Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Nikiambiwa niweke caption kwenye hii picha ningeiweka hivi:safi sana mtu wa pwani CCM DAIMA!!
View attachment 14249
"Hebu mwangalieni huyu maskini...anashabikia mauti yake"!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikiambiwa niweke caption kwenye hii picha ningeiweka hivi:safi sana mtu wa pwani CCM DAIMA!!
View attachment 14249
nishalieleza kuwa hiki ni chama cha watanzania na hata wapinzani wameapa kukilinda mpaka kufa
yaani ndugu wewe kama unafikiri umemka basi nina mashaka umo ndani ya ndoto mbili...
View attachment 14250
CCM kimeongozwa na wenyeviti wafuatao:
J K Nyerere (Mkristo)
A H Mwinyi (Muislam)
B W Mkapa (Mkristo)
J M Kikwete (Muislam)
nionyeshe chama chengine mfano wa CCM katika kubalance mambo ya udini?
suala la kadhi halikuingizwa kwa sababu ya udini na wakati huo walioandaa ilani ya chama wengi hawakuwa waislam (kama Mh Kingunge) waliona kuna umuhimu wa sehemu ya jamii wa watanzania kutekelezewa matashi yao ambao ni haki na ni sehemu ya kutekeleza imani yao. kitu ambacho CCM inaheshimu na kuthamini michango ya dini zote ktk kuimarisha amani na ustawi ktk taifa letu.
chama kingine kilichoweka ni chama cha NCCR wakati ikiongozwa na Mrema
CCM inathamini michango ya dini zote na ndio maana ukaona mwenyekiti wake anahudhuria hafla za dini zote na anapokea ushauri wa dini zote
ingelitaka CCM ingepitisha suala la Kadhi ila baada ya kusikiliza wananchi wameona waangalie utaratibu mwengine wa kuwawezesha waislamu kutimiza ndoto yao
CCM ilifuta misamaha ya kodi na ilipoenda bungeni na kusikia kilio cha wakristo iliamua kubadilisha msimamo, ni chama pekee chenye kusikiliza shida za watu
chama cha Mapinduzi ndio chama kilichozaliwa kutoka vyama vilivyotuletea ukombozi wa nchi zetu
ndio chama kilicholeta mapinduzi ya kifikra kwa watanzania katika nyanja mbali mbali, kama elimu, uchumi, afya na mengineo
ndio chama kilichojitolea kusimamia mapambano ya huru kwa bara la afrika na duniani kwa ujumla
ndio chama kilicholeta demokrasia na kuleta mfumo wa vyama vingi kwa amani bila ya vurugu
CCM imesimamia na kuwa nguzo ya amani ya nchi yetu
CCM ni chama ambacho kimechagua bendera yake kuwa kijani kwa kuamini :
rangi hio ni ishara ya maendeleo, ustawi, bahati, na ndio maana ukizungumzia usalama wa afya unawakilishwa na kijani, amani na usalama hata kwenye ICT connect ikiwa safi basi green color inapresent hilo
sio blue rangi ya mikosi
karibuni kwenye chama chenye neema na chama chenye demokrasia ndani ya chama na hata ktk kuendesha serikali zake zote mbili
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1976 wakati nilipokuwa JKT, tuliambiwa tuchague jina la chama kipya kitakachotokana na muungano kati ya ASP na TANU. Vikao kama vile vilifanyika na baada ya hapo tukaambiwa kuwa jina la chama litakuwa Chama Cha Mapinduzi, na mboni zake ni jembe na nyundo kuashiria kinawakilisha wakulima na wafanyakazi. Tuliamini sana chama hicho na wengine tulikuwa tayari kufa kupigania sera na maadili ya chama hicho, maadili ambayo tulikuzwa nayo na yalitekelezwa kwa vitendo.
Kwa bahati mbaya sana, nasikitika kusema, kile chama ambacho kilitulea, ambacho kilikuza na kuumba fikra zetu (ambazo ndizo zinazonifanya niandike haya,) chama hicho kimegeuzwa na watu wachache wapendao uchu wa madaraka, wanaojilimbikizia mali na kukuza usultani. Chama hicho kimegeuka kuwa jini subiani ambalo limeenda kinyume na muelekeo wa kile chama tulichokuwa tunakijua na kuanza kunyonya damu ya Watanzania. ccm (sikukosea spelling), imekuwa kama cancer itokanayo na chembechembe nzuri za mwili wa binadamu, na kugeuka chembechembe mbaya ambayo inakula mwili huo huo. Matokeo yake ni cancer ambayo tusipoiondoa mapema, hakika itatuangamiza sote.
Najua kuwa wote ambao mnaotetea cancer hii mnafaidika nayo kwa njia moja au nyingine, hamna uchungu na mamilioni ya wananchi wanaosota na kutokuwa na matumaini ya siku za mbele, kwani wao wanaishi tu bora siku ipite...wanaishi maisha kama ya wanyama. Lakini wananchi wa Tanzania sio wanyama, ni binadamu wenye akili. Kuna siku, na siku hiyo inakuja, watatwaambua wabaya wao na kuwatoa madarakani. Wabaya hao sio tu kwamba watatolewa madatakani, bali pia watawajibishwa kwa matendo yao maovu waliyowafanyia Watanzania kwa kisingizio cha CHAMA CHA MAPINDUZI kilichoanzishwa mwaka 1977.
Sijui unaishi kwa hisia za rangi, lakini kila mtu ana rangi aipendayo, au katika jamii yake, rangi hiyo inaashiria nini. Binafsi, baada ya kuona unafiki unaofanywa na ccm dhidi ya Watanzania, kila nikiona hiyo rangi ya kijani nasikia kichefuchefu. Nikifungua tovuti nikiziona hizo rangi walizovaa wakinadi uongo kwenye majukwaa, nafunga tovuto hizo haraka.
Kama una hata chembe moja ya utu, utaacha kuishabikia ccm na kuiondoa madarakani, kabla haijakuangamiza hata wewe mwenyewe!
USA
UK
Japan
France
Quatar
Germany
Do your research bro.... Kumbuka hata Mwl. Nyerere, mmoja wa waasisi wa CCM na TANU alisema... "CCM siyo mama", waweza kubalisha chama any time. Mapenzi unayoonesha kwa CCM na sababu ulizotoa ni mufilisi.
ni kweli mwalimu alisema kuwa CCM sio mama yake kama ambavyo nnasema CCm sio mama yangu
mwalimu alikua muasisi wa chama na hadi anafariki alikua ni mwanachama muaminifu wa CCM
aliamini wazi kabisa kuwa bila ya CCM imara nchi yetu itayumba, kwa hio yeye daima aliamini CCM ni chama makini ila tunatakiwa kujipanga na kusafisha uchafu uliomo ambao ni kazi tunayoifanya sasa
karibu CCM tuijenge nchi yetu
mWALIMU nYERER
Vyema kabisa Mtu wa Pwani.
Nami nakubaliana nawe kwamba chama cha CCM kina hitaji kusafichwa kwa machafu yaliyomo, lakini mbinu za kukisafisha chama hiki kikongwe siyo moja. Natumaini utakubaliana nami kwamba - uking'ang'ania aina moja ya kufanya jambo la kurekebisha mapungufu katika kitu ni kuonesha ukosefu wa mbinu, utafakari na maarifa. Na kikubwa ni kuonesha ubishi na ungangari hali njia mbadala zipo na zinajulikana. Na njia kubwa iliyopo ni kuhakikisha CCM haiko madarakani, ili ipate kujionea mambo yanavyokuwa ukiwa nje. Maana viongozi wake wamejisahau. Hivyo kamanda wangu nakuasa - kula chochote hicho kiduchu wanachokupatia CCM, lakini ukifika kwenye chemba ya kupigia kura, wewe mpigie Dr. Slaa!! Baada ya hapo utaona CCM inajisafisha vizuri na kutakata. Nasi tutakuwepo kuisaidia. Na pale akina Slaa watakapo anza kuchemsha, tutakuwepo hapa JF kuwarushia madongo na kuwasawazisha.
Wajua kwamba, nchi nyingi zilizoendelea kwa demokrasia tuliyoamua kuifata sisi, zimeendelea kwa kuwa na mwanga na uwezo wa kuweza kubadili viongozi wao na vyama pale wanapochemsha.
CCm ni chama ambacho toka kuanzishwa kwake hadi leo hakijabadili muelekeo wake na dira yake ambayo ni
kujenga siasa ya kijamaa na kujitegemea
CCM ni chama thabiti ambacho kinaenda na jina lake ni chama cha mapinduzi, ni chama ambacho kiko tayari kwa mapinduzi (dynamic sio static Party) Mapinduzi ya nani?
CCM ni chama ambacho kina wanachama kama ilivyo vyama vyengine, sasa kila mwananchama ana tabia zake kama yeye binafsi, sio sahihi hata kidogo mapungufu ya mwananchama mwenyewe ukakivisha chama
sawa na kusema muumini wa dini fulani anazini na wake za watu, ukasema kwa vile huyu ni muumini wa dini ile kwa hio dini hio ni ya wazinifu wakati ukijua wazi misingi ya dini ile ikikataza uzinzi
CCM ni chama ambacho kiko tayari kujikosoa na kujisafisha tokea kale, ndio ukaona wahujumu wa uchumi wakati wa muasisi wake waliondolewa kwenye chama hata wakiwa ni wana CCM. pia wakati wa fagio la chuma wakati wa mwinyi wana CCM walionekana hawaendi na misingi ya chama wameondolewa, hivi karibuni waziri mkuu na mawaziri wengine wamewajibika( huoni kwenye vyama vyengine hayo). na kun a kesi ziko mahakamani na kama ingekua CCM haitaki hayo yatokee hakuna chama chochote kingethubutu kufanya hayo. Mbona leo Kikwete anawanadi na kusema hawana makosa?
CCM bado kinapambana kuwawezesha wanyonge wa nchi hii wafaidi rasili mali za nchi yao,ingawa wako baadhi ya wana CCM hutumia vibaya mamlaka yao kuwaumiza wananchi ila tukiwabaini tunawachomoa, na ndio hukimbilia upinzani Mbona Kikwete, Rostam Aziz, Chenge, Mramba, Lowassa hawajakimbilia upinzani?
ndio TUNASEMA upinzani wao DAIMA HUOKOTA PUMBA
hapana CCM haijachemsha, na kwa uchafu CHADEMA wao ndio hawafai kabisa, ndio ukaona hata wagombea wao wameanza kukihama chama huwezi kuona hilo CCM
mgombea wao hauziki ni mzinzi na mropokwaji, kila analoambiwa hukimbilia kulisema bila ya kufanya utafiti
ni chama kisicho na dira, ukiwauliza mnafuata mrengo upi hawajui, kila kiongozi tajibu vyake
ni chama cha wababaishaji na kimekaa kikanda zaidi
katu sirogwi wala sirukwi na akili kwenda kwenye chama kinachookoteza wagombea bila hata ya kuwapima
mtu katoka leo kwenye chama chengine hajasoma hata katiba wala hamumjui mnapa nafasi ya kugombea
kweli nyny mmepwerewa pwere
Mkuu, haina haja kwangu kuendelea kujadili maswala ambayo yameshajadiliwa kwa kina kila pahala hapa JF, na hata kwenye mitandao mingine. Kwa mwaka huu wa uchaguzi, kwangu mimi na wengi niwajuao, sababu kubwa ya kutopenda uongozi wa CCM uendelee kuongoza nchi yetu ni kuchoshwa na ahadi kemkem wanazoziasi pale wanapochaguliwa. Issue ya kuruhusu akina Mramba, Chenge na Lowassa waingie tena kugombea uongozi vimekera wengi. Na sasa wengi tumechoka, na tunaangalia alternative itatufanyia nini. Jiwe lililokataliwa na waashi... tunalijaribisha!!
Labda nikuachie hapa chini burudani itakayokufanya utafakari zaidi maamuzi yako ya kuendelea na kilekile kilichoshindwa kwa zaidi ya miaka 25:
Siku njema mkuu!!
Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiihaaaaaaa kweli ccm hoyeeeeeeeeeee
crapchama cha Mapinduzi ndio chama kilichozaliwa kutoka vyama vilivyotuletea ukombozi wa nchi zetu
ndio chama kilicholeta mapinduzi ya kifikra kwa watanzania katika nyanja mbali mbali, kama elimu, uchumi, afya na mengineo
ndio chama kilichojitolea kusimamia mapambano ya huru kwa bara la afrika na duniani kwa ujumla
ndio chama kilicholeta demokrasia na kuleta mfumo wa vyama vingi kwa amani bila ya vurugu
CCM imesimamia na kuwa nguzo ya amani ya nchi yetu
CCM ni chama ambacho kimechagua bendera yake kuwa kijani kwa kuamini :
rangi hio ni ishara ya maendeleo, ustawi, bahati, na ndio maana ukizungumzia usalama wa afya unawakilishwa na kijani, amani na usalama hata kwenye ICT connect ikiwa safi basi green color inapresent hilo
sio blue rangi ya mikosi
karibuni kwenye chama chenye neema na chama chenye demokrasia ndani ya chama na hata ktk kuendesha serikali zake zote mbili