Nairudisha Bandari ya Bagamoyo ukumbini, nikiiunganisha na ujenzi wa Bomba la Mafuta (EACOP)

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Ujenzi wa Bomba la Mafuta toka Hoima hadi Tanga, ni "Joint Venture", na tumekwishashuhudia hatua zote zinazohusika na mradi huo zinavyoandaliwa na kupata maelezo namna mradi utakavyotekelezwa.

Haya mambo kwa sehemu kikubwa yamewekwa wazi, na hatujashuhudia kelele nyingi zikipigwa toka kwenye makundi yenye maslahi binafsi na mradi huo.

Nimejaribu kuwaza, kuna utofauti gani katika utekelezaji wa mradi kama huo, na huu wa Bandari ya Bagamoyo? Haiwezekani hatua zikachukuliwa, tukitumia kama mfano hatua zilizopitiwa kwenye huu mradi wa bomba la mafuta?

Yanayosisitizwa kuhusiana na mradi wa bandari ni umiliki wa bandari hiyo na wawekezaji, na masharti husika wanayotoa kuwa ya siri au mkanganyiko, maana hakuna anayejua masharti yanasemaje hasa!

Mradi wa bomba la mafuta, ardhi ya Tanzania itakuwa ikilipiwa, tozo za kodi zinafahamika

Sasa wenye kujua, elezeni kama kuna utofauti mkubwa sana kati ya miradi hii miwili kiasi kwamba masharti yake hayawezi kulingana kwa vyovyote.
 
Back
Top Bottom