nifanyeje?

wa ukenyege unajua hawa vijana kabla ya kuoa huwa kunakuwa na expectation sasa wakizikosa wanaanza kulalamika.no perfect marriage in this world.
Mkuu unaona eee! Yaani nilishaliona nikuamua tu kuweka ubabe chini na kuridhika huku ukimtunza vizuri na kumwelewesha vizuri uliyenaye!! Hakuna kitu kizuri kama kumtoa ushamba uliyenaye na hatimaye akaja kuwa msaada kwako, you must be proud and respect one another. Huyu mkuu amepost lakini hajasema ni kitu gani kinachomfanya asimpende, pengine ni ule ushamba wa kijijini ambapo wakati mwingine mke wake mpendwa anayaacha nje manyonyo bila kuyasitili au anakuwa mchafu mchafu kiaina huku yeye mwenyewe haionyeshi kukereka. Kama anasoma huu uzi wake, ajitahidi kumuweka sawa huku akinunulia vitu vikali na kumpa outing za nguvu kila weekend akimuonyesha wanawake wengine wanaonekanaje!!
 
Mkuu nafikiri tatizo lako umeanza kufanya compare and contrast.itakusumbua sana hiyo attitude uliyoitengeneza kichwani mwako baada ya kutoka chuo.ila waulize kwanza wenye wake walioenda shule na mkwanja na stutus yao iko juu wakuambie.inshort kuna watu wanatamani miaka irudi nyuma akajiolee kabint ka kijijini awe anakaa nyumbani na kumlelea wanae tu kutokana na maisha ya ndoa anayoishi. ninachoweza kukushauri ni kuwa jitahidi kumweka mwenzio hiyo level unayofikiri kwako ndio sahihi na ndio kigezo cha mwanamke unayemwazia kwa sasa.
Hapo ndo nahisi msingi wa tatizo ulipo!! Huyu jama ningepata bahati ya kukutana asijaribu kumuacha!! May be he is still too young kiasi kwamba kauzoefu kamahusiano kanamsumbua!!
 
Nenda ukaombewe hilo ni pepo, hata siku moja hutampata aliyekamilika, utaendelea kuoa na kuacha. Mf. ukioa mwanamke kwa kupenda miguu yake siku akipata ajali akakatwa miguu utamuacha? Jitahidi sana upate maombi ili hilo pepo likemewe na kukuacha
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana uliamua kuishi kwa kuogopa wana kijiji.

Me naona humtendei haki huyo dada sababu ungesema mapema.

Unasikitisha sana hadi mtu una zaa nae ulitegemea nini sasa,

Piga chini mkuu....kumbuka ndoa ni for life mkuu,huwezi kukaa na mtu ambaye moyo hauridhiki for the rest of your life.....inauma na huwezi kumweleza mtu akakubali,lakini kuzidi kuchelewa unaongeza tatizo....BWANA NDOA NI KTU KINGINE...UNATAKIWA UWE 100% SATISFIED KABLA HUJAMUOA MTU....ASIKUDANGANYE MTU!!!
 
Mh apo chacha,,, sasa why bro?.hapa kukupa ushauri kaZi ila mm naamini.mapenz huwa yanakufa pia n watu kupeana talaka sasa kama unahisi humpendi tena mwambie usimtese bcz ukimtesa utabeba jukumu kwan nae ana deserve happy ,au jaribu kurekebisha zungumza nae nn hupendi na abadilike la no changes then unafanya maamuzi yako
 
kikubwa bwana kaka muulize huyo mkeo kama nae bado ana mapenzi kwako kwani inawezekana na yeye mapenzi yameisha kama wewe, kama ni hivyo kumbe itakuwa rahisi sana wewe utaenda zako na yeye ataenda zake! ila kama bado anakupenda basi nae anateseka sana,usimuache vumilia,
 
Piga chini mkuu....kumbuka ndoa ni for life mkuu,huwezi kukaa na mtu ambaye moyo hauridhiki for the rest of your life.....inauma na huwezi kumweleza mtu akakubali,lakini kuzidi kuchelewa unaongeza tatizo....BWANA NDOA NI KTU KINGINE...UNATAKIWA UWE 100% SATISFIED KABLA HUJAMUOA MTU....ASIKUDANGANYE MTU!!!

mkuu majany uje upate kinywaji. Nakuunga mkono. Kweli linapofika suala la ndoa inabidi uridhike na huyo mtu kwanza. Mshkaji inawezekana alipofika chuo akaanza mambo mengi, kurudi bush anamuona wake yupo tofauti na wale wa chuo. Kama anaweza jifunza kumpenda tena ni bora afanye hivyo otherwise apige chini fasta.
 
