Naipenda nchi yangu (Tanzania),nawapenda pia viongozi wake,lkn tufanye yafuatayo...

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,486
13,017
Habar za leo ndugu wajumbe,

Namshukur Mungu Mwingi wa Rehema,huruma na mwenye kusubir anayetupa pumzi,jua na mvua bila malipo

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja; ndg zangu mm naipenda nchi yangu ya Tanzania na viongozi wake wa vyama na serikali,lakn naomba niwashauri hawa ninaowapenda kufanya yafuatayo ili kila Mtanzania aweze kuifurahia na kuipenda zaidi nchi hii

Viongozi wa nchi yangu ambao wengi wenye mamlaka wanatokana na chama cha mapinduz wawekeze zaidi kwenye ukuaji wa uchumi,hii itajumuisha kutengeneza ajira hasa kwa vjana watakao kuwa tayar kuajiriwa ndani na nje ya nchi.Pia wafikirie zaidi kukuza uzalishaji wa bidhaa za ndani ya nchi na kuzitafutia soko nje ya nchi pamoja na kuwafutia wawekezaji sambamba na kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi
Hali iliyopo kwa hivi sasa nchini kwetu kiuchumi ni mbaya sana,wazawa wanakimbilia nchi za jirani na kuwekeza mitaji yao,kodi zimekuwa nyingi kuliko maelezo

Wanasiasa wa pande zote waachwe wafanye siasa on a free and fair ground, hii utawafanya wananchi na wanasiasa kuiamini serikali na kuiheshimu hasa katka 'angle ya siasa'
Kilichopo hivi sasa ni manung'uniko makubwa sana kutoka kwa raia na wanasiasa kutokana na hisia za upendeleo kwa chama fulani,kupigwa risasi kwa raia wasio na hatia ktk muktadha wa kisiasa (Refer to Acquilina,Tundu Lissu,Diwani wa CDM wa Moro)

Viongozi wa nchi yangu pendwa wawafungie wanasiasa wanaojiuzulu kwa kigezo cha kijinga kuwa wanamuunga mkono m2 fulani,jambo hili linaigharimu serikali rasilimali nyingi sana ikiwemo muda,rasilimali watu hupotea (Refer to Acquilina and others) ninauhakika kama mpuuzi mmoja asinge jiuzulu hata Acquilina angekuwa hai kwa muda huu,pia rasilimali fedha na akili hupotea

Hawa viongozi wa nchi yangu waruhusu uchunguzi huru wa matukio ya kujeruhiwa au kuuawa kwa wanasiasa wa upande fulani ili kuuhakikishia umma kuwa there is no strong hand of the government to those assassinations of opposition

Vilevile,viongozi watukufu wa Taifa langu tukufu waache kuingilia majukumu ya kitaaluma au kitaalam,kwa mfano sasa hivi wanasiasa ndyo wanaofanya maamuzi kwenye fields mbalimbali wakati wao ni lay men, pia wanasiasa kwa hivi sasa wanawashurutisha sana watumishi,siku ikiisha na bado hujadhalilishwa na kutumbuliwa basi unaona kama ni bahati,tena wengine wanatumbuliwa na kudhalilishwa mbele za wa2 (kumbuka waratibu elimu kata waliotumbuliwa na DAB)

Zaidi ya yote wasisitize sana upendo miongoni mwa Watanzania

Naipenda nchi yangu,nakupenda Rais wa nchi yangu, nampenda hata Mh.Makonda kwa ubunifu wake lkn hayo niliyoyaainisha tuyafanyiebkazi sote
Mungu ibariki Tanzania,Mungu wabariki viongozi wa Tanzania
 
Kwa jinsi hali ilivo CCM wangeshaita kikao wajinusuru, ila sasa mwenyekiti ndo mtuhumiwa ....CCM inaenda kuzama bado kitambo kidogo
 
Kwa jinsi hali ilivo CCM wangeshaita kikao wajinusuru, ila sasa mwenyekiti ndo mtuhumiwa ....CCM inaenda kuzama bado kitambo kidogo
Wenyewe wakisikia hivyo roho zinawauma sana,kwa sababu kwa kupitia hyo hyo ccm kuna wa2 wanasukuma ndinga kali, wanamiliki majumba mazur,wanawake wazur,fedha nyingi na miradi binafsi mikubwa so hawawez kukubali ccm isemwe vbaya!
 
Back
Top Bottom