NAIOMBA SERIKALI IJE NA MAJIBU SAHIHI KUHUSU HILI

Tizzo G

Member
Jun 9, 2012
25
17
Ndugu wanajamvi hamjambo?
mimi binafsi sijapendezeshwa na hali ya serikali kuagiza kukamatwa kwa gari au pikipiki zinazopita katika barabara ya magari ya mwendokasi ile hali magari hayahaya ya mwendokasi yanaenda nje ya mipaka yake. kwa mfano, barabara za magari ya mwendokasi zinaishia kimara mwisho, sasa mbona magari haya yanaenda mpaka mbezi mwisho ile hali hamna barabara yake rasmi? basi kama yanaweza kutembea sehemu ambayo sio rasmi kwao basi wayaruhusu pia kwenda gongo la mboto, mbagala na kwingineko.
kwanini mbezi mwisho? na pia nina shaka na ukusanyaji wa mapato kwa sababu zile tiketi zinazogawiwa pale mbezi mwisho zinakusanywa punde unapopanda gari hilo pale mbezi mwisho, kama kweli ni njia halali kwanini zile tiketi zinakusanywa na haziingizwi kwenye system ili zitambulike kama zimeshatumika?

anaejua mawasiliano ya waziri wa uchukuzi pamoja na waziri wa tamisemi awaalati ili waje na majibu ya msingi katika hili. nakerwa sana na hili maana naona kama kuna dalili mbaya ya upotevu wa mapato ya serikali.
 
Back
Top Bottom