Nairobi, Kenya: Mwanafunzi aliyefukuzwa shule kwa kukosa Karo, ajinyonga

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha masuala ya Habari cha Shauri Moyo, jijini Nairobi, amejiua baada ya kupita wiki mbili tangu arudishwe nyumbani kwa kukosa ada.

Mwanafunzi huyo Frederick Kinyanjui (22), ambaye alikuwa mwaka wa pili katika chuo hicho kwa masuala ya Habari (Multimedia) alikutwa amening'inia darini nyumbani kwao juzi jioni.

Alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Polisi wa Kaunti ya Buruburu OCPD, Godfrey Mayiek, amesema sababu hasa za Mwanafunzi huyo kujinyonga hazijafahamika bado na hakuacha ujumbe wowote.

Mama wa marehemu aliuambia mtandao wa Citizen kuwa, Kijana wake ni kweli alirudishwa nyumbani kutokana na kukosa Karo, lakini hajafahamu hasa kwanini amejiua.

Chanzo: Azam news
 
Nilikuwa nafikiri mambo haya ni ukanda fulani mwa Tanzania, kumbe hata huko
 
Back
Top Bottom