Last edited by a moderator:
ok bro nimekupata
Tatizo kubwa ni la kisaikolojia inaonekana una mwanamke mwingine zaid ya huyo.
Je wakati unaanza naye mlikubaliana nini au mlikuwa unajipatia burudani.
Kweli ni kwamba ukiendelea kuish naye unaumia moyo piga nikushauri +255757788363
 
Mkubwa je Huyo Mwanamke mala ya kwanza mlikutana mazingila gani ? Ushauri wangu kwako inaonyesha Mkubwa Huyo hukumpenda ulimtamani tafuta Mwingine unaempenda si kumtamani Hilo ndo suluhisho la tatizo
 
mkuu majany uje upate kinywaji. Nakuunga mkono. Kweli linapofika suala la ndoa inabidi uridhike na huyo mtu kwanza. Mshkaji inawezekana alipofika chuo akaanza mambo mengi, kurudi bush anamuona wake yupo tofauti na wale wa chuo. Kama anaweza jifunza kumpenda tena ni bora afanye hivyo otherwise apige chini fasta.

hahahaaaaa...CAtherine ntapitia bwana...niandalie ndovu bariiiidiiiiiii...lakini ukweli ndio huo.....
 
"2006 ulimpenda kwa kiasi fulani" ni nini kilivutia kwake hadi ukamuwazia kuishi nae kama mke na mume hapo baadae,,,, find that thing,, halafu also try to find out if SHE still has love for you bcoz inawezekana mapenzi yameisha kwa upande wake pia na ndo maana huoni kile alichokuonesha miaka hiyo ambacho kilikuvutia wewe,,, relationships are never easy believe me either iwe kwenye ndoa ama nje ya ndoa..... lakini kama you have both fallen out of love for each other DONT FORCE THE RELATIONSHIP.....ni hayo tuuu,, pole hayo yote ni mapito ya hapa duniani...
 
Habari ndg zangu wadau wa JF, ndg zangu ni takribani miaka miwili ss naishi na mwanamke ambae nilizaa nae tangu mwaka 2006 kabla sijajiunga na chuo kikuu, baada ya kumpa ujauzito niliamua kumtolea barua ya posa kipindi kiukweli nilikuwa nampenda kwa kiasi fulani nikiwa na imani kuwa nitaishi nae km mume na mke hapo baadae. Wakati mwenzangu alikuwa ameshaacha shule baada ya kufeli mtihani wa kidato cha pili na tayari nilikuwa nimemaliza kidato cha sita. Hatimaye 2007 nilifanikiwa kujiunga UDSM na muda wote wa masomo yangu sijahi kufikiria kuachana na huyu msichana kabisa. Lkn baada ya kuhimu chuo na kuja kuonana nae huko kijijini nilikomwacha ktk maongezi ndani ya siku kadhaa nikaanza kugundua nilifanya makosa sana kumkeep hasa baada ya kugundua kuwa ana mapungufu mengi ambayo pengine hayawezi kulekebishika kabisa kiasi cha kunifanya niendelee kuamini kuwa lilikuwa chaguo sahihi kwangu. Hata hivyo nililazimika kumchukua na kuishi nae mjini baada ya kugundua wanakijiji walishaanza kuwa na mtazamo hasi kwangu, hivyo nikamchua ili kuwaridhisha wanajamii. Vibaya zaidi nazidi kuyaona mapungufu zaidi na zaidi, kiasi cha kunifanya nisiwe na furaha ya kuendelea kuishi nae na mara nyingine najikuta namfanyia vituko vya kukosa upendo kabisa kwake. Kumrudisha naona noma kwani km mjuavyo watu watasema coz tumepishana elimu kiasi kikubwa. Naishi nae simpendi kutoka moyoni. Wadau naomba ushauri kwani hili ni suala zito sana kwangu sijafunga nae ndoa.................

BEFORE MARRIAGE OPEN YOUR BOTH EYES,AFTER IT CLOSE ONE.waliosema haya walikuwa na maana sana!
 
hebu rudisha hisia kama ulivompenda mara ya kwanza mpaka akapata ujauzito wako, na mlipendana mpaka mkafikia hatua ya kuzaa, cha muhimu muweke soap soap then mpeleka shule, huwezi jua huyo ndo anaweza kuwa mwanamke wa maisha yako!!
 
Mkuu chaguo la kwanza ni chaguo la MUNGU, nakuhakikishia kuwa, unaweza ukapata mwanamke mwingine na yeye utapoteza upendo kwake. Tulia mwombe MUNGU, jaribu kukaa nae mueleze mapungufu yake Mungu ni mwema atatenda. Hakuna jambo ambalo MUNGU analiheshimu kama ndoa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom