Naipenda CCM na nitaipenda Daima kwa sababu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naipenda CCM na nitaipenda Daima kwa sababu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Sep 24, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  chama cha Mapinduzi ndio chama kilichozaliwa kutoka vyama vilivyotuletea ukombozi wa nchi zetu

  ndio chama kilicholeta mapinduzi ya kifikra kwa watanzania katika nyanja mbali mbali, kama elimu, uchumi, afya na mengineo


  ndio chama kilichojitolea kusimamia mapambano ya huru kwa bara la afrika na duniani kwa ujumla


  ndio chama kilicholeta demokrasia na kuleta mfumo wa vyama vingi kwa amani bila ya vurugu


  CCM imesimamia na kuwa nguzo ya amani ya nchi yetu


  CCM ni chama ambacho kimechagua bendera yake kuwa kijani kwa kuamini :

  rangi hio ni ishara ya maendeleo, ustawi, bahati, na ndio maana ukizungumzia usalama wa afya unawakilishwa na kijani, amani na usalama hata kwenye ICT connect ikiwa safi basi green color inapresent hilo

  sio blue rangi ya mikosi


  karibuni kwenye chama chenye neema na chama chenye demokrasia ndani ya chama na hata ktk kuendesha serikali zake zote mbili
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  Unaongelea CCM ipi? Kile chama cha wakulima na wafanyakazi au hiki chama cha mafisadi? Hivi ni vyama viwili tofauti kabisa vimebaki kufanana kwenye rangi tu na herufi za majina yao.
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  CCM hadi sasa hakijaacha kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi


  ni chama ambacho kinafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea


  ni chama kinachoumwa na shida za wanyonge
   
 4. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  List ya wanyonge:- Rostam, Lowasa, Chenge, JK, mramba, .........
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  katu si chama kinachokumbatia ubepari na ubeberu

  ndio chama ambacho kimewalea karibu wapinzani wote wa nchi na kuapa watakilinda mpaka kufa


  CCM ndio chama pekee ambacho kina utaratibu mzuri wa kiutawala, kinabadilishana uongozi kwa njia ya demokrasia na si chama cha kikabila wala cha kidini

  ni chama chenye sura ya kimuungano ambacho kina wabunge pande zote za muungano kwa kuchaguliwa na wananchi
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu nani amekudanganya hayo unayoyaamini?
   
 7. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mapenzi haya ni ya ushabiki sawa na ushabiki wa vyama vya mipira ambayo hayazingatii hali halisi ya jinsi Chama hicho kilivyokwenda nje ya misingi na kukosa mwelekeo. Hata muasisi Namba moja wa Chama ama vyama vya na TANU na CCM alishabaini uozo wa CCM na alikatamka wazi kwamba CCM sasa hivi ni sawa na kokoro linalosomba kila aina ya uchafu! Kwa bahati mbaya 'uchafu' huo ndio ambao sasa unalimaliza taifa la Tanzania.
   
 8. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  rangi ya kijani mahospitalini huzungushiwa kitanda chenye maiti hapo sasa hapo cjui utasemaje.

  ni kweli inaendesha serikali 2 moja ni hii ya mkwere na nyingine ni ya mafisadi

  ni chama ambacho kinasamimia uminywaji wa demokrasia nchini kwa nguvu zote hata kama kuuwa watu kama ilivyotekea 2001 Zenji mwaka huu tuombe MUNGU WASIFANYE HIVYO

  ccm ndio iliyofanya TANZANIA KUWA NYUMA KIELIMU HIVYO imeongeza utumwa kifikra badala ya kuupunguza.

  amani ya nchi hii imeletwa na upole wa WATANZANIA hata kama wananyanyasika.

  sasa baada kusaidia mapambano ya uhuru ya nchi zingine kama nchi tumefaidika na nini?
   
 9. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hapo zamani JamiiForums ilijiita " Forum for Great Thinkers". Sijui kama bado bado inaamini katika hilo?
   
 10. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  safi sana mtu wa pwani CCM DAIMA!!
  59997_115120691879448_108449092546608_116349_3161421_n.jpg
   
 11. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Wewe ulinyweshwa maji ya bendera ya chama na kupumbazika.AMKA!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  sisi ndio magreat thinkers wenyewe, ambao tulianza toka tukiita Jambo forums wala usiwe na khofu
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  yaani ndugu wewe kama unafikiri umemka basi nina mashaka umo ndani ya ndoto mbili...


  ccm_header1.jpg
   
 14. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  tunaendesha serikali mbili moja ya muungano na ya pili ni ya zanzibar

  mauaji ya 2001 ni sababu wapinzani hasa CUF kupuuza nguvu za serikali na kuvunja amani kwa hio kuonyesha serikali zinazoongozwa na CCM sio lege lege ndio yale yalitokea

  kuhusu suala la elimu hata hivi majuzi umoja wa mataifa na hata Rais Obama ameikubali Tanzania katika kupambana suala la elimu na tuzo tumepata tukiwa na serikali ya CCM


  tulichopata ktk harakati za uhuru ni kutimiza ile adhma yetu ya kuwa Tanzania haiwezi kuwa huru ikiwa bado nchi nyengine haziko huru


