ngota wa nzambe
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 120
- 135
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inapitia kipindi cha ukata uliokithiri kwa sasa kiasi kwamba, inashindwa mpaka kugharimia baadhi ya vitendea kazi muhimu kama gloves, mabomba ya sindano (syringes) na vingine vingi. Hali hii imepelekea ubora wa huduma kuwa hafifu sana.
Pia ulipaji wa stahiki za watumishi kama night duty allowance na overtime umekuwa wa kusuasua mno jambo linalowavunja moyo wafanyakazi wengi, wengine mpaka kufikia hatua ya kukata tamaa na kuacha kazi.
Tunaiomba serikali iiangalie kwa jicho la karibu hospitali hii vinginevyo inaelekea kufa kabisa kwa sababu ya ukata.