Solution ni watu wapimwe kwa gharama za serikali... Wa roll-out mass-testing mitaani hasa hizo sehemu mnazohisi maambukizi ni makubwa...
Wanaoonesha dalili ndo wapelekwe karantini...
Ukiwafungia watu ndani bila kujua nani ana hali gani sioni kama utakuwa umesaidia chochote...!
Unakumbuka yaliyotokea India?? Wahindi walilazimima kutembea kwa miguu kutoka mijini kukimbilia vijijini...
Mkilazimisha lockdowns hapa kwetu mtakuwa mmewakimbiza watu wengi sana kurudi vijijini katika hali isiyo ya kibinadamu kabisa!!
Mkuu kumbuka tunayo maabara moja tu yenye uwezo wa kufanya huu upimaji. Aliyekwisha pimwa anaweza ambukizwa dakika au sekunde chache baada ya kupimwa. Kwa maana ya kuwa validity ya matokeo ya kupimwa a few seconds baada ya kupimwa may be absolutely null and void.
Unaonaje hili, kwani linafanikiwa katika maeneo mengine kama yetu? Typical case ni Rwanda, nchi maskini na yenye raslimali duni kuliko sisi:
Huko Rwanda, uwezo tofauti wa kiuchumi wa wanajamii umezingatiwa katika kipindi chote cha lockdown (wako siku takribani ya 20 zinabakua 9):
1. Wanaohitaji msaada kabisa (in totality) wametambuliwa na wanasaidiwa.
2. Wanaohitaji msaada kiasi (partial) wametambuliwa na wanasaidiwa.
3. Wanaojitosheleza wametambuliwa.
4. Wenye ziada na nia kiasi cha kuweza kusaidia wengine wametambuliwa na wanakaribishwa kufanya hivyo.
Kama mfano Azam Rwanda imechangia tani 20 za chakula (juzi) kuunga mkono juhudi kule. Mifano iko mingi.
Lengo ni kuona watu wanasalia majumbani na waathirika wote wanatambulika kwa hatua stahiki. Ndiyo maana wao hadi sasa hata vifo vya Corona hamna. Wanaanza matunzo (care) mapema. Kasi ya maambukizi tayari wameidhibiti vilivyo.
Katika mazingira kama haya mkuu ningeshukuru kufahamu kwa nini bado tunadhani lockdown itakuwa na madhara.
Ni kweli kuwa hatutakula ambacho tungependa kula kwa kipindi hicho. Ila ni wazi kuwa tunaweza kujipanga asife mtu kwa njaa. Tukamaliza salama na ugonjwa ukadhibitiwa.
Mawazo yako mkuu yatakuwa ya msingi mno katika kuchangia kuona uelekeo upi ni bora kabisa hata kama wewe na mimi hatuna influence yoyote.
Au siyo mkuu?