Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

Naona sisi na wake zetu hatukauki kusoma hii story, inafundisha sana kwa sababu binadamu huwa tuna kasumba ya kutoka nje ya mstari.

Kina mama Karisa wapo wa kutosha kwenye jamii zetu, mwanamke akishindwa kuchagua marafiki mwisho wake ndoa inaota mbawa...
Kuna wengine wamejifunza kudanga kupitia story hii..
 
Yaani wanawake mnauwana wenyewe....
1. Asipozimwaga Siri zako nje basi....
2. Atakushauri usikubali nawe chepuka au kaanze maisha yako binafsi

Niwaulize wanawake wote ndani na nje ya JF.... UNALIPIZAJE KISASI KWA KUGEGEDWA NJE..??? HIVI UNAJUWA unapomkomesha mumeo Kwa kugongwa kisirisiri bila yeye kujua, UNAMKOMESHA YEYE AU WEWE MWENYEWE..??? YAANI UNAMKOMESHA MTU ASIYEJUA KWAMBA ANAKOMESHWA...!!¡

Halafu cha ajabu anayekushauri kuachana na mumeo YEYE ANAYASEMA HAYO AKIWA KWA MUMEWE...!!!

Mbona huongelei juu yenu.. ukidakwa na mke inakuwaje.. unamuacha mchepuko au unaendelea nae? Kwanini unachepuka.. unamkomoa nani? Kwanini hampendi na wake zenu waende kupata utamu ambao nyie hamuwapi?
Si mkubali tu unachosaka wewe huko nje upate furaha nacho mkeo anasaka.
Sio kulipiza or visasi blah blah blah.. bali ni kutafuta raha na furaha.
 
Mbona huongelei juu yenu.. ukidakwa na mke inakuwaje.. unamuacha mchepuko au unaendelea nae? Kwanini unachepuka.. unamkomoa nani? Kwanini hampendi na wake zenu waende kupata utamu ambao nyie hamuwapi?
Si mkubali tu unachosaka wewe huko nje upate furaha nacho mkeo anasaka.
Sio kulipiza or visasi blah blah blah.. bali ni kutafuta raha na furaha.
Wanasema wao ni haki yao kuchepuka, hutakiwi kuchukia wala kuwauliza
 
Hii story muisome na muielewe, ina mengi sana ya kujifunza hasa wanawake, dada zetu, wake zetu.....nimeguswa sana nikamkukumbuka my ex wife,,,,,duh Mungu msamehe alipo......in deep hii iko ktk maisha yetu kabisa....sana tuu....wanawake ache kuwa na marafiki wanafiki,,,,,muombeni Mungu ktk Christ Yesu mupate marafiki wema.....mkisali mmaanishe,,,mna nguvu KUU na ya ajabu,,,hamuitumii mnataka shortkati.....kumdhalilisha mmeo, kutangazia kila ubaya.....kwenda kwa waganga,,,,,,,wanawake MTUPONYE , tunawapenda sana hamjui tuu....

Mke wako ilikuwaje akakuacha? Ulichepuka akakuacha kwa kupata bwana mwingine?
Hayo ya eti story hii ni ya wanawake.. basi wewe unaubishi sana.. hii wanaume pia inawahusu tena sanaaaaaa.. ikiwa nyie ndio chanzo kwenye mengi.
 
SEHEMU YA 43
FB_IMG_1562824765205.jpg


SEHEMU YA AROBAINI NA TATU.
Mama Naomi alibaki na watoto wake, akili yake ilikuwa imelemewa sana na mawazo tangu siku tatunne hapo nyuma.Alikuwa anawaza mambo mengi sana, alikumbuka namna ambavyo mama Saimoni alivyopitia kwenye changamoto kubwa ya ndoa yake, na anakumbuka wakati huo alipokuwa anayaona hayo aliuwa anasema … mimi mwanaume haninyii hivi, mimi sio wa hivi,, lakini leo nay eye anakumbana na changamoto hii na yuko ndani ya ndoa na hafanyi lolote zaidi ya kupata wehu wa muda lakini bahati nzuri sana anakutana na mwanamke kijana mwenye kitu cha kumwambia.
**********
Ni vyema kila mwanamke akawa na roho ya utiaji moyo,moyo wa ushauri na moyo wa kusaidia, . Mwanamke huyo anaenda kwa Lipina na hapati msaada wowote ulena alilala usiku mzima kule, na anakutana na mwanamke mwingine kijana ambaye kwa masaa machache ameweza kumuonya, kumelimisha, kumkaripia na kumuombea, Mwanamke ambaye amejaa maarifa,na anamuacha mama Naomi akiwa na ahueni,na jambo la kwanza kabisa analofanikiwa kumshauri ni kukubali kukabili changamoto, kitu ambacho sio wanawake wengi ambao wako tayari kukabiliana na changamoto bali kuzikimbia changamoto.
Naomi anachukua watoto wake na kuhakikisha wanalala kisha nay eye anaingia chumbani kwake, na kupanda kitandani.
Kuna mambo ukiruhusu yakiingia moyoni yatakugharimu kuyatoa.
Unapoacha moyo wakoukaingiza vitu ni ngumu kutoa vitu ndani ya huo moyo. Gharama za kulinda moyo zinaweza kuwa kubwa sana lakini sio kama gharama za kuruhusu jambo liingie moyoni alafu ulitoe. Mama Naomi kama angetumia gharama kulinda moyo ingekuwa ni afadhali kwani moyo ukilindwa vyema unaepuka mambo mengi, na ndio maana maandiko yanasema Linda sanamoyo wako kuliko vyote ulindavyo maana ndipo zitokako chemichemi za uzima . Kujaza vitu moyoni kunaziba zile chem chem za uzima. Mama Naomi hakufanya kazi ya kulinda moyo, na badala yake moyo wake ulikuwa umejaza mume ndani, na kuamini kabisa chem chem za uzima wake ni mume kumbe sio . Mama Naomi analia usiku kucha kitandani, anakumbuka maisha yake ya ndoa siku za nyuma, anakumbuka maombi aliyofanyiwa na sasa kaambiwa asamehe,, anajiuliza nitawezaje kusamehe? Kusamehe ni jambo linalohitaji hatua kwanza,
1. Kuamini kabisa kwamba kama hutasamehe na wewe huwezi kusamehewa.
2. Pili unayemsamahe umsamehe haijalishi atajua kosa lake ama la kwa maana kwamba hata asipokuomba msamaha umsemehe tu.
3. Lakini hata akirudia kosa wewe unatakiwa kusamehe tu.
Ni jambo zito sana hili. na.linahitaji mwanamke ambaye amekomaa Kiimani.
biblia inasema vaeni Ngao ya imani. ili kwa hiyo muweze kuizima mishale.yooye ya moto. hivi huoni sasa imani yake ni dhaifu na si thabiti hata kufuhusu mshale wa moto wa mume kumchoma na kumjeruji kiasi hiki.

