Naibu Waziri Wizara ya Kilimo na ukuu wa mkoa

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Kumbukumbu zangu zinaonyesha, mara kadhaa manaibu waziri wa wizara ya kilimo wanapata bahati ya kuteuliwa kuwa wakuu wa mikoa

Nakumbuka mzee Stephen Masato Wassira, alikuwa naibu waziri wizara ya kilimo, baadaye hayati Mwalimu Nyerere akamteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mara

Mzee Njelu Kasaka, alikuwa naibu wizara ya kilimo, baadaye hayati Rais Benjamin Mkapa akamteua kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa kisha baadaye Tabora

Adamu Mallima, alikuwa naibu waziri wa wizara ya kilimo, baadaye akateuliwa na hayati Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Mara

Ndugu yetu Godfrey Zambi, alikuwa naibu waziri wa kilimo, baadaye hayati Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli akamteua kuwa mkuu wa mkoa Lindi

Na sasa Onary Mgumba, alikuwa naibu waziri kilimo, na sasa mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amemteua kuwa mkuu wa mkoa wa tatu wa mkoa mchanga kabisa wa Songwe

Inawezekana wapo na wengine miaka ya nyuma huko
 
Back
Top Bottom