Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
23,146
Points
2,000
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
23,146 2,000
Mimi mwenyewe amenifungua kwa kweli, kumbe naombaga juu juu sana, Mungu nisaidie niwe na roho ya uombaji kama Tilda
Umuhimu wa maombi ni kumaanisha na kuweka imani.. sio kutamka tu maneno.

Unaweza kusali dakika chache sana na maombi yako yakawa yanapokelewa. Kuomba ni muda wowote na haswa pia pale unapoona sauti ya roho mtakatifu inaongea pia nawe ufanye hayo. Hata ukiwa unaendesha gari huku unaangalia huku na kule ni maombi.. mwisho wa siku ni kama nilivyeleza mwanzoni.

Ukiomna basi mtu weka imank sio baada ya mufa unaanza kufikiria mabaya kama hayatakiwa au kunena kama haya bado mabaya.. n.k. n.k. ni unakuwa umesali na kujigutia maombi mwenyewe.. hapo utaomba tu na kusubiri kumbe mdomo na fikra za mtu zimezima anayotumainia kutendeka mwenyewe.. uwiiii kuandika maneo mengi huwa sijui.. ubarikiwe omba na kuwa na imani yatakuwa.
 
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
23,146
Points
2,000
cocochanel

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
23,146 2,000
Sitaki kuamini siku yangu nzima Leo imetekwa na Mama D mpaka nikaunguza chakula jioni, Good Lord..!! hata sijui nilikuwa wapi nimekuja kwa kuchelewa namna hii..!
Ooooops' ila story tamu hasa.!!
Pole kwa kuunguza chakula kwa uhondo.. stoty hii ina mengi na mafunzo na inafikirisha sana sana.

Tunasubiri muendelezo
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
112,990
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
112,990 2,000
View attachment 1123992


SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA

Akili yangu imeshachoka Ndoa,lakini sio ndoa tu, imeshamchoka na baba Davis, kila ninapomuangalia kuna kitu kinaniambia akilini ondoka,achana naye, kama ni mwanaume umempata, anayekupenda, anayekujali anayetamanikuwa pamoja na wewe, anayejua thamani ya mwanamke,
Kuna maneno ambayo Yanazunguka akilini kwangu kwa kasi ya ajabu sana, na kunifanya nashindwa kuvumilia . Kuna nguvu ya ajabu inayotenda kazi ndani yangu ambayo inaniendesha na sio akili zangu, hata ninapojaribu kuvumilia inakataa.
Baba Davis, umeishi na mimi miaka mingapi, siku zote niko pamoja na wewe unashindwa kunitoa out, unashindwa kunijali, unashinda kunihudumia, leo mpaka ufundishwe? Hivi kwa nini ulikuwa unanitendea mambo mabaya kiasi kile? Leo umeachana na Sarah ama unanizuga tu?
Muda wako umepita, wacha nikae karibu na wanaume wenye mapenzi ya dhati na mimi.
Nawaza huku naelekea kwa Moses,, nilikuwa nipo ndani ya taxi,, anti umefika,, anti ni hapa,,
Nilifika enfo la tukoo, nje kulikuwa na magari mengi sana, nilimwambia dereva taxi, naomba subiri kidogo,
Nilipiga simu kwa Moses na aliipokea kisha nikwambia niko nje anaweza kutoka?
Ndio aljibu, na haraka sana, niliona mwanaume akitoka nje ambaye alikuwa kashikilia sigara inayowaka mkononi wake wa kulia na mkono wa kushoto alikuwa ameshikilia chupa ambao kwa mbali sikujua ni chupa yenye nini.
Lakini ilikuwa ni chupa.
Ooo Shemeji, Mambo?, Moses alinisalimia,
Salama shemeji,, samahani, tunaweza kuongea? Nilimuuliza,
Ndio shemeji yangu…
Shemeji samahani ,nimempigia Fadhili simu lakini kuna mwanamke kapokea hiyo simu na kanitukana sana, ni nani huyo mwanamke?
Shemeji na wewe,, una wivu kiasi hicho? Moses alinijibu.
Sio wivu shemeji,, ila tu nimeshangaa kwa nini nimetukanwa,,
Shemeji kwani wote si mnaiba, wewe na Fadhili wote si mnaiba… huoni mwenzako alikuona na mr akavunga,, sasa na wewe ulipaswa kuvunga tu shemeji yanguu,,
Huyo mwanamke ni mwanamke wake,, kwani hajakuambia kwamba ana mke?
Ameniambia,, nilimjibu..
Basi sasa kawivu shemeji ukaache,, Moses aliniambia kisha akaniambia,, ingia ucheze kidogo mziki uondoe stress.
Dereva Taxi aliniambia anti niondoke?
Moses alijibu, ndio ondoka nitamrudisha..
Ingia shemeji yangu upunguze mawazoo..
Ingia ucheze kidogo, nitamuambia jamaa niko na wewe usijali kabisa.
Niliingia disco, kulikuwa na watu wengi sana, wengine nawafahamu, wengien siwafahamu, lakini niliona wanaume kama watatu hivi ninaowafahamu.
Nilishtuka sana kuwaona, lakini bila shaka na wao walishangaa kuniona pia.
Mziki sijui kucheza, hivyo nilikuwa nazunguka zunguka tuuu..
Nilikuwa kama ambaye kaachanganyikiwa sana,, ninawaza akilni, nikitoka hapa sitaenda nyumbani, nikitoka hapa narudi Boma kwa mama na ndoa ndio sitaki tena, narudi kwa mama na ndoa sitaki tenaaa…
Wakati nawaza hayo,, nikiwa ndani ya mawazo marefu sana ambayo yalinifanya hata nisisikie sauti na kelele za miziki,,
Ndipo nikasikia watu wakishangilia kwa kelele sanaaa, tena kelele nyingiii mno wakifurahishwa na mziki ambao ulikuwa unapigwa,
Wimbo ambao nami huwa naufahamu sanaaa,