Hizi hatua sio kitu cha siku moja wala mbili, ni kitu ambacho kinamhitaji mhusika kugangwa moyo wake. Maandiko yanasema, Mungu huganga miyoyo iliyojeruhiwa. Mama Naomi ni lazima aanze uponyaji wa moyo wake. Akishapata kuponywa na kugangwa jeraha zake itamsaidia sana kuweza kuendelea mbele kwani ndio mwanzo wa kuweza kulinda moyo wake. Mama Naomi anakosa usingizi kwa kuwaza ukubwa wa tatizo. Anamuwaza mume wake namna kamgeuka, anawaza namna mume wake alivyokuwa na mwanamke na zile sauti zinajirudia masikioni mwake, lakini anakumbuka shukrain ambazo Marino alizitoa kwa mumewe, kwa kupata penzi tamu lakini kupewa zawadi ya simu . Hivi vitu vinaisonga akili yake sana, na analia sananakushindwa kunyamaza kabisa.
KUSAMEHE, KUSAMEHE KUSAMEHE . Kusamehe ni kazi kubwa sana, ni lazima mtu uwe na ulinzi mkali sana kwenye moyo. Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo,, maana ndiko zitokako chem chem za uzima. Kumbe hatutakiwa kulinda mume kuliko moyo, hata kama mume tutamlinda lakini alindwe na moyo ambao unalindwa, maana ndiko zitokako chem chem za uzima . “Linda moyo wako kuliko vyote”, vingine tulinde lakini MOYO Kuliko vyote…
Neno la Mungu linasema WANA AMANI TELE WALISHIKAO SHERIA YABWANA , WALA HAKUNA LA KUWAKWAZA.. Jambo la kukusaidia ili uweze kusamehe ni kuishika Sheria ya Bwana,, kwani itakupa amani kwa sababu hakuna la kukukwaza. Hivyo moyo ili ulindwe ni lazima SHERIA YA BWANA UISHIKE.
Lakini maandiko matakatifu yanasema tena, Neno la Mungu ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia zangu,, na akasema tena, Moyoni mwako nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi,, na mahali pengine akasema,, NENO LAMUNGU NA LIJAE KWA WINGI NDANI YAMOYO KWANI
Huko ndiko kulinda moyo. Neno la Mungu lijae moyoni kwani Neno linafundisha, linahusisha, lina adabisha, lina onya pia.
Kukosa Neno moyoni ni matokeo ya kushindwa kusamehe.
Mama Naomi angetumia gharama nyingi kulinda moyo asingekutana na gharama za kushindwa kusamehe.
Ngoja nikupe ushuhuda kidogo wakwangu kama muandishi wa Mkasa huu wa naipenda jumamosi yangu
Nakumbuka mwaka 2008, Mwezi wa Saba nilikutana na changamoto ambayo mimi sikuionani changamoto kabisa, japo ndugu, marafiki , majirani waliona niko kwenye changamoto kubwa sana na wengine walijua kabisa ndio imefika mwisho wangu wa mafanikio katika afya , uchumi, ndoa na hata malezi ya watoto. Wengi walijua nimekwisha.. Unamuona mtu anavyoongea na wewe tatizo na changamoto sio yake lakini kachanganyikiwa , ana hasira kuliko wewe ambaye una changamoto hiyo. Lakini nakumbuka jambo moja tu ambalo lilinisaidia katika changamoto hiyo ambayo wengi waliamini kabisa, SITAWEZA KUSAMEHE KABISA.
Jambo ambalo lilinisaidia katika changamoto hiyo ni limoja tu, KULINDA MOYO.
Moyo wangu ulikuwa umelindwa kikamilifu na hakuna dhaifu, hata moja ambalo lilipatanafasi ya kuingia ndani ya moyo na kuujeruhi moyo huo. Na walinzi ambao walikuwa wakilinda moyo ni KUSOMA NENO Huyu ni mlinzi ambaye huwa nasema analinda upande wa Kaskazini.
, Ninapenda kusoma maandiko matakatifu sana, yani ni lazima nisome maandiko matakatifu kwa style ya ,
(i). Kujua historia ya Walioandikwa kwenye Biblia.
(ii)Kusoma kwa kufundishwa kanisani ama kwenye semina.
(iii)Kusoma kwa kufundishwana Roho Mtakatifu mwenyewe, ,kwa maana ya kujifungia ndani na kusoma maandiko nikiwa nimetulia.
Hivyo mlinzi huyu wa kuulinda moyo wangu alikuwa imara na nilikuwa na maneno mengi ya kunijenga , kunifariji, kunionya na kunitia nguvu. Hivyo hata ndani ya changamoto hii nilikuwa imara kwa sababu tayari nilikuwa nina maneno yenye nguvu ambayo yaliujaa moyo wangu.
Lakini pia Neno la Mungu ni taa na mwanga, hivyo nilikuwa naweza kabisa kupata maelekezo niendeje, nikanyage vipi, madhara ya tatizo nayaona na kuyakabili na kujua ukubwa ama udogo ama madhara mbeleni . Hivyo Neno la Mungu likijaa ndani ya moyo wa mtu ni msaada tosha.

