Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kuna wanaosema kuwa tuungane ktk jambo hili na kushikamana kama nchi. Yani kwa kuwa wafadhili wameshikamana kutunyima misaada basi na sisi tushikamane against them.
Tena wanafika mbali na kusema kwenye masuala ya kitaifa lazima tuungane pamoja bila kujali kama nchi imekosea au lah. Nimecheka sana. Kama kuna watu wanaofikiri hivi basi kuna haja ya kutizama upya mfumo wetu wa elimu maana hautujengi kufikiri.
Tujiulize kwanza hivi tunapoambiwa tusimame kwa pamoja kama nchi dhidi ya wafadhili, tunasimama kuhusu nini? Yani hoja yetu dhidi ya wafadhili ni nini?
Ingekua wafadhili wametunyima misaada kwa sababu wametulazimisha kukubali "ushoga" hoja ya kuungana ingekuwa na mashiko. Hata mimi ningehamasisha tuungane kwa pamoja kama nchi na tushikamane kukataa huo ujinga. Ningekubali kwamba bora tutaabike lakini tulinde heshima yetu na utu wetu.
Lakini wafadhili wametunyima misaada kwa sababu tumevunja misingi ya demokrasia kule Zanzibar. Sasa mnataka tuungane kama nchi ili iwaeje? Eti jamani hiki ni kipindi cha kushikamana kama taifa.. Tushikamane ili tuzidi kuvunja demokrasia au? Akili za wanywa viroba hizi.!
Pale tunapoonewa na mataifa ya nje nipo tayari kusimama na taifa langu kupambana hata tone la mwisho la damu yangu. Lakini pale tunapofanya ujinga kama tuliofanya Zanzibar na mataifa ya nje yakatukemea siwezi kujivika "uzalendo mandazi" wa kujifanya natetea nchi uangu hata kwenye ujinga.
Zanzibar tumefanya ujinga. Sasa kwanini tunalazimishwa kuungana kutetea ujinga huo? Mimi si goigoi wa kutetea ujinga eti kisa tu umefanywa na watawala. Ujinga ni ujinga tu. Ufanywe na Askofu, ufanywe na Imamu, ufanywe na Rais ni ujinga tu.
Watawawla wamefanya ujinga Zanzibar. Tusione aibu kusema ni ujinga eti kwa sababu umefanywa na watawala. Nchi Wafadhili wametusaidia kusema kuwa Zanzibar imefanyiwa ujinga na watawala.. na kwa sababu ya ujinga huo wa watawala wamepunguza misaada..
Sasa badala ya kuwapongeza wahisani kwa kukedmea ujinga huo kwa vitendo, tunaanza kutafuta huruma kwa wananchi. Tunaanzisha propaganda za kitoto eti tuwe wazalendo kutetea nchi yetu. Tushikamane kwa pamoja.. Mi nadhani Uzalendo wa kweli ni kuwaambia watawala wamefanya ujinga Zanzibar.
Siwezi kuunga mkono ujinga wa watawala eti ili nionekane mzalendo. Huo "uzalendo maandazi" mimi siuwezi. Uzalendo wa kuwa vuguvugu. Kwamba Ujinga ukifanywa na wanyonge unaitwa ujinga lakini ukifanywa na watawala unaitwa uzalendo.. Na tunahamasishwa tuungane kuutetea. Akili za wapi hizi??
Mimi ni Mzalendo sana na ninaipenda sana nchi yangu lakini siwezi kuunga mkono hata mambo ya kijinga kwa hoja ya uzalendo. Huo si uzalendo ni uzwazwa. Salaam kwa "Mazwazwa" wote popote walipo.!
Malisa GJ.!