… nataka nitoke na mpenzi wangu seyaaaa…. Ujue seyaaaa…
Disko zima lilipiga kelele za shagweee… seya niko wakooo.. wa kufa na kupona,, Seya tutoke woteee.. wasema niko wakooooo.
Seyaaaaa. Seyaaaaa. Mamaaaa..
Disko liliendelea kpiga kelel kwa dakika zisizopungua kama tatu hiviii

Moses alishika mkono na kunisogeza kati kati kabisa ambako kulikuwa na watu wengi sana wakicheza nao mziki na kuufurahia,, sikuwa na sababu za kushangaa, japo sikuwa najuwa vyema stape, lakini nilitazama wengine wanafanyaje na mimi nikwawa nacheza, na kwa Vile Moses alikuwa akijua kucheza, basi alianishika na akawa ananisogeza kwa kufuatisha stape, nami nafuatisha vile anacheza,,
Mziki ulinoga hasa, na akaniuliza utakunywa nini? Nami nikamjibu savanna, akanipatia savanna yangu na nikawa nakunywa huku nachezaaa.. ghafla nikaziwezea stape, na yeye akiendelea kunipapasa, mara kiuono,, mara makalio..
Baba na mwanaaa, tunaimba na kucheza,, ilipofikia hapo, nikawa na mimi naitikia,,
Baba na mama tunaimba na kuchezaaa… mziki uliuwa mzito sanaaa,
Papa Fadhilii.. sikia hiyooo eeeee, ndama mutoto ya ng’ombe, nilisikia Moses akisema hayo maneno wakati muziki unaendeleaaaa
Wazeee wa mujiniii.. Fadhili,, Moses,, Abasiii.. wazeee wa mujinii..baba na mwanaaaa,, tunaimba na kuchezaaa,,,
Moses aliendelea kuupamba huo wimbo huku akiwa kanikumbatia vizuri sanaaaa,
Na kwa vile na mimi nilikuwa na hasira zangu na stress zangu nikaona wacha nijiachie hasaaaaa.
Nikasikia tu watu wakisema, rudiaaaaa. Rudiaaaa.
Na DJ Akaurudia tena huo wimbo,na sasa hivi hakuna ambaye alikuwa amekaaa, kila mmoja alisimama na kufurahia huo mziki,
Na mimi sasa kwa vile nilishabwia bia zangu tatu haraka haraka,, nikajikuta nimeshaanza kuchangamka, na kuanza kucheza haijalishi nilikuwa napatia stape ama vipi lakini nilijiachia hasa na kuyaachia mauno bara bara..
Aaaa. Shemela unaua sasa… Moses alikuwa akiniambia, huku akiwa nyuma yangu na mimi nikiwa nacheza hasaa tena kwa kukatika mauno hasaaa.
Seya tutoke woteeee…. Mpenzi wangu seyaaaa… mamaaa seyaaaaa.
Nilicheza hasa na sasa nilishajua maneno Fulani Fulani nikawa nayarudia kutokana na ngoma kunoga.
Nilijisahau kabisa kwamba mimi ni mama wa watoto, ama mke wa mtu, sikuwa nakumbuka kabisa, wala sikuwa nafikiri.
Mziki umenoga, disko limenoga hasaaa.
…….Vaa vizuri mpenzi wangu, upendezee,
donge liwashike, mabusu moto motoo.
Mimi na wewe mpaka kufaaaa…
uuu iiiiii usiwasikilize haoo wanaotaka kuharibu mapeeenzi yetuuu..

