Habari ndg zangu wadau wa JF, ndg zangu ni takribani miaka miwili ss naishi na mwanamke ambae nilizaa nae tangu mwaka 2006 kabla sijajiunga na chuo kikuu, baada ya kumpa ujauzito niliamua kumtolea barua ya posa kipindi kiukweli nilikuwa nampenda kwa kiasi fulani nikiwa na imani kuwa nitaishi nae km mume na mke hapo baadae. Wakati mwenzangu alikuwa ameshaacha shule baada ya kufeli mtihani wa kidato cha pili na tayari nilikuwa nimemaliza kidato cha sita. Hatimaye 2007 nilifanikiwa kujiunga UDSM na muda wote wa masomo yangu sijahi kufikiria kuachana na huyu msichana kabisa. Lkn baada ya kuhimu chuo na kuja kuonana nae huko kijijini nilikomwacha ktk maongezi ndani ya siku kadhaa nikaanza kugundua nilifanya makosa sana kumkeep hasa baada ya kugundua kuwa ana mapungufu mengi ambayo pengine hayawezi kulekebishika kabisa kiasi cha kunifanya niendelee kuamini kuwa lilikuwa chaguo sahihi kwangu. Hata hivyo nililazimika kumchukua na kuishi nae mjini baada ya kugundua wanakijiji walishaanza kuwa na mtazamo hasi kwangu, hivyo nikamchua ili kuwaridhisha wanajamii. Vibaya zaidi nazidi kuyaona mapungufu zaidi na zaidi, kiasi cha kunifanya nisiwe na furaha ya kuendelea kuishi nae na mara nyingine najikuta namfanyia vituko vya kukosa upendo kabisa kwake. Kumrudisha naona noma kwani km mjuavyo watu watasema coz tumepishana elimu kiasi kikubwa. Naishi nae simpendi kutoka moyoni. Wadau naomba ushauri kwani hili ni suala zito sana kwangu sijafunga nae ndoa.................