NAIROBI, KENYA: Wapigakura waishtaki Tume ya Uchaguzi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Nairobi, Kenya. Hatima ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya urais itajulikana kesho pale Mahakama ya Juu itakapokaa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na wapigakura watatu wakitaka uahirishwe.

Naibu msajili wa mahakama, Daniel Ole Keiwua amewataka walalamikaji hao Khelef Khalif, Samwel Mohochi na Gacheke Gachihi kuupatia notisi upande wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) ifikapo saa 12:00 jioni leo.

Wapigakura hao wameishtaki IEBC na mwenyekiti Wafula Chebukati. Chebukati anatarajiwa kujibu mashtaka dhidi yake ifikapo saa 2:00 asubuhi ili kuwezesha shauri kusikilizwa saa 4:00 asubuhi.

Huenda watu wengi wakafika kusikiliza shauri hilo hasa ikizingatiwa Serikali imetangaza Jumatano kuwa siku ya mapumziko ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kwa maandalizi ya uchaguzi wa marudio Alhamisi.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang'i ameweka notisi hiyo leo katika Gazeti la Serikali. Pia Alhamisi ya Oktoba 26 itakuwa siku ya mapumziko.

Wakenya watakwenda kwenye vituo kuchagua kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi mkuu wa muungano wa upinzani (Nasa) Raila Odinga ingawa alitangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo wa marudio.

Badala yake, Raila amewataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo na kampeni zake kubwa kwa sasa ni kuhakikisha haufanyiki kwa madai Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeshindwa kutekeleza marekebisho muhimu ambayo amekuwa akitaka yafanyike tangu yalipobatilishwa matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.

Nasa waliopanga kuandamana leo na kesho, wamesema watafanya mama ya maandamano yote Alhamisi.

- Mwananchi
 
Kuendelea kuahilisha uchaguzi kunachelewesha maendeleo yao wafanye wajue mbivu na mbichi kama Odinga kasusa wampigie aliyepo maisha ya wakenya yawe na amani kuliko hivi sasa wanaishi roho juu juu
 
Back
Top Bottom