Basi Moses akawa anayaimbia haya maneno masikioni mwangu, nami nikawa sijali kabisa lolote lile, nimejiachia kabisa na ninacheza hasa mziki kama nilipanga kuwepo disko.
Mamii sasa? Moses alikuwa kanikumbatia wakati ananiambai mamii sasaaa..
Nilimtazama nikiwa nimechoka na kulegea hasa,, nikamwambia ninataka kupumzika,,
Haina shida,, utapumzika, wala isikusumbue,, na mimi pia nataka kupumzika,,
Naomba basi tukapumzike wote,,Nilicheka kilevi levi, na tukaondoka kwenye gari yake haooo, tukawa tunaelekea kwenda kupumzika.
Simu yangu ilikuwa inaita sana muda Fulani, Moses akaizima,
Na nilisikia akisema,, hatuhitaji usumbufu.. sikujua wala ni nani kapiga, ila simu zilikuwa zikiita sana.

Nilikuwa nimechoka sana na nililala kama gogo.
Ni kwenye nyumba nzuri tu ambayo nilikuwa nimelala, nyumba ambayo inaonekana ni chafu chafu, vichungi vya sigara, chupa za pombe na mikate na mabaki ya nyama za kuku na chips ndivyo niliweza kuviona mara baada ya kuamka.
Pole shemeji yangu…
Aliniambia Moses, asante nilijibu,, na sikuwa na ujanja wowote.
Nilichukia sana kulala na Moses bila ridhaa yangu, kwani ni pombe zilizonisababisha nikalala naye.
Aliniambia,, nikuombe tu mapenzi yetu tufanye siri kubwa, nakuomba sana Fadhili asije wahi kujua jambo hili, tena naomba kabisa usiwahi kumwambia kwamba ulikuwa na mimi Disko,, umesikia mamiii
Alinipiga kibao cha usoni kwa utani, akiwa kavalia kaptula tu na kifuani hajavalia nguo yoyote,,
Nguo zangu zilikuwa chini na nilikuwa nimejifunga tu taulo ambalo hata sijui nilijifungaje na saangapi.. japo kuna saa akili kama ilikuwa inakumbuka namna nilivyokuwa nimelala naye, na namna wimbo wa Seya ulivyokuwa ukiimba ni kama ulikuwa unaimbia akilini mwangu..
Usisononeke,, usijali shemela,nakupenda ila naomba iwe siri kubwa sanaa, umesikia..
Ndio nilijibu,, sikuwa na ujanja wa kutojibu wala kubishana, maana ni kama nimeyataka mwenyewe,, nilisikia hasira lakini nifanyeje?
Ngoja wanoko waondoke kisha nitakutoa,,, Moses aliniambia.
Mh.. wanoko, ni kina nani?
Nilikuwa nasikia tu sauti za wanaume wakiongea humo ndani lakini sikujua ni kina naani,
Ni kina nani hao? Nilimuuliza Moses,, wanoko. Ni wanoko… ndio maana nataka watoke kwanza.
Dah.. nilijiskia uoga naaibu..
Moses,, nilimuita,, naaam.. Fadhili hawezi kuja huku?
Hawezi,, alinijibu..
Unamuogopa sana Fadhili eee.. hata mimi ni mwanaume hembu usimtaje taje sawa..
Moses alisema akiwa kakunja sura.. Fadhili Fadhili, alafu ukiwa na mimi uniheshimu…
Alisimama na akawa anaondoka,, kisha akaniambia nakuja natoka kidogo, narufunga mlango ili nitoke na wao watoke. Usiogope.
Moses aliniambia hivyo kisha akatoka na kufunga chumba chake kwa nje kwa funguo kabisa na kuniacha ndani.
Aliondoka na nikawa nachungulia kwa dirishani kwa umakini kabisa, na nilibahatika kuona wanaume wawili wakitoka wakiwa wameongozana na Moses, Mungu wangu? Sikuamini nilichokiona,, ni Dogo na mwanaume mwingine, nilishtuka sana.