Lakini mlinzi namba Mbili ambaye huwa namuita ni mlinzi ambaye amesmiama Kusini ni MAOMBI
Mlinzi huyu Maombi ni mlinzi ambaye kazi yake ni Kuniimarisha, Ninaomba bila kukoma, si ngoji mpaka nikutane na changamoto ndipo niombe , la hasha, nimejijengea utaratibu wa kuomba daima, kuomba kila wakati kuomba kuomba kuomba,na katika kuomba huko naomba kama sitaomba tena, Naomba kama ambaye nafasi ya kuomba sitaipata tena. Maandiko yanasema Ombeni bila kukoma, ombeni kila wakati, kesheni mkiomba. Hivyo ninakuwa nahakikisha naomba daima. Neno la Mungu linasema katika 1 Wakorintho 14: 4 “ Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake” Maana yake ni kwamba, unapokuwa kwenye maombi na inapotokea unanena kwa lugha unaijenga nafsi yako, na ni katika kuomba ndipo ambapo Roho wa Mungu hutuombea kwa mlio usioweza kutamkikwa Rumi 8:26 -27 . Roho hutusaidia, Roho anaona zaidi yetu, anajua, hivyo unapokuwa unaomba na kujipatia muda mzuri wa utulivu kwenye kuomba ndipo mahali na wakati ambao Roho Mtakatifu hukusaidia inavyopasa. Hivyo unaimarika zaidi na zaidi, Moyo unakuwa na ulinzi wa kutosha.
Lakini jambo lingine katika kuulinda moyo ninaye mlinzi mwingine wa upande wa Mashariki, Mlinzi huyu ni MAOMBI YA KUFUNGA.
Ninapoamua kulinda moyo wangu ili utoe chem chem za Uzima ninahakikisha pia ninakuwa mtu wa kuomba na kufunga mara kwa mara, Kama mama na kama mke ninakuwa na maombi yangu ya mwezi kama ifuatavyo.
Nina kuwa na maombi ya mapatano kutoka kwenye vikundi vyangu vya maombi na wanawake wenzangu. Lakini ninakuwa na maombi yangu binafsi ya siku saba kwa maana ya masaa 12 kila siku kwa siku saba katika mwezi,
Na katika maombi haya ninakuwa na maombi ya mfululizo ya kufunga tu. Na
1. Ninajiombea binafsi.
2. Naomboa mume wangu.
3. Naombea Huduma yangu.
4. Naombea watoto wetu.
5. Naombea Afya zetu.
6. Naombea uchumi wetu.
7. Naombea Nchi yangu.
Haya ni maombi ambayo yanafanyika kila mwezi kwa siku hizo saba kwa kuomba hasa kila siku nabeba hitaji moja moja. Na hi inakuwa ni ulinzi mkubwa ndani ya moyo wangu kwamba, Mume, huduma, watoto, afya, uchumi hauwezi kwamwe kuwa mwiba katika maisha yangu kwa sababu tayari nimefanya ulinzi ambao ninajiwekea mazingira ya kuwa salama ,hata tatixzo linapotokea kumbuka Roho huniombea kwa kuugua kwani siwezi kuomba ipasavyo, na hata jambo likijiinua katika hayo hapo ninakwua Imara kwa sababu nina amani tele moyoni mwangu. Amani ambayo imeshajitengeneza.
Lakini ninakuwa na maombi ya siku tatu kavu, kwa maana ya masaa 72 bila kula kitu chochote, Maombi hayani special sana. Ni maombi ambayo huwa ninayafanya pale ambapo ninaona jambo Fulani linakuwa gumu, hivyo nachukua lile andiko linalosema kwamba lakini mambo mengine hayatoki ila kwa kufunga na kuomba. Hivyo Haya nayafanya kispecial zaidi, ikibidi hakuna kusafiri ama kutoka nje ya nyumbani ili niwe katika hali ya utulivu sana, Na ndani ya haya maombi mara zote ninapoyafanya ndipo ninapata maonyo hasa, taarifa, maelekezo na mafunuo mbali mbali katika huduma ninayoifanya pia. Hivyo huyu naye huwa namuita Mlinzi wa Kuulina moyo wangu.
Lakini yuko mlinzi mwingi wa upande wa Magharibi. SADAKA.
Sadaka ni jambo jema sana katika maisha ya mwanake mkristo. Ni jambo ambalo linaubariki moyo wa Mungu. Hivyo katika kuulinda moyo wangu nimekuwa pia mtu wa kupenda kutoa sadaka. Neno la Mungu linasema katika kitabu cha Matendo ya Mitume kwamba, Kornelio alikuwa akiwapa watu wengi sadaka, na alikuwa akiomba Daima, hivyo unaona jinsi ambavyo malaika wa Bwana alimtokea katika maono wazi wazi. Na kumpa maelekezo. Hivyo ni vizuri sana kuhakikisha unakuwa mtu wa kutoa Sadaka , Na sadaka ninazozitoa nazitoa kwa mfumo ufuatao.
1. Fungu la kumi kwa maana ya kila ninachokipata kwenye kazi zangu.
2. Sadaka za kanisani sehemu ninapoamudu (michango nk)Utaratibu wa kanisa.
3. Sadaka za Kila jumapili ninapoingia ibadani nisiende mikono mitupu.
4. Sadaka za Shukrani, hii ni binafsi yangu ninapokuwa na jambo a kushukuru. Na hizi naweza kuzitoa katika namna nipendayo.
(i) Kupeleke kanisani ninapoabudu
(ii) Kupelekea kwa wahitaji nk.
5. Sadaka za wahitaji. Yatima, Wajane na Wasiojiweza. Nilijifunza kutoa kilo ya sukari kila mwezi mara moja kwa mhitaji, kisha mara mbili,kisha mara tatu,kisha mara nne. Kwa kadiri nitoavyo nikawa naongezwa na Yesu. Ikawa ni njia ambayo moyoni nakuwa na mambo mazuri tuu ya kufanya. Sina nafasi kujaza visivyo na faida.

