Naiomba Serikali ya chama cha mapinduzi ifute mfumo wa vyama vingi

Alex Xavery

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
230
196
Mimi ni muumini wa CHADEMA, nina ndugu, jamaa na marafiki wengi sana wa ccm.

Ombi langu, tumieni mamlaka mliyonayo hata kwa wingi wa wabunge mlionao mfute siasa za vyama vingi Tanzania, uhai ni bora kuliko utamu wa madaraka tunaougombea, rasilimali watu ni nyenzo mojawapo ya ustawi wa taifa lolote ikiwa patakuwa na umoja, upendo na mshikamano baina yao wote kama ambavyo mh. raisi wa awamu ya tano alivyowahi kutolea mfano taifa la China.

Kama mnaona pana utamu sana hapo kwenye madaraka na mngependa ccm itawale milele mnayo mamlaka ya kukibakisha chama kimoja ccm mpaka Yesu atakaporudi na mle na kunywa miguu juu ya meza bila mapambano, hira, chuki, fitna, ufilauni na vita katika hichi kinachoitwa siasa za vyama vingi.

Ikiwa si hiari yenu na mnalazimishwa na kubanwa mbavu na wenye utimamu wa akili mtekeleze siasa za vyama vingi basi ni vyema muwe tiyari kukipa chombo huru mamlaka ya kusimamia maamzi ya wananchi bila kuingiliwa na utashi wa wanaogombea, kura zipigwe waziwazi ikiwezekana nje kweupe na zihesabiwe wazi wazi nje kweupe na kwa sauti, na baada ya matokeo waumini tupeane mikono na kupongezana kwa furaha bila kuonyeshana chuki hata chembe kisha turudi kufanya kazi kwa pamoja tukicheka na kufurahia mchuano ulivyokua, na huu ndio ustawi wa demokrasia, uchumi wa taifa na watu wake.

Lakini hali ya kisiasa ikiachwa iendelee hivi ilivyo basi ni hatari kwa taifa hili na watu wake, imani za watu katika vyama haziwezi komeshwa kwa kuwajeruhi na kuwaua waumini, ni vyema sasa serikali ya chama cha mapinduzi mfanye maamzi ya busara kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani duniani, chagua kuitekeleza demokrasia ya vyama vingi bila uhuni na ufilauni au kuifuta demokrasia ya vyama vingi, haya yote mawili yapo ndani ya uwezo wenu.

Ikiwa mna hofu ya Mungu ndani yenu basi mtaguswa kuyapenda maisha ya watu wa taifa hili kuliko ulafi wa madaraka. Kila mtu atakufa na hatoondoka wala kuzikwa na chochote anachokipigania kwa sasa juu ya uso wa dunia lakini kila mmoja atajibu kivyake mbele ya hukumu.

Narudia tena, mimi ni muumini wa CHADEMA lakini nina ndugu, jamaa na marafiki wengi ccm, nilitarajia tutachuana kwa uwazi na kupeana mikono baada ya matokeo ya wazi na huru kama ilivyotokea ndani ya jimbo letu la Bukoba mjini 2014-2015 lakini kwa kilichotokea uchaguzi wa marudio mpaka watu kupigana mapanga na wengine kuua kabisa ambavyo ni matokeo ya maagizo ya baadhi ya wanasiasa wenyewe majukwaani si dalili nzuri kwa taifa letu.

Tunajengeana chuki baina yetu wenyew bila sababu za msingi na chuki ikikomaa matokeo yake ni mabaya sana.

Serikali ya chama cha mapinduzi chagueni moja na litekelezwe kwa ukamilifu kwa ajili ya uhai wa watanzania wote. Ni imani yangu mtatekeleza.

Asanteni sana.

Alex Xavery
 
Umesema wewe ni chadema?

Hujui kama chadema wanapokea ruzuku au unataka ufukuzwe uanachama maana kama unataka kumpokonya mbowe tonge mdomon

Uliza uongoz wa chama chako ile milion 200 kila mwez anayochukua lowasa huwa ni ya kaz gan?
 
Wewe jamaa unaota...hvi kwa akli yako chadema ije itawale kweli? Una akli au matope? Nahsi akli yako imejaa funza...mtakufa haraka kwa misongo ya mawazo isiyo na tija....kuna kiongozi gan huko chadema wa kumpa nchi....?? Chama hakina hata ofsi..hi taabu kwel kwel..

Sasa jibu ni hvi: Chadema haiwezi kupewa hii nchi by any means ova...walijisajili wenyewe wakajifute kwa msajili wenyewe..hakuna haja ya kumpeleka mara ooh sijui mswaada...tunalojua ni moja tu CCM itatawala milele...watavurugana wao, watarogana, Watapigana but mwisho wa siku raisi anatoka CCM
 
Slowly,

Acha hizo watarogana wao watavurugana wao vipi? CCM ndiyo inavuruga chadema inawadhoofisha kwa kuwanunua madiwani kisha uchaguzi ukirudiwa wanafanya uchakachuaji mtupu, kwa awamu hii ya Tano upinzani haupo huru hakuna Demokrasia na msongo wa mawazo unaletwa na Udikteta wa CCM kwa kuzuia mikutano kuwabambikia kesi kuwakomoa kuwadhalilisha chadema kupitia polisiccm,
 
Umesema wewe ni chadema?

Hujui kama chadema wanapokea ruzuku au unataka ufukuzwe uanachama maana kama unataka kumpokonya mbowe tonge mdomon

Uliza uongoz wa chama chako ile milion 200 kila mwez anayochukua lowasa huwa ni ya kaz gan?
Propaganda za kumsingizia Lowasa vingi haina uhusiano na mbinu ya CCM kurejesha mfumo wa chama kimoja kwa mbinu haramu za kuwapiga Risasi akina Tundu lisu kuwabambikia kesi Wapinzani kuwakomoa kuwakoroga kununua madiwani kwa pesa za Umma, CCM mjue mwisho wa Ubaya ni Aibu hakuna mabaya yasiyo na mwisho kila baya lina mwisho wake ipo siku CCM watajutia unyama wao dhidi ya Wapinzani.
 
Kodi inalipwa na watanzania wote wakiwemo Wapinzani cha ajabu hao hao CCM wanakwenda Hazina kuchota pesa kumpatia Lipumba Maliyamungu Bashite, le mutuz na kikundi chake cha akina Jerry muro wazitumie kudhoofisha upinzani, pesa za walipa kodi zinatumika na wachache kwa mambo ya hovyo hovyo kuwanunua madiwani makusudi wanapoteza pesa za Umma ingawa wakakula 10% humo humo kisha kurudia uchaguzi ambao haukupaswa kuwepo kama kusingekuwa na hujuma dhidi ya Chadema.

Chaguzi zinapoteza pesa nyingi ambazo zingeweza kufanya maendeleo makubwa, CCM ni chama kisichojali pesa za Umma kutafunwa na Madalali wa Siasa wapo tayari wakose maendeleo lakini waweze kuikomoa chadema, kwa sasa maendeleo ya CCM ni kuikomoa chadema pekee ukibuni mbinu ya kuidhoofisha chadema ukampelekea Maliyamungu Bashite akaikubali huomba pesa kwa Mtukufu malaika wa chato mara moja na kazi ya kuidhoofisha chadema inaanza, kwa sasa ni mradi wa mkubwa wa kuvuna pesa za walipa kodi kwa kisingizio cha kuzitumia kuwakomoa kuwadhoofisha chadema.
 
Matunda ya ziara ya Sirro Rwanda yameonekana. Chadema wajifunze mbinu waliyotumia wakenya kupata katiba mpya. Kulalamika kwenye mitandao hakutaizuia ccm kufanya figisu.
 
Nitawashangaa sana kama kuna watu watashupaa tena na kujiita wapinzani.Akili ya kawaida inaniambia kadri mnavyoshupaa na kujiita wapinzani ndivyo mnavyoipa uhalali ccm kuwa hivyo ilivyo.

Mwanzo niliwashangaa akina Kafulila,lakini sasa naanza kuwaheshimu maana wameona mbali.Hebu tususie upinzani ibaki ccm pekee.

Hii italeta mabadiliko ya kweli.Hatuhitaji kuona watu wakimwaga damu eti tu kwa sababu wanataka wapigiwe kura kupitia upinzani!

Bora waziombe kura hizo hizo kupitia ccm kwa amani kabisa.Tuwanyime kazi wale walioajiriwa kutesa na kuua,sote tuwe ccm.
 
Nitawashangaa sana kama kuna watu watashupaa tena na kujiita wapinzani.Akili ya kawaida inaniambia kadri mnavyoshupaa na kujiita wapinzani ndivyo mnavyoipa uhalali ccm kuwa hivyo ilivyo.

Mwanzo niliwashangaa akina Kafulila,lakini sasa naanza kuwaheshimu maana wameona mbali.Hebu tususie upinzani ibaki ccm pekee.

Hii italeta mabadiliko ya kweli.Hatuhitaji kuona watu wakimwaga damu eti tu kwa sababu wanataka wapigiwe kura kupitia upinzani!

Bora waziombe kura hizo hizo kupitia ccm kwa amani kabisa.Tuwanyime kazi wale walioajiriwa kutesa na kuua,sote tuwe ccm.
Kuwa ccm ni sawa na kumbaka mama yangu mzazi, ni dhambi inayostahili mauti ndani ya sekunde tangu kuifanya.
 
Wewe jamaa unaota...hvi kwa akli yako chadema ije itawale kweli? Una akli au matope? Nahsi akli yako imejaa funza...mtakufa haraka kwa misongo ya mawazo isiyo na tija....kuna kiongozi gan huko chadema wa kumpa nchi....?? Chama hakina hata ofsi..hi taabu kwel kwel..

Sasa jibu ni hvi: Chadema haiwezi kupewa hii nchi by any means ova...walijisajili wenyewe wakajifute kwa msajili wenyewe..hakuna haja ya kumpeleka mara ooh sijui mswaada...tunalojua ni moja tu CCM itatawala milele...watavurugana wao, watarogana, Watapigana but mwisho wa siku raisi anatoka CCM
Hahaha.. Kwa namna ulivyoandika tu inaonesha wewe ni mtu wa namna gani, in short wewe ni mmoja wa wale wanaojeruhi na kuua kwa mapanga hivyo na wewe ni sehemu ya tatizo linalotafutiwa ufumbuzi.

Gaddafi alikuwa strong than any mpuuzi na takataka zote za ccm na ma dictators wengine wote but mwisho wao huwa ni mbaya tu, asili ya mwanadamu ni uhuru, ukimbania tu uhuru hata kama unampa maziwa na asali ipo siku atakudhuru.

Eti kuna mtu CHADEMA wa kumpa nchi! nchi ni taasisi boya, siyo mali ya mtu kufanya anavyotaka kama sasa, ndiyo maana kuna katiba, sheria, kanuni na miongozo, so citizen yeyote anayekubalika kikatiba anaweza kuiendesha nchi bila kujali ni ukoo gani wala chama gani.

Nisipoteze zaidi muda wangu, naweza kuwa namjibu kipofu wa fikra, I am humanitarian thats why nikaandika hivi sio wewe mpuuzi usiyejali matokeo ya uvunjaji wa haki za watu.
 
Nitawashangaa sana kama kuna watu watashupaa tena na kujiita wapinzani.Akili ya kawaida inaniambia kadri mnavyoshupaa na kujiita wapinzani ndivyo mnavyoipa uhalali ccm kuwa hivyo ilivyo.

Mwanzo niliwashangaa akina Kafulila,lakini sasa naanza kuwaheshimu maana wameona mbali.Hebu tususie upinzani ibaki ccm pekee.

Hii italeta mabadiliko ya kweli.Hatuhitaji kuona watu wakimwaga damu eti tu kwa sababu wanataka wapigiwe kura kupitia upinzani!

Bora waziombe kura hizo hizo kupitia ccm kwa amani kabisa.Tuwanyime kazi wale walioajiriwa kutesa na kuua,sote tuwe ccm.
Hahaha.. Sio hiari kuwepo kwa siasa za vyama vingi kijana labda kama huelewi hizi mambo, au hujui kama 80% ya wana ccm walizikataa siasa za vyama vingi!? na kwa nini Mwl. Nyerere akavipitisha? unahisi ilikuwa ni kwa hiari yake. Serikali ya ccm kama ina jeuri iviondoe kwenye katiba ndo utajua duniani kuna watu hawapendi upuuzi juu ya maisha ya wengine.
 
Hahaha.. Kwa namna ulivyoandika tu inaonesha wewe ni mtu wa namna gani, in short wewe ni mmoja wa wale wanaojeruhi na kuua kwa mapanga hivyo na wewe ni sehemu ya tatizo linalotafutiwa ufumbuzi

Gaddafi alikuwa strong than any mpuuzi na takataka zote za ccm na ma dictators wengine wote but mwisho mpuuzi usiyejali
Wewe ni matako....zero kabisa....Ghadafi alikufa je nchi imefaidika nini? Sadam alikufa nchi imefaidika nin? Kuna nini kule Kongo? Kwa nini zimbabwe chama tawala bado kinatawala mbali na mapinduz...huwezi kuipa chadema nchi...hapo ni kuwauzia wazungu kila kitu...ni heri risasi zitumike kuzuia hyo hali lofa wewe...mpak wazungu wanasikitika kwa yanayotokea Libya, wewe unayafurahia kisa una chuki ya kufukuzwa kazi
Screenshot_20171128-163914.png

FB_IMG_1511876400563.jpg
 
Amani iwe nanyi japo nahisi kwa Tanzania hatuna tenà amani. Nimesikitshwa sana na mauji ya RAIA wasio na hatia japo kwa serikali ya ccm hawana cha kupoteza kwa sababu wanaouliwa na kupotea Ni wafuasi wa vyama vya upinzani.

Ukiacha mauji yaliopita Jana ameuawa mwanafunzi wa chuo NIT mwaka was kwanza na ameuawa na police tofauti na huko nyuma waliokufa wameuliwa na watu wanaosemekana wasiojulikana.

Jana waziri was mambo ya ndani amewaagiza police kuwachunguza na kuwakamata watu wasiojulikana. Wakati anatoa agizo hilo jioni ya Sikh hiyohiyo police wanamuua binti wa watu bila kuawakosea.

Naishauri serikali ya ccm, kwa kuwa INA wabunge wengi na majeshi yote; wapelekevmuswada bungeni wabadilishi katika wafute sura na ibara ya katiba yetu ilioanzisha vyama vingi vya siasa tupaki na chama kimoja ili kuepusha uhasama na mauji yanayoendea tena kiholela.

Namsahauri mwenyekiti wa chama cha mapinduzi atoe japo rambirambi kwani Ni MTU wa nyonge na ametuaminisha maendeleo hayana chama alieuawa Ni kijina tena Ni msomi Ni nguvu kazi ya taifa hili. Wala asilaani aendelelee kukaa kimya kwani ubinadamu Ni kazi, azingatie maona ya wazee na viongozi wa dini; kwa mfano ushauri wa askofu kakobe ameshauri serikali ya ccm irudishe mfumo wa chama kimoja isiue watu. Sote tumeshuhudia TRA Ikimwandama kumbe hivi ss kusema ukweli Ni dhambi unaweza kupotea.

Mwisho naishauri serekali sikivu ya ccm izingatie ushauri wa baraza la maaskofu wa katoliki Tanzania juu ya democrasia na Uhuru wa vyombo vya habari na Uhuru wa kujielejiza kwa mujibu wa ibara 18 ya katiba ya nchi ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa Mara.

Mungu tunusuru na maasia.
 
Hata mimi ningependa kuona hichi kitu kinatokea.

Nina hamu ya kuona ni mabadiliko gani yatatokea endapo nchi ikiwa ni ya chama kimoja. Mabadiliko ambayo yameshindikana angali CCM ikimiliki Bunge kwa zaidi ya 90% tangu mwaka 95.

Hii falsafa ya Magufuli itaenda kushindwa vibaya mno. Na imedhihirisha wazi huu ni uongozi unaopoteza mwelekeo siku hadi siku.

Huwezi kutumia resources za nchi kutaka kumiliki 10% ya cake ya upinzani angali wewe una uwezo wa kufanya chochote
bungeni. None sense,

Najua kwa speed ya hila za sasa hivi upinzani hautavuka 2020 ila natamani nione hicho kitachokuwa cha tofauti ukishakuwa na control ya bunge kwa 100%

Period!
 
Back
Top Bottom