Naibu Waziri wa Serikali ya JK akiri kushindwa Kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Waziri wa Serikali ya JK akiri kushindwa Kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Nov 7, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amewasihi wanafunzi wa elimu ya juu nchini kuandamana ili kushinikiza waliokopeshwa fedha za elimu miaka ya nyuma walipe ili wapewe wengine. Amesema wahitimu wengi walikopeshwa zaidi ya Sh21 bilioni ili kusoma kwenye vyuo mbalimbali, lakini baada ya kupata kazi wanakwepa kulipa mikopo hiyo.

  Mlugo alisema wanaosoma vyuoni sasa hawana budi kuandamana ili kuwashinikiza waliotangulia walipe fedha hizo ili ziweze kukopeshwa kwa wanafunzi wengine zaidi. "Fedha hizo zilikopeshwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu tangu utoaji wa mikopo ulipoanza mwaka wa masomo wa 2004/05 na kama zitapatikana zitaiwezesha Serikali kukopesha wahitaji wengi zaidi kuliko idadi ya sasa", alisisitiza. Naibu Waziri Mulugo alisema hayo alipozungumza kwenye sherehe za mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Mount Meru eneo la Ngaramtoni, nje kidogo ya mji wa Arusha.

  Nionavyo mimi Waziri huyu wa JK amekiri kushindwa kazi aliyopewa na bosi wake na hivyo kuwataka wanafunzi wa elimu ya juu kupitia maandamano wamsaidie kushinikiza waliokopeshwa fedha hizo wazirejeshe. Nimeshtushwa na kauli hii ya waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha hayo madeni yanarudi akigawa kazi kwa wanafunzi ili wanafunzi wakishindwa kuandamana "vizuri" ionekane wanafunzi ndio wameshindwa kushinikizwa zirejeshwe. Ni utendaji wa aina hii hii wa Mawaziri/watendaji wetu wameifikisha nchi yetu hapa ilipo, hali ni hivi hivi TIB, EPA, na maeneo mbalimbali ambayo Serikali imekopesha.

  Je hii maana yake ni kwamba Waziri hana takwimu za waliokopeshwa???Huu utaratibu wa kutaka walokopeshwa warejeshe pesa hizo kwa maandamano ya wanafunzi umeanza lini?? Kama ni utaratibu mpya wa kudai mbona hamjatuambia tuandamane kudai 40 Bil za Kagoda na zaid ya 130 Bil za Deep Green na ndugu zake???Au zile hazifai kusomesha wanafunzi wetu au zile huna uchungu nazo kwa vile mmekula ninyi viongozi???Uchungu huo Waziri wa Serikali hii umeupata wapi wakati kila kukicha mnafanya ufisadi??unatutaka tuandamane wakati mmesema Al Shabaab wanatuvizia lengo lako ni nini????au Al shabaab wameshatoweka???? Huoni kufanya maandamano ya kipuuzi kama hayo ni kulishushia Taifa hadhi kwa kushindwa kwako kufanyakazi????Kama kunaugumu wa kupata fedha hizo kutoka kwa wanafunzi waliokopeshwa, kweli majizi ya EPA yalirejesha fedha zetu au sanaa tu????

  Mi nadhani unataka kuficha uzembe wa Serikali kwa kuwatupia lawama waliokopeshwa. Hakuna asiyejua kuwa Serikali ni legelege. Hivyo kwa kuwa mshashindwa kufwatilia Kagoda, Deep Green na Tangold zenye zaidi ya 200Bil zilizoliwa na majizi, nashauri hata hizi mlizokopesha wanafunzi mtemane nazo kwani zimerudi kwa walipa kodi wenyewe.

  Mwisho, kwa kukiri kushindwa kulifanyia kazi suala dogo kama hili, nadhani umepoteza sifa ya kuendelea madarakani mana hujui ulifanyalo na ninashauri ujiuzuru mara moja mana inaonekana unalipwa mshahara wa bure na kulitia Taifa hasara. Wanajamvi naliwasilisha kwenu ili tujadili kama Tanzania hii choka mbaya inahitaji Waziri mwenye utendaji wa kibabaishaji kama wa aina hii wa kutaka marejesho kwa maandamano?????