Mungu wanguu.
Ndio maana Moses alisema wanoko… nilirudishia pazia pole pole na kurudi kutulia kitandani.
Walitoka kabisawote na akaingia mwanamke mmoja mtu mzima ambaye alipewa maelezo yakufunga na kufanya usafi ndani,, Mama Zawadii,, ufue nguo zote,,
Nilisikia tu Moses akisema kisha wakatoka wote.
Nilikuwa naogopa sana, moyoni naomba Mungu tu Fadhili asije akaja kwa Moses,,n itakuwa mgeni wa nani,, ndicho nilikuwa nawaza.
Yule mwanamke aliingia naanza kufufanya usafi kama alivyoelekezwa, alikuwa akideki na kuosha vyombo na kufagia,,,
Nilikuwa nasikia hivo movement tu na mimi nikiwa ndani nimetulia kwani niliambia ninyamaze kimya.
Baada ya muda nikachuka simu yangu ili kuangalia nani kanitafuta.
Nilikuta msg za Tilda za kutosha, nilikuta msd calls za Fadhili.
Na wa kwanza kuamua kumpigia ni Fadhili.
Nilimpigia Fadhili na alipokea kisha akaniambia,, pole mpenzi.
Pole sana, jana usiku umepiga wife akapokea, sorry mpenzi wangu.
Sikukuambia..
Asante sana, nilimjibu.
Enhe,, vipi mlimaliza salama? Aliniuliza, asijue niko kwa rafiki yake,,
Hapana hatukumaliza salama, Yani hatujamaliza salama hakuna kabisa usalama, na nimeamua kuachana tu na baba Davis, sitaki tena hii ndoa Fadhili, nilijikuta nalia na ninapata auchungu sijui hata ulikuwa unatoka wapi,
Fadhili sitaki hiindoa, naomba nisaidie, nimechoka kunyanyasika..
Basi usijali, usijali kabisa ngoja tutakaa tuongee tuone tunafanyaje mpenzi wangu. Fadhili alinijibu.
Ninatoka ofcn mara moja, naenda kumuona Moses kisha nikishamalizana naye utaniambia uko wapi alatu tukae tuone jinsi tutakavyofanya, usiogope, wewe ni mpenzi wangu usiogope kabisa.. sawa mamsapu..
Sawa.
Aliposema anaenda kuonana na Moses moyo wangu ulilipuka, nilihisi kama kufa, Mungu wangu,, sio anakuja kweli huku nyumbani,
Nilipokata simu nilichukua simu yangu na kumpigia Moses simu,
Halooo.. nimeongea na Fadhili ameniambia anakuja kwako kukuona…
Nilimwambia Moses…
Unaogopanini sasa? Mbona kama unawinya? Acha wenge wewe demu..
Moses aliongea na mimi kihuni sana,,
Sikupenda ila nifanyeje?
Wewe demu kama una wengeee sanaa, hembu tulia..
Mh.. ilibidi tu nitulie..
Lakini natuliaje? Yule mama bila shaka alisikia nikiwa ninaongea na simu,
Nilianza kumuita,, mama zawadi, mama Zawadiiii.. niliita mara tano hivi, kisha akasikia akaja,, akafika mpaka mlangoni,
Abeeee, unasemaje?
Samahani, naomba nifungulie.
Hapana siwezi kukufungulia, ngoja nimuulize Moses..
Nilishangaa Yule mama kukataa kunifungulia, nilishangaa sana,
Sasa akili yangu ilikuwa inawaza mambo mengi, je kama Moses anaenda kumuambia Fadhili kalala na mimi na Fadhili anakuja itakuwaje?
Mapigo ya moyo yalianza kudunda kwa kasi,, Nimefanya nini? Nilikuwa naanz a kujilaumu.
Ama nimpigie Dogo? Ama nifanyeje jamani?
Mama Zawadiii, naomba nifungulie, nakuomba dada yangu, please.
Nilim bembeleza sana huyo mama ambaye wakati huo alikuwa nje anafua nguo.
Aliniambia tu siwezi kukufungulia je ukitoka na mawe ya watu mimi nitasemaje?
Mh.. ukitoka na mawe ya watu? Niliwaza, ahaaa, mawe, mawe ni Tanzanite… ahaaa, Moses bila shaka ni mchimbaji ama muuzaji wa madini,,
Hapana mamii.
Kweli tena sikufungulii mama yanguu, Moseee ananiamini sana sikufungulii mpigie tuuu. Huyo mama aliongea kwa sauti ya kiarusha kabisa akivuta manenoo, moseeeee aliposema hiyo moseee ndipo nikajua ni muarusha.
Dah. Sina ujanja.. nilishangaa sana.
Nikiwa nimekaa tu sina hili wala llile, nikiangalia saa ni saa saba mchana, nimekosa pozi, ndipo nikaona geti linafunguliwa,,
Na anaingiza gari Moses..
Nilikuwa nimechoka kwa mawazo.
Aliingia na akanifungulia nikiwa na hasira sana,
Enhe,, ratiba zako mama? Aliniuliza kwa kejeli.
Nilimwambia tu nataka kuondoka.
Poa, una nauli ama unaondokaje?
Nina nauli, nilimjibu.
Poa,, basi badae,,
Aliniambia hivyo kwa kejeli na nikatoka, nikamkuta Yule mama anafua pale nje nikamsalimia,,
Kisha nikatoka mpaka getini.
Nikawa natembea kuelekea barabarani.
Nilitembea umbali mrefu kidogo mpaka kufika bara bararani, kama km mbili hivi.
Nikiwa na mawazo mengi sana, nawaza imekuwaje mpaka nikalala na Moses bila ridhaa yangu, nilichukia sana na kujilaumu sana.
Nikiwa njiani simu yangu ikaingiza ujumbe,, nikaangalia ujumbe,
Ni m-pesa.. nikaangalia umepokea kiasi cha shilingi 250,000 kutoka kwa Moses Kilazo… na namba ya simu ya Moses ikawa pale..
Mh… afadhali hata nimepata pesa, nikajisemea,
Kisha akanitumia na ujumbe,,
Asante kwa penzi,, nilienjoy asbh, asante sana.
Nilipomaliza kusoma ujumbe akapiga..
Wala sikuona sababu ya kupokea ile simu maana moyo wanngu ulikuwa na maumivu.
Niende wapi? Nilikuwa najiuliza,, akili ikaniambia nenda kwa Mama Karisa,
Nenda Kwa Thea, nenda kwa Tilda,
Mwisho akili ya Nenda kwa Mama Karisa ikashinda,
Huyo nikaita taksi, kwa sababu nilikuwa na ile pesa kwenye mpesa, nikaenda mpaka dukani kwa Mama Karisa.
Nilimkuta yupo na aliponiona alishangaa sana,
Karibu, alinikaribisha,, niliingia na nilikuwa nimechoka sanaaa.
Afadhali shoga yangu, nimekuona yani nina hamu na bia balaa, bora hata umekuja utaninunulia biaa, boraaa.
Dadaa.. hizo nguo usisahau kuziweka pembeni,, mimi natoka na mama Diii..
Mama Karisa aliongea haka haaka kana kwamba alijua nitakuwa pale muda ule,
Yani hata hakuniruhusu nikae muda,, wakati huo huo aliuwa anachukua pochi yake na tayari alikuwa kashasimama ,,
Haya twende tukakae mahali unipe michapo ya safar maaana naona ulikuwa honeymoon,, na ninazo habari njema zako,, Fadhili anataka kukuoa kabisaaaa akufanye mke, ha ha ha halaaaa…
Yani mwanamke wewe ni hatariii.. Mama Karisa aliongea kwa kejeli lakini ni kama anayemaanisha jambo.
Fadhili anataka kunioa?
“Nakupenda sana Mamiii, naomba usiniache, nakupenda sana” Nilikumbuka hayo maneno ya Fadhili usiku wa kwanza nikiwa naye hotelini Dar es salaam, alipokuwa akiniambia hayo maneno kwa hisia kali sanaaa.

