Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,304
- 12,965
CHADEMA imeitisha maandamano nchi nzima kupinga bunge la katiba kuendelea huku ikijulikana wazi kuwa katiba mpya haitapatikana. CHADEMA ni mojawapo ya vyama vinavyo unda umoja wa katiba mpya - UKAWA. Mimi naona kwa CHADEMA kuitisha maandamano peke yake ni kama kujitenga na vyama vingine vinavyounda UKAWA na hivyo kudhoofisha nguvu ya pamoja. Ingekuwa ni vizuri CHADEMA ikashirikiana na vyama vyenza vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi - UKAWA. Kwa CHADEMA kutoka chenyewe ni kudhoofisha nguvu ya pamoja unless waseme kuwa wenzao wamekataa. Wakumbuke kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Ilitakiwa wafanye kwa pamoja na wenzao kama walivyotoka bungeni na viongozi wakuu wa vyama hivyo ndio wangeongoza maandamano hayo ingeleta impact kubwa kuliko hivi CDM walivyoamua kutoka kivyao vyao. Hii ni kama kusema CUF, NCCR, DP na wengineo watoke kivyao, sasa nini maana ya UKAWA??!!. Hiyo itakuwa sawa na kujenga mnara wa baberi