  Source: Mwananchi Sunday, 06 November, 2011[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Kwani Intelijensia ya uwepo wa Al Shabab Haitakuwepo?
  Arudi tu kijijini akalime kwanza uwaziri umemshinda
   
 3. m

  muvimba Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Inaonekana hajui anatakiwa kufanya nini kutimiza wajibu wake
   
 4. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Msaidieni jAman ila mnavyofanya hivyo jipangeni saana mana Police wa Tz mmmmmmm
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Huyo naibu waziri kweli hamnazo,, huh...!
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  yule bwana no form six leaver....
   
 7. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Like Father like Son.
   
 8. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huyo Mlugo(naibu waziri) amekosa cha kuongea, waliosoma enzi za mwalimu nyerere bila shaka na yeye akiwemo tena bure kabisa wanadaiwa na nani? anaosema wamepata kazi alafu wanakwepa kulipa deni amewaona wapi!! ni takribani asilimia 4 ya waitimu wanaoajiriwa kila wanapomaliza Chuo wanaosalia ni kuganga njaa mitaani: huyu naibu waziri kama ameshindwa kuwa mbunifu ktk uhamasisha upatikanaji wa mapato kwa serikali yake huku alikoelekea inabidi aandike kuwa ameliwa.
   
 9. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mimi nilisoma miaka ya 1996 hadi 1999 na ninalipa mkopo wangu kila mwezi nakatwa kwenye mshahara wangu! Huyu waziri hajui kazi yake, yeye na wizara yake wanatakiwa kufuatilia wadaiwa wote!
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hatuna muda wakupoteza tena kwa uzembe wao
   
 11. TEMPOLALE

  TEMPOLALE JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yule jamaa kweli aliishia form Six hakufanya vizuri sana ikabidi aombe Tempo sehemu kufundisha pale Mbeya katika shule moja ya Muhindi iitwayo Southern Highland Secondary School. Inasemekana ana vinguvu vya giza kutokana na maneno ya watu wanao mzunguka, maana from no where yule Muhindi akampatia u-head master wa ile shule na katika mazingira ya kutatanisha yule Mhindi akakimbia nchini akaelekea Canada na kumkabidhi ile shule aendeshe kama yake, baadaye ikagundulika katika taratibu za elimu form six asingeweza kuwa headmaster wa shule ya secondary hivyo akajipa umeneja wa shule na kuteua Headmaster mwingine, baadaye akaamua kusoma Open University(Namna alivyoimaliza elimu ya Open University ndo kichekesho kabisa na kwa bahati mbaya zaidi ilimu hiyo anatakiwa kuitumia kuendesha wizara) Hii kamaliza siku chache kabla ya kwenda kugombea ubunge, alipata nguvu za kugombea ubunge maana pesa yote ya shule ni kama yake na kutokea kipindi kile mpaka leo ile shule ni kama yake, kuna uvumi uliozagaa Mbeya mjini kwamba kampumbaza kabisa yule mmiliki hataki kabisa kurudi nchini. Wanaomfahamu kielimu Huyu Mlugo wanadai hata cheti chake cha form six alicho ajiriwa nacho pale shuleni alichukua cha jamaa mmoja aliyekuwa anaitwa Philipo Mulungu, ukitaka kuthibitisha hilo nenda pale Southern Highland Secondary School muulize mwalimu yeyote atakuambia jamaa anafahamika kama Philipo Mulungu nasiyo Philipo Mlugo. Nina wasi wasi kama ikatokea mtu akaamua kufuatilia huyu mtu lazima atamkuta na kosa la kufoji. Mulungu ni mtu tofauti na Mlugo. Lakini huyu Mlugo aliajiriwa pale Shuleni kama Mulungu.
   
 12. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kweli hakuna aliye msafi ndani ya CCM, kila mtu anakaufisadi kake na ndiyo maana hawawezi kunyoosheana vidole!!
   