  Demokrasia imekua kwa kiasi kikubwa na ndio maana ukaona waizi wa wake za watu wanaendelea kutukana na kuzunguka bila ya kubughudhiwa
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Mbona ccm ni chama cha dini ya kiislamu na ndiyo maana waliweka mahakama ya kadhi kwenye ilani yao.............chama gani kingine kilichowahi kuweka kwenye ilani yake kuwa kitasaidia dini fulani....................kweli watz wanazidi kudanganywa kwa maneno badala ya kuangalia matendo...........ccm na kikwete wameonesha udini kwa vitendo lkn watu wanabuni maneno ya kupotosha umma................
  Siamini iwapo wana-ccm kweli ni watz
   
 16. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Huyu ndiye muwamuzi ....

  kura.jpg

  ole wenu wanachadema mumfanyie vurugu
   
 17. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  CCM kimeongozwa na wenyeviti wafuatao:

  J K Nyerere (Mkristo)
  A H Mwinyi (Muislam)
  B W Mkapa (Mkristo)
  J M Kikwete (Muislam)
  nionyeshe chama chengine mfano wa CCM katika kubalance mambo ya udini?

  suala la kadhi halikuingizwa kwa sababu ya udini na wakati huo walioandaa ilani ya chama wengi hawakuwa waislam (kama Mh Kingunge) waliona kuna umuhimu wa sehemu ya jamii wa watanzania kutekelezewa matashi yao ambao ni haki na ni sehemu ya kutekeleza imani yao. kitu ambacho CCM inaheshimu na kuthamini michango ya dini zote ktk kuimarisha amani na ustawi ktk taifa letu.

  chama kingine kilichoweka ni chama cha NCCR wakati ikiongozwa na Mrema


  CCM inathamini michango ya dini zote na ndio maana ukaona mwenyekiti wake anahudhuria hafla za dini zote na anapokea ushauri wa dini zote

  ingelitaka CCM ingepitisha suala la Kadhi ila baada ya kusikiliza wananchi wameona waangalie utaratibu mwengine wa kuwawezesha waislamu kutimiza ndoto yao

  CCM ilifuta misamaha ya kodi na ilipoenda bungeni na kusikia kilio cha wakristo iliamua kubadilisha msimamo, ni chama pekee chenye kusikiliza shida za watu
   
 18. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  nishalieleza kuwa hiki ni chama cha watanzania na hata wapinzani wameapa kukilinda mpaka kufa
   
 19. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1976 wakati nilipokuwa JKT, tuliambiwa tuchague jina la chama kipya kitakachotokana na muungano kati ya ASP na TANU. Vikao kama vile vilifanyika na baada ya hapo tukaambiwa kuwa jina la chama litakuwa Chama Cha Mapinduzi, na mboni zake ni jembe na nyundo kuashiria kinawakilisha wakulima na wafanyakazi. Tuliamini sana chama hicho na wengine tulikuwa tayari kufa kupigania sera na maadili ya chama hicho, maadili ambayo tulikuzwa nayo na yalitekelezwa kwa vitendo.

  Kwa bahati mbaya sana, nasikitika kusema, kile chama ambacho kilitulea, ambacho kilikuza na kuumba fikra zetu (ambazo ndizo zinazonifanya niandike haya,) chama hicho kimegeuzwa na watu wachache wapendao uchu wa madaraka, wanaojilimbikizia mali na kukuza usultani. Chama hicho kimegeuka kuwa jini subiani ambalo limeenda kinyume na muelekeo wa kile chama tulichokuwa tunakijua na kuanza kunyonya damu ya Watanzania. ccm (sikukosea spelling), imekuwa kama cancer itokanayo na chembechembe nzuri za mwili wa binadamu, na kugeuka chembechembe mbaya ambayo inakula mwili huo huo. Matokeo yake ni cancer ambayo tusipoiondoa mapema, hakika itatuangamiza sote.


  Najua kuwa wote ambao mnaotetea cancer hii mnafaidika nayo kwa njia moja au nyingine, hamna uchungu na mamilioni ya wananchi wanaosota na kutokuwa na matumaini ya siku za mbele, kwani wao wanaishi tu bora siku ipite...wanaishi maisha kama ya wanyama. Lakini wananchi wa Tanzania sio wanyama, ni binadamu wenye akili. Kuna siku, na siku hiyo inakuja, watatwaambua wabaya wao na kuwatoa madarakani. Wabaya hao sio tu kwamba watatolewa madatakani, bali pia watawajibishwa kwa matendo yao maovu waliyowafanyia Watanzania kwa kisingizio cha CHAMA CHA MAPINDUZI kilichoanzishwa mwaka 1977.


  Sijui unaishi kwa hisia za rangi, lakini kila mtu ana rangi aipendayo, au katika jamii yake, rangi hiyo inaashiria nini. Binafsi, baada ya kuona unafiki unaofanywa na ccm dhidi ya Watanzania, kila nikiona hiyo rangi ya kijani nasikia kichefuchefu. Nikifungua tovuti nikiziona hizo rangi walizovaa wakinadi uongo kwenye majukwaa, nafunga tovuto hizo haraka.


  Kama una hata chembe moja ya utu, utaacha kuishabikia ccm na kuiondoa madarakani, kabla haijakuangamiza hata wewe mwenyewe!
   
 20. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Chama kinachothamini fedha za wagombea wake wa nafasi za uongozi kuliko maadili yao, ndo maana Jambazi na muuaji wa Maalbino amepewa tiketi ya CCM kugombea ubunge jimbo la Muhambwe.
   
Loading...