Nairobi, Kenya: Tundu Lissu azungumza na kula chakula kwa mara ya kwanza

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Hali ya Mbunge na Wakili Msomi mwenzangu Tundu Lissu imeimarika baada ya leo,kwa mara ya kwanza,kuzungumza na kula chakula.

Taarifa kuhusu jambo hilo imetolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe aliyeko Nairobi Kenya anakotibiwa Lissu.

Kwa mujibu wa Mbowe,hali ya Lissu inaendelea kuimarika. Lissu anatoa salamu kwa wananchi wote. Mbowe anasema taarifa rasmi zitatolewa nao waliopo Nairobi.

Mbowe pia amekanusha kuwa Lissu hana infection katika kifua chake kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii

Let us pray more for Lissu!

Chanzo: ITV Habari
 
Back
Top Bottom