Nairobi flyovers challenge kwa mawaziri wa ujenzi?

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,458
Jamani, Mwakyembe na waziri wako, naomba mpitie hapa muone jinsi Nairibo inavyofanya kupunguza foleni. hizi flyovers hata south africa sidhani kama sipo, wala cairo wala Lagos au Abuja.....mnajifunza nini?
 
Weka picha tuone hizo flyovers za aina gani ambazo haziwezi kuwa RSA au Egypt!!! Anyway, za TZ ni za maneno ya kampeni tu. Kwa sasa washa sahau mpaka 2014 vuguvugu la kampeni likianza.
 
hao wakenya wanazo project kama sita, sio kamoja au viwili...na sisi tunataka selikali ifanye hivyo haraka...

1. Tunataka fly over ya kueleweka pale Ubungo mataa kama hii http://www.arabcont.com/projects/Images/moharem-2-l.jpg

2. Tunataka fly over ya kueleweka pale buguruni na ingine Tazara mataa kam ahii http://forum.bauforum24.biz/forum/index.php?act=Attach&type=post&id=61594

3. Tunataka fly over ya kueleweka pale Magomeni mataa. kama hivi http://farm5.static.flickr.com/4082/4903387119_e324c2fc58_b.jpg

4. Tunataka fly over ya kueleweka pale Moroco kinondoni mataa kama hivi http://i23.photobucket.com/albums/b365/luv_nudao/16.jpg

5. Tunataka fly over ya kueleweka pale Fire kuingia mjini kama hivi http://farm5.static.flickr.com/4152/4947217312_026a169cb5_z.jpg

6. Tunataka kitu cha kueleweka pale mwenge kama http://i23.photobucket.com/albums/b365/luv_nudao/6.jpg

KWA KIFUPI, TUNAHITAJI PIA watuwekee taa za barabarani za kumulika mwanga, si za kuongoza magari, ziwe za kutosha na zenye urembo ili kulipamba jiji letu. Selikali ihakikishe inaweka kitu cha kueleweka, project kama sita, kama nilivyoziweka hapo juu, moja hadi sita zote zifanyiwe kazi. sio kutuwekea kafly over kamoja tu halafu wanafikiri kila kitu tayari.
 
nimefurahi ulivyoainisha maeneo sita ya kuziweka hizo barabara. maeneo sita...ubungo, Tazara, buguruni, morroco, magomeni, fire kwenda muhimbili na posta barabara ambayo asubuhi foleni inaweza kuanzia magomeni mapipa hadi fire kule, na mwenge...
 
Jk aanze kujenga studio ya kisasa alizowaahidi wasanii wa Bongo Flavor kwanza.
Hizo ahadi nyingine eti sijui Kigoma kuwa Dubai na Mwanza kuwa Amsterdam of Afrika ni porojo za kampeni na ndio imetoka hadi 2014 wakati wa uchaguzi
 
Mimi sioni kama hizo flyover ndy mwarobaini wa kudumu, cha muhimu ni kuangalia solusheni sahihi na endelevu ya kupunguza foleni za magari!
Wenzetu walijenga flyover kitambo-na sasa wanagundua kuwa siyo ufumbuzi wa kudumu! Tuumize vichwa jamani........! Tusiangalizie kwa jirani tu, tukiwa na public transport inayoeleweka tutaondokana na mateso! Mpango kama wa wachina na mabasi yapitayo juu ya magari ni mpango wenye nuru zaidi kuliko flyover-ni mfano Tu. Bangua bongo
 
Jamani, Mwakyembe na waziri wako, naomba mpitie hapa muone jinsi Nairibo inavyofanya kupunguza foleni. hizi flyovers hata south africa sidhani kama sipo, wala cairo wala Lagos au Abuja.....mnajifunza nini?

egyp.jpg
Cairo
 
Jk aanze kujenga studio ya kisasa alizowaahidi wasanii wa Bongo Flavor kwanza.
Hizo ahadi nyingine eti sijui Kigoma kuwa Dubai na Mwanza kuwa Amsterdam of Afrika ni porojo za kampeni na ndio imetoka hadi 2014 wakati wa uchaguzi

Chonde chonde ijengwe barabara ya kuunga Kigoma na Tabora kabla ya hizo flying over au viende sambamba, Majambazi yanatutesa wenzenu, Magari hadi yasindikizwe na askari!!!! Barabara ikitengenezwa huko njia itakuwa na magari mengi hivyo majambazi watakimbia wenyewe.
 
Uwezo huo tunao ila kwasababu wachache wanataka wajinufaishe basi hizo flyovers itakua drama.
Barabara ya Tunduma-Sumbawanga hadi leo ni hadithi wkt nasikia BUSH alimwaga hela ijengwe.
Tangu UHURU hadi LEO Rukwa haijaunganishwa na mkoa wowote kwa lami,ni aibu.
 
Back
Top Bottom