 13. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Huyo Mh.Philipo Mlugo amesoma enzi za Mwinyi na Mkapa hivyo siyo babu ki-hivyo! Hajafika 40years lakini issue ni kwamba kama ulikopeshwa na serikali huna budi kurejesha mkopo ili hiyo pesa iendelee kusomesha wengine! Tatizo hapa Watanzania ni wabinafsi sana!
   
 14. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Si ni Serikali hii hii ya Philipo Mulugu iliyokataza SIASA kwenye vyuo vya Elimu ya juu?!
  Inakuwaje leo Waziri awashauri tena wanafunzi kufanya siasa (maandamano) vyuoni?
  Hivi hawa CCM kila kiongozi huwa anakuja na lake? Kwanini hawana common standing?
  Au ndiyo dalili za chombo kwenda mrama?!
  Ingawa common sense is not always common to commoner, lakini mimi ningeushauri
  waziri angewahamasisha wanafunzi kundama kushinkiza fedha za EPA, TBI, deep green
  Meremeta, majengo pacha BoT ambazo ni nyingi zaidi kuliko hiyo mikopo, na ambayo
  iko mikononi wa watu wachache > 10 people, kuliko maelfu ya wahitumu ambao in
  the first place hawakuiba ni kodi zao.
   
 15. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kwa uongezea,
  Huyo naibu waziri, alianza kufoji tangu shule ya msingi, na baadaye alifanikiwa kuwenda Songea Boys huko nako hakufanya vizuri ndo maana nadahni alienda Meta au Sangu Mbeya (zote private) ambapo napo hakufanya vizuri na hapo alipofanya huo umafia wa kum-yahaya muhindi wa shule ya southern highlands. Kwa ujumla uwezo wake ni mdogo sana. Kinachofanyika katika nchi hii ni kwa sababu bosi wao naye ndo hivyo hivyo, uwezo mdogo na wasaidizi wake wengi uwezo ni mdogo.
   
 16. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Majungu hayajengi,unamjua huyu au umeletewa habari usizokuwa na uhakika nazo halafu unazi-share na watu wengine bila kujali kwamba unaudanganya umma!

  Mseme Mlugo kwa matatizo yake mengine lakini hayo ya background yake hayatusaidii kwasasa!
   
 17. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #17
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Na pia ni uchafu wa mtu ndani ya CCM unaomfanya aweze kuvumilia na kuendelea kukaa ndani ya CCM. Kwa utaratibu huu mtu msafi na mwadilifu hawez kuwapo CCM hadi leo hii.
   
 18. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #18
  Nov 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hiyo haina neno, tuliokopeshwa na tukafanikiwa kupata ajira tuko tayari kulipa kwa mtindo wa kukatwa kidogokidogo; lkn je hao 96% wasiokuwa na ajira itakuaje? au maandamano ya wanafunzi ndo yatapelekea kurejeshwa kwa huo mkopo????
   
 19. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,161
  Likes Received: 1,250
  Trophy Points: 280
  Serikali ya JK imejaa mawaziri wengi vipute, huyu hata ukimuuliza ni wahitimu wangapi waliomaliza wameajiriwa au kujiajiri ataishia kutoa takwimu za uongo, na ukimuuliza hao walioajiliwa wao kama serikali waliokuwa na dhamana ya kuwakopesha wamechukua hatua gani kuhakikisha wanalipa hiyo mikopo atajibiwa sijui, aache kutuaminisha mambo ya kipuuzi kama haya
   
 20. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani hakuna aliyekataa kulipa na wala huwez kukataa kulipa ingawa utaratibu wa kuanzia 2004/5 hatujaelewa/hatujaelewa ni kigezo gani kilitumika ilhali utaratibu wa kukopeshwa ulianza siku nying. Tatizo hapa ni Serikali ambayo inaonekana haina utaratibu wa kukusanya hayo madeni na utaratibu inaotaka kuutumia ili kupata hizo fedha ni kwa migomo na maandamano. Hawa viongozi hawataki kujifunza, kwanini wasijifunze kwa wenzao madeni yanakusanywaje??? Ukiangalia mafile yao muda mwingi wanashinda nje ya nchi, sasa kama suala dogo kama hili hawalielewi je masuala complex wataweza watendaji kama hawa????
   
Loading...