Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mwanamke huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na mapema Jumatano katika mtaa wa Kayole.
Gazeti la kibinafsi la Daily Nation linasema mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wanne wa kiume pale walipofumaniwa na polisi wakitekeleza wizi katika eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole
Anadaiwa kufyatulia risasi maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao wakauawa huku wenzao wakifanikiwa kutoroka.
Taarifa katika gazeti la Daily Nation inasema polisi waliwaandama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzao kupitia Whatsapp kwamba majambazi hao waliokuwa wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa.
Chanzo: BBC