Uchaguzi 2020 Naipongeza Ilani ya CCM ukurasa wa 29 mpaka 33, MgombeA ukishinda ivunje SCOUT, COASCO na Tume

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,012
8,360
Hakika Tanzania kumekucha, tusio wanasiasa tunaanza kupokea CV za walio tutaka tujiajiri rejeeni kauli zao walipo kuwa Bungeni.

Sina haja ya kurejea kauli zao,nimeisoma Ilani ya chama cha mapinduzi ukurasa nilioutaja mwanzo mwisho nao unajadiri yaliyofanywa na CCM kupitia serikali waliyoiunda 2015 mpaka 2020 kwenye kada ya ushirika

Ninaomba nawapongeza walio sema waliyafanya kwa asilimia 35% ni kweli ila zilizobakia ni porojo ambazo kimsingi kushindwa kufanikiwa kumeletezwa na uwepo wa Sheria za ovyo mfano sheria no 6 na nyingine Sheria hizi ni za ovyo nadhani zilitungwa na mijitu hisiyoelewa kabsa dhana nzima ya ushirika.

Sababu nyingine iliyopelekea washindwe pamoja na kuwa na Rais mzuri ni majungu,yaliyojaa Wizara ya Kilimo na ushirika kuanzia hata kwenye Ofisi ya Tume mpaka huku chini hata kwenye kada nyigine mfano coasco na scoult.

Sababu nyingine ni kukosa watendaji waaminifu na waadilifu wenye taaluma katika kada ya ushirika.

Mwisho niseme yaliyosemwa yatafanywa ni mazuri ila yafatayo yaongezwe

Kwanza Tume ya Maendelea ya ushirika ivunjwe ni kichaka hicho kimejaa siasa,na watu waliojaa majungu wengi wao mlio wateua mmeishia kuanglia vyeti vyao mfano mtu alikuwa mwalimu wa chuo cha ushirika anapewa nafasi kubwa kupitia Tume akishafika pale ni kuunda mtandao wa upigaji.

Pili Mdudu anaitwa sijui scoult huyu ameua vyama mchunguzeni muone.

Mwisho ni shimo la ulanguzi coasco ili nalo ni shimo la wizi mtupu ingawa mgombea wenu alishaelekeza lifutwe.
 
Ukifustilia kwa umakini lazima utakuwa ulikuwa mtoa huduma hasa wa Tume na umepigwa chini kwa kukosa sifa ndio maana unatolea hasira zako hapa
 
Back
Top Bottom