6. Sadaka za Nadhiri. Kutoa nadhiri zangu ninazoweza kuziondoa.
7. Sadaka za msukumo. Kuna wakati Napata msukumo kutoa sadaka kwa mtu binafsi, mtumishi wa Mungu nk.
Sadaka hizi unaweza kuona ni nyingi sana lakini nikuambie tu natoa kwa moyo, sio lazima mamilioni ila natoa kwa moyo . Sadaka yenye heshima. Sadaka yenye kumgusa Mungu.

Hao ndio walinzi wangu ambao wananifanya kuulinda moyo wangu kuliko vyote nilindavyo. Na tangu nimeanza kujifunza hayo na ninaendelea kujifunza nimejikuta kwanza kuepukana na dhambi, kuna tabia mbaya na dhambi ambazo zilikuwa zinanisonga na nikawa mtumwa kwazo lakini leo najishangaa nimewezaje, ama kwa hakika UTUKUFU KWA JEHOVA MUNGU WA BWANA WETU YESU KRISTO.
Moyo wangu naulinda kwa namna hiyo. Hivyo mpenzi mtasomaji,unapoendelea kuburudika na kujifunza kupitia mkasa na ushuhuda huu nimeona mimi Irene Mbowe nikushirikishe kitu hichi cha kuulinda Moyo wako kuliko vyote ulindavyo kwa kuweka hao walinzi wan ne wazunguke kuta za Moyo wako,. Kuomba kwa kumaanidha kutakufanya uwe karibu na Mungu, kusoma neno hali kadhalika kutakutanya uache dhambi maana Biblia inaseme Neno la Mungu linaonya na kuadabisha. Hembu soma hili Andiko hapa kidogo uone,
2 TIMOTHEO 3: Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kuwaonya watu makosa yao, ka kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.
Unapokuwa mtu wa kusoma Neno la Mungu kwa kumaanisha unakuwa mlinzi wa Moyo wako sana kwa maana ya kupata ufahamu, ikiwa ni pamoja na KUJUA UMUHIMU NA UTHAMANI WA KUSAMEHE . Maana Biblia inasema je ni nini kitatutenga na upendo ulio katika Kristo Yesu? Je kutosamehe kutakutenga na upendo huuu??

