lil wayne
JF-Expert Member
- Apr 15, 2016
- 992
- 904
Binafsi ni shabiki damu wa Klabu ya Simba.
Ila napenda kuzungumzia swala fulani kwa jicho la kipekee kabisa ambalo mwana Simba wa kawaida hawezi kuliona.
Hii leo tumeshuhudia Yanga SC ikiumana na Medeama ya ghana. Kuna kitu numejifunza mimi kama shabiki wa Simba.
Licha ya Yanga SC kufanya ovyo katika hatua hii ya Kombe la Shirikisho wanaonekana sio wa level yetu (Simba) kwa sasa.
1. Kama kuna Klabu ambayo Mungu amepanga ije kubeba Ndoo ya Michuano mikubwa ktk miaka ya usoni basi itakuwa ni Yanga na wala sio Simba. Hii ni kutokana na Uzoefu wanao endelea kuupata Yanga kwenye hii michuano.
Ni rahisi sana kwa wao kufanyia kazi mapungufu na makosa ya timu kutokana na kuwa kwenye ushiriki wa muda mrefu. Tofauti na sisi Simba ambao hata ikitokea tunashiriki ktk hii michuano sidhani kama tutaweza kuleta mafanikio ya ghafla. Itatuchukua misimu zaidi ili tuweze kugaina ile momentum ya michuano. Ikifika hatua hii basi hawa wenzetu watakuwa kwenye hatua ya juu zaidi.
2. Suala la pili ni jinsi Yanga wanavyo sajili. Sisi Simba tumekuwa tukisajili aina ya wachezaji ambao tunalenga watusaidie kwenye ligi tu. Tofauti na Yanga ambayo wananunua mchezaji ambaye wanaona kama ataweza kuwasaidia kwenye michuano ya Kimataifa au la. Usajili huu wa Yanga unawafanya wachezaji waweze kufanya vyema kwenye Ligi zaidi, hii ni kutoka ubora wa players wao ni wa hali ya juu.
Klabu yangu ya Simba Sioni ikija kutoa ushindani mkubwa pindi Ligi itapo anza, hii ni kutokana kusajiliwa kwa wachezaji ambao hawakulikani kama wata_click kwenye kikosi au la. (Ingawa si mshabiki wa Yanga, niseme kuwa bado hatma ya ubingwa wa msimu 2016/17 upo mikononi mwa Yanga SC na kidogo sana kwa azama).
Wapenzi wenzangu wa Simba kaeni mkijua kuwa Klabu yetu inahitaji Msimu ujao kujitathmini kama iko imara au la, asije akakuambia mtu kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kubeba ndoo msimu ujao.
Hawa Yanga tunaweza kuwacheka na kuwakejeli kwa kufanya vibaya mechi zao za Shirikisho, ila wakiridu kwenye Ligi hawato kamatika kabisa.
Leo hii wakitolewa kwenye hii michuano hawana la kupoteza kwa kuwa akilini mwao bado wana uhakika kuwa Msimu ujao ni lazima watashiriki michuano hiyo.... Msimu huu wa Ligi watautumia kama kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa ya msimu Keshokutwa.