Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Mwikabi akiongea na TBC Live leo asubuhi, amesrma kuwa hakuamini kama yeye angeteuliwa na a Rais Dk. John a Pombe Magufuli kuwa Naibu Waziri serikalini. Amesema amekuwa na historia ya uongozi katika maisha yake kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.
Alisema amekuwa Kiongozi nafasi zote katika Elimu ya Msingi; Kiongozi katika nafasi zote za elimu ya sekondari; na Kiongozi pia katika Chuo Kikuu.
Amesema amejiandaa kutekeleza wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.
Alisema sifa Kuu ya Kiongozi ni kufanya maamuzi. Hivyo atajitahidi kushirikiana na wenzake katika utekelezaji wa majukumu yake. Alisema kwenye Wizara, tukishakubaliana kufanyia kazi jambo fulani, kama hujalikamilisha hadi deadline, basi tutatafutana ubaya.
Mwita alisema kuwa yeye siye mkali wala mbabe bali huwa anatumia akili katika kufanya maamuzi. Alisema yeye hapendi mzaha ndio maana wakati mwingine anaonekana ni mkali. Hivyo, alikanusha na kudai kuwa yeye siye mbabe.
Aliongezea juu ya umuhimu wa kutekeleza yote wanayokubaliana ikiwa ni pamoja na kutoa feedback.