Naioana Tanzania mpya iwapo Majimbo yataridhiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naioana Tanzania mpya iwapo Majimbo yataridhiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Hunter, Oct 20, 2011.

 1. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Naamini maendeleo ya dhati ya Tanzania yataanzia pale katiba mpya itakapoanza kufanya kazi;
  naamini mfumo wa majimbo ukikubaliwa mambo kama;

  1.Umiliki wa vyanzo mbalimbali vya mapato utabaki chini ya jimbo husika na hii ina maana senator atakuwa ndo mkuu wa jimbo, hivyo scope ya kiuongozi itakuwa ndogo hivyo kumfanya senator kumudu jimbo lake.

  2.Pia mambo ya ubadhirifu yatadhibitiwa kwa urahisi maana kutakuwa na ukaribu toka kwa kiongozi wa juu mpaka wa chini.
  3.Nafasi ya majimbo kuendelea itakuwa kubwa ikizingatiwa kutakuwa na nafasi kubwa ya viongozi wa majimbo kuishi majimboni mwao
  tofauti na sasa ambapo kila kiongozi anakimbilia kuishi Dar. mfano ni viongozi wengi wa Zanzibar wanaishi zanzibar japo kuna wachache wabishi
  bado wanaishi dar, huku wakiongoza Zanzibar.
  4.Ule wizi wa ki bluetooth kama ulioripotiwa pale KIA, ambapo mwizi mkuu yupo dar huku akiratibu wizi kilimanjaro hautakuwepo, kwani gap toka
  alipo kiongozi na mwananchi itakuwa ndogo hivyo kiongozi ataona yote yanayotokea hivyohivyo mwananchi.
  5.Uzalendo utarejea kwani kwasasa tumeona viongozi wengi hususani wakuu wa mikoa hawana uzalendo na hari ya kuleta maendeleo katika mikoa waliyomo hasa inapotokea wao ni wenyeji wa sehemu tofauti na hapo, Tujiulize kama mbunge flani labda wa Kibondo anapoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa sehemu ambayo mbunge wa pale ni kutoka chama pinzani unafikiri ataleta au kuwaza kuleta maendeleo.
  6.Kutakuwepo na shindani wa kimajimbo katika maendeleo, jambo ambalo litakuwa bora kwa mustakabali wa Tanzania tunayoitaka
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,198
  Likes Received: 10,540
  Trophy Points: 280
  yale yale ya kwenye biblia mwenye nacho ataongezewa! kwa level hii ya maendeleo bado hatujafikia huko mkuu still kuna mikoa bado haiwezi kujiendesha yenyewe inahitaji tafu kidogo kwenye mikoa ambayo inamaendeleo atleast. By the way wazo zuri.
   
Loading...