Nairudia; Stori ya kweli ya kijana Ayubu

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,212
2,809
Habari Wakubwa, natumai hakuna mdogo humu

Utangulizi
Kipindi cha nyuma nilileta stori kuhusu jamaa mmoja aitwaye Ayubu. Kutokana na uandishi duni nilionao pamoja na hadithi yenyewe kuwa ni ya kimapokeo zaidi (kwani nilifanya kuhadithiwa- sijaishuhudia) basi wengi waliona kama nimeleta CHAI kama chai nyinginezo. Hadithi hii ni ya kweli ila hata mimi nimefanya kuhadithiwa tu na rafiki yangu ambaye kipindi cha nyuma huko yeye na huyo Ayubu walikuwa marafiki hasa.

Kwanza nilimuonesha picha (huyo jamaa yangu) miongoni mwa avatars humu JF ndo akasema kuwa anamjua huyo aliopo kwenye hiyo avatar. Nikamwambia acha uongo akaniambia "ni kweli tena nimesoma nae Mandaka tena alishinda umiss chuoni tukawa tunamuita Miss Mandaka". Baada ya hapo akanipa stori hiyo sasa akasema nimuulize huyo miss Mandaka na nimtajie jina la aliyenipa stori lakini nimemcheki PM yake imefungwa

Sasa nitairudia hapa vizuri kabisa na nitaihadithia kama ambavyo huyo rafiki yangu alivyokuwa amenihadithia

"Nilikuwa na rafiki yangu aitwaye Ayubu ambae tulisoma wote shule. Ayubu na mimi tulikuwa ni vinara katika somo la Biology nakumbuka tulichuana vikali na kuachana kwa maksi ndogo sana kwa kila mtihani. Ilikuwa kama siyo kugongana maksi basi akinizidi yeye lazima kuna kipindi nitamzidi mimi yaani kama tupishana kwa zamu

Tulipohitimu elimu ya Sekondari 2012 ikaja habari ya kusahihisha upya mitihani matokeo yakarudiwa, mara ikaja kuwa waombe vyuo vya kati wenye sifa basi kwa pale shuleni kwetu mmoja tu ndiye alifaulu kwenda advance na wengine tulikuwa wachache sana wenye hizo Div.IV nzuri nzuri tukatuma maombi. Kwenye kuchaguliwa tukajikuta tumepangwa chuo kimoja tena na rafiki yangu Ayubu.

Tuliripoti vizuri pale Chuo Cha Ualimu Mandaka na ndio mwaka wa kwanza kinapokea wanafunzi mchanganyiko (wa jinsi zote). Urafiki wetu na Ayubu uliimarika zaidi kwani tulikuwa tukienda mesini basi tunakula meza moja, tunashea mambo mengi pamoja. Nakumbuka ilikuwa kama mimi nimewahi kufika kabla yake basi nilimchukulia chakula na kutangulia nacho kwenye meza yetu, kadhalika na mimi nikichelewa.

Tukiwa angali wageni kabisa Ayubu akaniita siku hiyo akaniambia kuwa ana jambo ambalo anataka kuniambia ila akaomba iwe siri yangu na yake.

Baada ya kumhakikishia kutunza siri yake akasema kuwa yeye anataka kuacha chuo maana anaona fedheha kuna video imevuja ikimwonesha yeye aki ambarutiwa na mwanaume mwenzake. Binafsi nilishtuka sana akasema kuwa siyo jambo geni kwani wengi pale chuoni wameipata video hiyo na inazagaa mitandaoni labda kasoro mimi tu ndo sijaiona. Akasema kuwa yeye hajawahi wala hatarajii kabisa kufanya mambo hayo ila itakuwa kuna waliotumia sura yake ku mkono wa baunsisha na nilipomhoji zaidi ili anitajie alipoiona video hiyo akakataa katakata akasema haina haja ndo atazidi kufedheheka

Basi nilimsihi sana juu ya jambo lile kuwa avumilie tu asiache chuo lakini akasisitiza kwamba ni lazima muda wowote kuanzia tulipozungumza angeweza kutoroka tu kwani hangeweza kuvumilia

Muda wa kulala bweni lao ni tofauti na la kwetu sasa ilipofika asubuhi nimefika mesini yeye hakuwa amefika bado nikamchukulia chakula kama kawaida yetu. Nilisubiri sana mpaka mimi nikamaliza kula hakutokea. Mpaka inafikia naondoka mesini Ayubu hakutokea basi ikawa nikizunguka zunguka lazima nije nipige jicho pale ila cha kushangaza chakula kile nilikukuta vilevile na palepale.

Jioni ilipofika kaka yake wa Ayubu ananipigia simu anauliza Ayubu kafanya nini chuoni maana kaendaa tu pale anasema hataki chuo sababu anazotoa hazieleweki nikakosa cha kumjibu. Baada ya hapo akampa mwenyewe nikamuuliza akasema kuwa alitoroka usiku kwa kuruka fensi akakanyaga ya mguu mpaka nyumbani

Kilichonishangaza ni kwamba alivyokuwa anaongea akiwa nyumbani ni tofauti na tulivyokuwa chuoni yaani hakuwa tena na ule unyonge wala hakugusia tena habari ile aliyokuwa ameniambia ila akasema tu kuwa asingerudi tena chuoni amechoka kusoma. Nilimuuliza kuhusu vitu vyake maana aliondoka yeye kama yeye tu akaniambia hana mpango navyo

Baada ya hapo ndio mimi nikawa nasubiri labda nisikie wanachuo wakizungumza kile alichoniambia lakini sikusikia yeyote hata wale masela wa karibu. Nilichukua daftari nikatumia na tranka lake jipya kabisa nikalihifadhi

Sasa kuna wale wanaoenda nyumbani kwa dharula mbalimbali wakawa wakirudi wanatuambia kuwa jamaa kawa chizi pale mtaani nikawa siamini hadi siku niliyokwenda likizo. Nilimkuta Ayubu kachafuka anarandaranda tu pale barabarani. Nilihofia kumsogelea labda angenidhuru au kunikimbia lakini nikajikaza nikamsogolea kwa kumnyemelea. Nilipomkaribia nilimuita naye kunigundua akanitaja jina langu akanichangamkia sana lakini akiwa kama mwenye haraka hivi.

Nilimwambia kuwa asiwe na haraka akasema anashida ya shilingi miamoja nilishangaa nikampa elfu mbili nikimwambia akale chakula ila nilishangaa zaidi kwani baada ya kupokea tu ile elfu mbili ikawa kama hatujakutana. Aliniacha pale kiaina kwa dizaini kama nilikuwa naongea mwenyewe tu pale, yaani ilikuwa kama nampotezea muda vile

Kufikia hapo ndo nikaamini kweli jamaa kawa chizi (mwendawazimu sijui kichaa) nikivuta picha ya alichokuwa amenihadithia mpaka alivyotoroka toroka chuoni. Fensi ile ilikuwa ni ndefu sana na chuoni kulikuwa na walinzi muda wote. Chuo kilipo mpaka huko alipokanyaga ni parefu na panatisha lakini katembea usiku saa 7. Mambo ya Ambaruti aliyonihadithia sikuwahi kuyasikia kwa mwingine yeyote zaidi yake yeye mwenyewe tena nashukuru maana sikufanya upelelezi wa kuropoka kwa wanachuo kile alichoniambia.

Kitu ambacho sijajua hadi leo ni je yule jamaa alirogwa, madawa au ajali kama ajali nyingine japokuwa kuna waliosemaga wanamkuta anakula mjani akiwa hivyo hivyo mwendawazimu"

Mwisho
 
ni miaka nane sasa tangu hiyo 2012. vipi umeshawai kukutana na rafiki yako ayubu hivi karibuni? au urafiki uliishia kwenye kumtunzia tranka tu
 
Asikwambie mtu, kumshuhudia mtu wa karibu akiharibikiwa akili inauma sana, mi imenitokea kwa watu watatu, mmoja nilisoma nae shule ya Msingi, mwingine sekondari, na mmoja alikuwa mlinzi kibaruani japo ameanza kurecover sa hivi, na kikubwa ni uchawi wa kurogwa amna kingine.
 
Aiseee ilichukua Muda gan yeye kuwa chizi baada ya kutoka Chuo ?
Kuwa chizi nadhani ni kipindi kilekile alipokuwa anaropoka mambo ambayo hayapo... labda ungeuliza kuchanganyia kabisa na kuanza kuoneaha dalili za uchizi ambapo jamaa alisema washkaji kwenye likizo walipokwenda Same walimuona akiwa rodini
 
ni miaka nane sasa tangu hiyo 2012. vipi umeshawai kukutana na rafiki yako ayubu hivi karibuni? au urafiki uliishia kwenye kumtunzia tranka tu
Huo ni mwaka wa kuhitimu elimu msingi boss... chuo ni 2013... yeye mara ya mwisho kukutana sijajua ni lini
 
Back
Top Bottom