lakini Mlinzi mwingine ni kuwa na watu sahihi,Waliojaa hekima na maarifa ya kimungu. watu ambao wamekomaa. unapokuwa na.changamoto unahitaji kuwa na watu waliokomaa. ambao watakushauri kabla ma baada ya changamoto. watu ambao watakuwa wanakuona na kukusaidia. haikuwa rahisi katika eneo hili .Kujitenga ama kutengwa na marafiki wasiofaa sio zoezi rahisi hata kidogo. ni zoezi lilouma sana. mnoo. lakini nikaanza kutengwa na marafiki wapotoshaji, wasiofaa.
Katika kuulinda moyo ni vyema sana kuwa na marafiki ama washauri bora na waliokomaa katika imani. hawa ni msaada mkubwa sana.
Ngoja nikuambie mwanamke kijana ambaye unanisoma katika ushuhuda ama mkasa huu. Kuna.gharama tunazikwepa lakini madhara yake yanatugharimu mara dufu. Hivi kuomba sasa hivi inakugharimu nini?Kusoma neno la Mungu sasa hivi inakugharimu nini? kumtolea Mungu sasahivi inakugharimu nini?Ama mpaka usikie toa upate utajiri ndio unakimbilia huko?Mwanamke kijana mchaji wa Mungu hayumbishwi na manabii feki. Ni mwanamke anayeishi kwa utaratibu mzuri katika maisha yake. ni mwanamke mwenye Ratiba endelevu maishani mwake. Ratiba nzuri za ibada zake , hababaishwi na nyakati. maana neno la Mungi liko ndani yake. Roho wa Mungu anamuongoza. Moyo wake unalindwa na umelindika sanaa.

sasa mama Naomi anaingia kwenye gharama hii ya kusamehe kwa sababu hajalinda moyo.
Kitanda kinakuwa kama kimemwagiwa maji. hapati usingizi kabisa.Kweli kaombewa,lakini sio mtu wa kujiombea. hajui aombe nini. ana hasira na uchungu ataombaje?
kujizoeza kuomba, kusoma neno la Mungu ni jambo zuri. kwani linakuwa ni sehemu ya maisha yako. hata Ukutane na changmoto gani hutaacha kuomba Mungu.
Katika hiyo changamoto yangu nilifamikiwa sana kuikabili kwa sababu Sikucha ratiba zangu za kuomba. Niliendelea kuomba na kufunga. na Kachangamoto nikakaona ni kadogo sanaa. na hata kalikopitia sikujua. lakini ni kwa sababu nilikuwa na walinzi hao. walinziwa kulinda moyo wangu.

Mama Naomi angepaswa tuu apige amagoti na kumwambia YESU Pigana wewe. nitetee nivike unajasiri katika hili.
Ninapokumbana na hali ambazo si swari huwa nakumbuka jambo moja la muhimu sana ,
YESU NISAIDIE NISIKUTENDE DHAMBI.
Maneno haya ni machache sana. Lakini huwa yana nguvu ya ajabu mnoo katika maisha yangu.
huwa najikuta kila kitu nakiona cha kipuuzi na kujikuta najiona mshindi na mqenye kupendwa na Yesu.
Mwanamke kijana nikushauri tuu ULINDE MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO KAMA NENO LISEMAVYO.

Inaendelea sehemu ya 44

Post # 1200
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom