Naikumbuka kauli hii ya KIKWETE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naikumbuka kauli hii ya KIKWETE

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bujibuji, Jul 27, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,056
  Trophy Points: 280
  View attachment 11955 RAIS Jakaya Kikwete ameushangaza umma wa Watanzania baada ya kuanza kukiuka misingi iliyokiunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuwaheshimu Wakulima na Wafanyakazi pale alipokutana na wazee wa MSkoa wa Dar es Salaam na kutoa hotuba kali akiwashutumu viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafabnyakazi Nchini (Tucta) kuwa ni wanafiki kwa kuendelea kushinikiza mgomo wa wafanyakazi licha ya mazungumzo yanayoendelea kati yao na Serikali.

  “Hawa viongozi wa Tucta walisema sisi serikali ni watu wasioambilika… hawa viongozi wa Tucta ni waongo,” alisema Rais Kikwete akisisitiza kuwa hii ni moja ya sababu iliyomfanya jana awajibike kujibu.

  “Sasa iweje tunakubaliana hili, kesho yake asubuhi unazungumza kama hatujakubaliana,” alisema Rais na kusisitiza: “Ninayo kila sababu kuhoji dhamira zao iwapo kweli wana nia thabiti ya kuwabeba wafanyakazi ama wana lao jambo.”
   
 2. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Nadhani wafanyakazi wa Tanzania wako katika lile kundi la 70% ambao ni mbumbumbu na hufuata mkumbo, ndo maana JK alisema hivyo with confidence!

  Ukweli wote tutauona mara tu baada ya Oktoba 31.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,056
  Trophy Points: 280
  Mazuzu magic watampa tu kura zao
   
Loading...