Naiona hatari kubwa sana hatua ya Serikali kupeleka walimu wa Sekondari kufundisha shule za msingi

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Walimu wazidiwa na vipindi sekondari kwani halmashauri zingine zimelitekeleza zoezi la uhamisho bila utaalamu kabisa na sijui ni hujuma za makusudi ama laa.

Hata timu ya mpira huwa ina hakiba ya wachezaji kwa ajili ya dharura lakini kwa hiki kinachofanywa sasa kwenye elimu sehemu nyingi hawajaacha akiba kabisa yaani hadi wameacha upungufu Sekondari

Shule ya ******* Sekondari ina walimu 11 na ina wanafunzi 349 na kati ya walimu hao walimu wanne wameshapewa barua kwenda shule ya msingi.

Kuna kitu sijaelewa hapa mwalimu akiugua maana yake watoto hawasomi somo hilo.

Walimu wakihama au kustaafu shule hiyo watoto hawasomi.

Mwalimu akiwa kwenye likizo ya uzazi watoto hawasomi kwa muda huo.

Watoto wakiongezeka katika usajili hasa wa kidato cha kwanza mwakani hasa kwa hili la elimu bure ambalo litazidi kuongeza idadi ya wanafunzi sekondari kwa kuzingatia idadi ya watoto waliopo shule za msingi.

Sijaelewa lengo la hiki wanachokiita kinawashusha walimu wa sekondari kufundisha shule za msingi.

Bado utafiti unaendelea maana hadi sasa walimu mashuleni hawafundishi kabisaaa na hawana hamu ya kufundisha sababu hawaelewi kesho yao maana hadi sasa maofisa wanawatisha kila mara mara ntakutoa wewe mara yule hadi hamu ya kazi haipo

Lakin pia Bunge limedanganywa pia na waziri husika na wizara yake ni waongo maana walichoambiwa ni tofauti na kinachofanyika na wanaohamishwa si wale walioongelewa na waziri bungeni hasa kwa utafiti wa shule ambazo tayari walimu barua wameshapewa.

Si kweli kwamba wanaohamishwa ni waliojiendeleza habari hizi Serikali imedanganya Bunge na wananchi kwa ujumla bali wamehamishwa ambao hawakuwahi kuwa walimu shule ya msingi.

Serikali inaendeshwa kwa uongo na usanii mwingi na ujanja ujanja lakini hakuna faida bali ni hasara tupu kwa taifa hasa kwa sababu inaongozwa na watu wasioelewa uongozi bora.
 
Magufuli oyeeee Ccm mbele kwa kwa mbele, Ccm inashughulikia matatizo ya watu na watu wameona ndiyo maana wanaichagua.
 
walimu wazidiwa na vipindi sekondari kwani halmashauri zingine.zimelitekeleza zoezi la uhamisho bila utaalamu kabisa na sijui NI hujuma.za.makusudi ama.laa

hata timu ya mpira huwa ina hakiba ya wachezaji kwa ajilI ya dharura lakin kwa hiki kInacho fanywa sasa kwenye elimu sehemu nying hawajaacha hakiba kabisa yaani hadi wameacha upungufu sekondari

shule ya ******* SEKONDARI. Ina walimu 11 na ina wanafunzi 349 na Kati ya walimu hao walimu wanne wameshapewa barua kwenda primary.

kuna kitu sijaelewa hapa mwalimu akiugua maana yake watoto hawasomi somo Hilo

walimu wakihama au kistaafu shule.hiyo watoto hawasomi

mwalimu akiwa.kwenye likizo ya uzazI watoto hawasomi kwa mda huo

watoto wakiongezeka katika usajili hasa wa kidato cha kwanza mwakani hasa kwa hili la elimu bure ambalo litazidi kuongeza idadi ya wanafunzi sekondari kwa kuzingatia idadi ya watoto waliopo shule za.msingi

sijaelewa lengo la hiki wanacho kiita kiwashusha walimu wa sekondari kufundisha primary

bado utafiti unaendelea maana hadi sasa walimu mashuleni hawafundishi kabisaaa na hawana hamu ya kufundisha sababu hawaelewi kesho Yao maana hadi sasa maofisa wanawatisha kila Mara Mara ntakutoa wewe Mara Yule hadi hamu ya Kazi haipo

lakin pia bunge limedanganywa pia na waziri husika na wizara yake NI waongo maana walicho ambiwa NI tofauti na kinacho fanyika na wanao hamishwa si wale walio ongelewa na waziri bungeni hasa kwa utafiti wa shule ambazo tayari walimu barua wamesha pewa

si kweli kwamba wanao hamishwa NI walio jiendeleza habari hizi serikali imedanganya. bunge na wananchi kwa ujumla Bali wamehamishwa ambao hawakuwahi kuwa walimu primary

serikali inaendeshwa kwa uongo na usanii mwingi na ujanja ujanja lakin hakuna faida Bali NI hasara tupu kwa taifa hasa kwa sababu inongozwa na watu wasio elewa uongozi bora.

Kinachoendelea kwa sasa JPM atawaweka ndani wapinzani na kuwanyanyasa sana lakini wanaomuharibia si wapinzani bali ni wanaCCM wenzake ambao ndiyo amewateua kuwa wakurugenzi,Wakuu wa Mikoa/Wilaya na makatibu wakuu.Namuoenea huruma mno siku akija kufunguka macho Mzee wa watu anaweza hata akafa kwa kihoro
 
Walimu bwana... nyie sio wa kuwaonea huruma. Kipindi cha uchaguzi mnatumika sana kutuibia kura zetu. Nyie pigweni tu
 
Magufuli oyeeee Ccm mbele kwa kwa mbele, Ccm inashughulikia matatizo ya watu na watu wameona ndiyo maana wanaichagua.
na huo ndio upumbavu na ujonga tulio achiwa na watawala wetu kuingiza siasa hata kwenye mambo ya kitaalam na ndio maana itabakivkuwa nchi ya wajinga na wapumbavu daima. asante.
 
Kinachoendelea kwa sasa JPM atawaweka ndani wapinzani na kuwanyanyasa sana lakini wanaomuharibia si wapinzani bali ni wanaCCM wenzake ambao ndiyo amewateua kuwa wakurugenzi,Wakuu wa Mikoa/Wilaya na makatibu wakuu.Namuoenea huruma mno siku akija kufunguka macho Mzee wa watu anaweza hata akafa kwa kihoro
taifa linavurugwa kila sehemu.
 
Ni raha sana kupelekwa primary. Huna haja ya kujiandaa kufundisha kwani kule mambo ni mtiririko...mambo ya Coordination, genetics etc yote unatua chini..

Ila wanasema siku upungufu ukitokea sec watarudishwa tena
 
Habarini wanajamvi.....

Hivi ni kweli secondary kuna walimu wa kutosha kiasi kwamba wapelekwe primary kufundisha??

Sasa kama kweli kuna walimu wa kutosha mbona waliopelekwa primary ni wale ambao ni wasumbufu?,watoro?,walevi, na wale wanaohojihoji? kwanini??

Kwann wapelekwe hao?

Je serikali ina lengo la kufuta kazi wakiendelea na hali hyo wakiwa huko primary? maana wengine wameendelea na hali ile ile waliyokuwa nayo wakiwa secondary!

Hii inaweza ikawa namna ya kuwapunguza watumishi wa umma?

Swali langu kwanini wapelekwe wale ambao ni wasumbufu?

Je ilikuwa n lengo la serikali? au kuna hitilafu sehemu?

Nawasilisha......
 
Mkuu ulikuwa msumbufu? Unadhani mkuu wa shule anaweza kumpendekeza mtu ambae si msumbufu ashuke chini akuache wewe msumbufu? lakini kama mshahara ni uleule tatizo liko wapi wasiwasi wangu Mimi ni kuwa huko mbeleni hata uwo mshahara utapunguzwa tuombe Mungu atakayeachiwa rungu hasiwe na frustration kama za huyu jamaa
 
Mkuu ulikuwa msumbufu? Unadhani mkuu wa shule anaweza kumpendekeza mtu ambae si msumbufu ashuke chini akuache wewe msumbufu?

Mm siyo msumbufu aseeeee,

Kwanza nafundisha Masomo ya Science hata ningekuwa msumbufu asingenitoa.......

M sina time na Mkuu,natimiza tu wajibu wangu.......
 
Mm siyo msumbufu aseeeee,

Kwanza nafundisha Masomo ya Science hata ningekuwa msumbufu asingenitoa.......

M sina time na Mkuu,natimiza tu wajibu wangu.......
Ok mkuu nadhani hiki kikombe kitasaidia kuwashtua walimu wenzako ili wakati wa uchaguzi wasitumiwe kama kipindi cha nyuma
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom