Naingia kwenye kufuga kuku chotara(Saso)

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
2,629
2,000
Kumbuka haya
1.Kuku ili watage wanahitaji chakula lishe nzuri sana ili 50%-60% ya kuku watage mayai kwa siku(huwa hawatagi kuku wote kwa siku)

2.Kuku anakula kwa uzito.yani in kilograms siyo kwa debe.kwa hiyo debe moja la chakula kwa kuku 25 labda ni 4days tu.unaweza walisha mwezi ila hautapata matokeo tarajiwa .

4.Ufugaji siyo shughuli ya kujaribu,ni yakudhamiria na kujipanga.

4.Ukipekela mayai 100 utapata vifaranga around 66 mpaka 70.
5.Tafuta taarifa za watalaamu wa mifugo ili uweze kunufaika na ufugaji.otherwise utatengeneza umaskini zaidi na ugonjwa wa moyo
 

CoderM

Member
Jun 15, 2015
60
125
Hiyo namba nne ni uongo, na Kama ilikutokea ujue una tatizo, Kama sio kwenye mayai(hayana mbegu au uliyahifadhi vibaya baada ya kutagwa) au incubator inayotumia Ina tatizo.

Kama mayai yako vizuri incubator(ikiwa inarun under best environment ina uwezo wa kutotolesha kwa asilimia 100.

Kuhusu chakula huenda nilikosea mahesabu lakini kuku wangu wa miezi miwili na nusu wanakula debe moja wiki nzima bila hydroponics Wala funza. Nikieka na hivyo wanakula wiki mbili.
 

Geniustin

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
4,161
2,000
Nimefuga sasso 500 mwaka jana walikuwa wanakufa sana tofauti nanikifuga kroiler ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho.kila la kheri sasso mi mazuri kwa nyama siku kuhusu kutaga.sasso wanahitaji bio security yakutosha, hewa ya kutosha sio banda umetengeneza kama chumba cha kulala. Nasemea hao wengi maana 25 sio kaz kufuga.Dawa ya minyoo usisahau, Wape Newcastle wakifika minne.Ndui kama hawakuchanjwa watapukutika wote.muulize aliyekuuzia kama alichanja ndui.All the best
Mkuu, je akiwachanja ndui..na ikatokea kumbe awali walichanjwa! Kutakuwa na madhara?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom