Naishauri Serikali ije na Programu Maalum kwa Wanafunzi wanaomaliza Darasa la Saba Kipindi kirefu wakisubiria Matokeo yao

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Wanafunzi kumaliza Mitihani yao ya Darasa la Saba Mwezi Septemba na Kuwaacha tu wanarandaranda Mitaani hadi Mwezi Disemba majibu yao yakitoka ni Hatari mno Kwao.

Nitoe Kongole kwa baadhi ya Shule ambazo zilishaiona hii Hatari na kwamba Wanafunzi wao wakimaliza tu Darasa la Saba kuna Program huwa wanawaandalia ili kuwafanya wasiwe wanazurula Mitaani.

Niiombe Serikali ije ya Ubunifu wa Program Maalum ambayo itawafanya hawa Wanafunzi wanaomaliza Darasa la Saba wawe wanaifanya / wanaifuata mpaka pale Matokeo yao yakitangazwa ili Kuwaepusha na Mabaya mengi ambayo huwa yanawakuta.

Nimeshashuhudia Mabinti / Wasichana wanaomaliza Darasa la Saba Wakimimbika ( wakijazwa Ujauzito ) na Wanaume tena kwa Kununuliwa tu Muhigo ya Jero Jero na Bagia na Kukatisha rasmi Safari yao ndefu ya Kitaaluma.

Nimeshashuhudia Vijana / Wavulana wanaomaliza Darasa la Saba wakianza Kujiingiza katika Makundi mabaya ya Uhalifu huku wengine wakifanywa ni Mawakala wa Kuuza Bangi kwa Kulipwa Chips Soda tu na hatimaye wananogewa huko na kutotamani tena kuendelea na Masomo.

Nitashukuru huu Ushauri wangu ukifanyiwa Kazi na Wadau na Jambo lenye Tija Kwao ( hawa Vijana na Mabinti ) zetu Wapendwa likifanyika.

Nawatakia Mitihani mwema wote leo.
 
Watoto wa sasa malezi yao ni magumu sana, wamezungukwa na majaribu mengi.

Hiyo program pengine ikachangia kuwaharibu pia.

Wazazi nao wako bize hawajui hata watoto wanacheza michezo ipi

All in all anayekuza ni Mungu
 
Yaani wazazi wa siku hizi wamekua wavivu kulea wanao, serikali ilee watoto wenu paka lini? imewapa elimu bure matibabu bure, na kulee watoto wenu kwa miezi mitatu mshindwe?
 
Nimeshashuhudia Mabinti / Wasichana wanaomaliza Darasa la Saba Wakimimbika ( wakijazwa Ujauzito ) na Wanaume tena kwa Kununuliwa tu Muhigo ya Jero Jero na Bagia na Kukatisha rasmi Safari yao ndefu ya Kitaaluma.

Ulichuka hatua gani kuwaepusha na hadha hiyo?

Jukumu la malezi ni wazazi, kujua mwanao unamuandaje kupitia uwezo na matamanio aaliyonayo.

Kuna maisha nje ya darasa extra
Curriculum, kuijua jamii yake na fursa zilizopo. Biashara, kilimo, ufugaji n.k

Usipowajibika kumlea mwanao vyema jamii itamulea vile inapenda.

Timiza wajibu wako Baba na Mama
 
Back
Top Bottom