“Nimewahi kupata wanawake, lakini sijakutana na mwanamke kama wewe.. nakupenda,,, utaniua kwa penzi lako” Fadhili alisema usiku ule hayo maneno.
Mh.. kweli Fadhili anataka kunioa?
Mama Karisa kajuaje?
Fadhili ananipenda.. ananipenda..

Simu ya mama Karisa ilikuwa inaita. Iliita muda mrefu sanaa, kisha akaiangalia na kusema, Mh,, huyu Moses ananitaka nini saa hiii…
Moyo ulifanya paaaaa. Moses tena anamjua Mama Karisa.
Mungu wangu.. nilishtuka sana
Nilishangaa sana..
Mama Karisa, alichukua simu na kuanza kuongea..
Sema muzee ya mujini… una gram ngapi leo? Unataka kunihonga nini?
Nilisikia hayo maneno kutoka kwa Mama Karisa,, niliishiwa nguvu..
Nilikosa nguvu kabisa, nikijiuliza, Moses huyu ni rafiki tena na mama Karisa?
Mama Karisa alisogea pembeni na kuongea na Moses, kisha akarudi na kuniambia, mamii ingia kwenye gari twende zetu..
Nilipanda kwenye gari nikiwa sina tena raha kabisa, haoo tukaelekea mahali ambapo tutakaa na kuongea.
Pombe pombe pombe nilijua tu mwisho mama dii atakulwa na moses
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
112,990
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
112,990 2,000
Natimiza ahadi
T 1990 ELY

Blaki Womani Shunie
Joowzey Smart911 ram ukhuty moneytalk
Chloe 92

Na wengine wote mnaopenda hii story ya Lady Irene mnajua sio rahisi kukumbuka kila ID huku sikupangia kuwa nitabidi niwaite kama nilivyoamua sasa..

Imeendelea post #391
Asante coco babe
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
112,990
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
112,990 2,000
Kwa sasa kamuweka kama sio mke wa mtu.. eeeh tutasubiri.

Hata humu JF lazima atawasoma.

Kuhusu kurudi kwa mumewe akimua kutorudi sawa tu.. si kwa kumtenda yale live mbele ya mchepuko.. na home alikuwa mke mwema anaweka mambo sawa kwa moyo wake wote kama mke na mama anayejua majukumu yake.. baba d akamuona ni boring. Wanaume kama humpendi tena mkeo bora kuelezana muachane kurudiana inakuwa na chances kubwa kuliko mtu kukaa na kumbukumbu ya live actions.

Hata Mungu aliongelea uzinzi.. kwanini mwanamke afe augue magonjwa eti kisa mwanaume na hawaachani.. kuachsna pia kwa wengine ukutana na Neema na Baraka tele tele mbeleni.. upo eeeh
Niko pamoja na ww coco babe
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
112,990
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
112,990 2,000
Atakuwa mtumwa wa ngono kwa Moses
By the way Shunie hivi ile story ya ''Mtumwa wa Ngono" iliiishia wapi kule entertainment, sikuona mwendelezo wake tena
Ile story halafu niliirukia tu ile story ya watu nikaiendeleza baada ya mwenye thread kuona hapost sijaifatilia ebu ngoja nione itatolewa kitabu au vipi
 

Forum statistics

Threads 1,304,159
Members 501,282
Posts 31,504,846
Top