Naishauri Serikali kupitia Wizara ya Afya kuitupia jicho Hospitali ya Mloganzila

ngota wa nzambe

Senior Member
Jul 28, 2015
120
135
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inapitia kipindi cha ukata uliokithiri kwa sasa kiasi kwamba, inashindwa mpaka kugharimia baadhi ya vitendea kazi muhimu kama gloves, mabomba ya sindano (syringes) na vingine vingi. Hali hii imepelekea ubora wa huduma kuwa hafifu sana.

Pia ulipaji wa stahiki za watumishi kama night duty allowance na overtime umekuwa wa kusuasua mno jambo linalowavunja moyo wafanyakazi wengi, wengine mpaka kufikia hatua ya kukata tamaa na kuacha kazi.

Tunaiomba serikali iiangalie kwa jicho la karibu hospitali hii vinginevyo inaelekea kufa kabisa kwa sababu ya ukata.
 
Hali hiyo hiyo ipo ktk hospital na vituo vingi tu vya Afya nchini. Naskia had uchaguz upite.
 
Serikali haiipendi hii Hospital maana ikifanya vizuri sifa atapata JK. Wanaona waipe hela ila ya Chato tu
 
Cell kali pamoja na majivuno yote yanayotolewa na viongozi wake kwa kuigiliziana lakini ukweli ni kwamba kwa sasa haina fedha. Hilo halina ubishi na inaweza kufikia kipindi ikajitawaza kwa kutumia gunzi.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila inapitia kipindi cha ukata uliokithiri kwa sasa kiasi kwamba, inashindwa mpaka kugharimia baadhi ya vitendea kazi muhimu kama gloves, mabomba ya sindano (syringes) na vingine vingi. Hali hii imepelekea ubora wa huduma kuwa hafifu sana.

Pia ulipaji wa stahiki za watumishi kama night duty allowance na overtime umekuwa wa kusuasua mno jambo linalowavunja moyo wafanyakazi wengi, wengine mpaka kufikia hatua ya kukata tamaa na kuacha kazi.

Tunaiomba serikali iiangalie kwa jicho la karibu hospitali hii vinginevyo inaelekea kufa kabisa kwa sababu ya ukata.
Pamoja na kupungukiwa pesa kuna uradimu mwingi kwa viongozi ,serikali tupia jicho mloganzila hospitali!
 
Tumeipenda wenyewe .......tititi
Tumeichagua wenyewe.......tititi
Wacha tuisome namba eee
Ccm mbele kwa mbeleeeee
 
Back
Top Bottom