Naibu Waziri: Wananchi wapunguze matumizi ya sukari, kwanza sio nzuri kiafya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
brown-sugar-vs-coconut-sugar.jpeg

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutanisha wizara ya Viwanda na Biashara na wadau wa sukari nchini kuangalia uwezekano wa kushusha bei bidhaa hiyo kuelekea mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Mfungo huo unatarajiwa kuanza takriban siku tisa zijazo. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya wakati akizungumzia kupanda kwa bei ya sukari kunakosaidiwa kusababishwa na upungufu wake sokoni. Aidha alisema kuwa kutokana na kupanda kwa bei ya sukari, amewataka wananchi kutumia asali kama mbadala.

“Wananchi wapunguze matumizi ya sukari, kwanza hata kiafya sio nzuri sana, kama mtu asali haimdhuru basi ni bora akatumia asali,” alisema Manyanya.

Asali kwa sasa inauzwa kati ya Sh 12,000 hadi 15,000. Akielezea sababu za zaidi alisema kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, nchi nyingi zimesimamisha uzalishaji na pia mvua nyingi katika baadhi ya maeneo imesababisha uzalishaji kuwa mdogo.

“Mvua nyingi zinasababisha changamoto katika uzalishaji wa sukari, ile miwa ikiwa na maji mengi uzito wa sukari unapungua,” alieleza Naibu Waziri.

Hata hivyo, gazeti hili limebaini katika sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa wafanyabiashara wanaficha sukari na kuuza kwa kificho kwa bei juu ambapo wananchi wanalazimika kutoboka mifuko yao na kununua bidhaa hiyo kati ya Sh 3,000 hadi 4,000 kwa tofauti ya kati ya Sh 800 hadi 1,800 ya bei elekezi.

Upandaji huo wa sukari umeelezwa na wafanyabiashara wa rejareja kuwa unatokana na wao kupandishiwa kwa sasa mfuko wa kilo 50 .

Mfanyabiashara wa rejareja, White Tarimo akizungumza na gazeti hili, alisema, “Kwa sasa hata sisi tunapandishiwa wiki iliyopita mfuko wa kilo 50, tuliuziwa kati ya shilingi 136,000 mpaka na 140,000 maduka ya jumla na sisi tukauza rejareja kati ya shilingi 3,000 hadi 3,600.

Chanzo: HabariLeo
 
Hiyo ndio kauli ya Waziri baada ya tatizo kutokea! Mbona hakusema kabla?

Shida wengi wakurupukaji! Walishaharibu toka mwanzo walipojaribu maamuzi yao ya protectionism za sukari inayozalishwa ndani huku uwezo wa viwanda vyetu mdogo kukidhi mahitaji!

Waache kuungilia soko huria.
 
Makubwa haya, kwani si walikuwa wanalalamika magala.yao yamejaa sukari haitoki sababu ya sukari ya nje! Mara tena imekuwa adimu? Jamani nchi yangu mchawi nani hapa kwetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sisi tuliosoma Marketing hasa masuala ya DEMAND ... HII NI ELIMINATING DEMAND ..Kwa tunatengeneza sababu ili kupunguza DEMAND ..hapa ni kwasababu demand imekuwa kubwa kuliko product Manafucturing ... Pia unaweza kupunguza demand Kwa kuongeza bei ya juu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom