Naibu Waziri wa Mazingira apongeza uwekezaji kiwanda cha A to Z Arusha

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
ARUSHA

KIWANDA cha kutengeneza nguo na vyandarua kilichopo jijini Arusha,A to Z kinatarajia kuongeza ajira kwa vijana baada ya kuwa na mipango ya kuzalisha bidhaa za plastiki kutokana na taka ngumu za chupa za maji na mifuko ya safleti.

Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho Viral Shah, aliyazungumza hayo jana wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Hamad Chande, alipofanya ziara ya ukaguzi ya siku moja.

Shah alisema kiwanda chake kinatarajia kukusanya taka ngumu aina ya chupa za maji na mifuko ya saflet, kuzichakata na kutengeneza malighafi kwaajili ya kutengenezea vifungashio vya plastiki ambavyo hutumika kwaajili matumizi ya maduka makubwa ya jumla na reja reja.

Alisema tayari utafiti wa uwekezaji huo umeshanza na kupata tathmini, kuwa zoezi la kukusanya taka ngumu aina hizo litatekelezwa na vijana katika wilaya
6 za Mkoa wa Arusha na vianga vyake vyote.

"Vijana watakuwa wamepata ajira wakisubiri matarajio ya ajira walizosomea, watakusanya chupa na kusubiri magari ya kiwanda kuziputia na watalipwa kwa mwezi.Tutawapa vitambulisho maalumu vya kiwanda ili wasibughudhiwe, lakini pia tutaomba baraka za Wizara inayohusika ili kufuata miongozo na taratibu zilizopo"alisema

Shah alisema tayari kiwanda chake kimeshanunua mashine moja ya kutengeneza malighafi kutokana na takangumu za chupa za maji, ambazo zitatengeneza ndoo, vikapu vitokanavyo na plastic ambacho ni rafiki wa mazingira.

"Tutahakikisha hakuna taka ngumu aina ya chupa za maji zinazagaa mitaani, chupa badala ya kuwa kero sasa zinageuka uchumi na ajira, tunaomba Serikali ijiandae kutupatia wataalamu katika kutekeleza mpango huo ili tuibue ajira kwa vijana"alisema.

Aidha aliitaka Serikali kutambua mchango wa kiwanda chake cha A to Z kwani hadi sasa kimeajiri wafanyakazi Watanzania zaidi 800.Kiwanda hicho hutengeneza vyandarua maalumu kwaajili ya kujikinga na malaria na kusambaza kwa Nchi za Afrika.

Naibu Waziri Hamad Chande alishukuru jitihada na maono ya kiwanda hicho, kwani zaidi ya kuindolea kero Serikali itokanayo na kuzagaa kwa chupa za maji lakini pia kusaidia ajira na kipato kwa vijana hilo likiwa ni kipaumbele na ahadi za Serikali kila wakati.

"Hilo ni jambo jema anzeni tutawapa ushirikiano wote utakaohitajika, naomba na wawekezaji wengine Nchini waige hili,tupanue wigo wa ajira lakini pia na usafi wa mazingira yetu ambayo sote tunayategemea ili tuendelee kuishi"alisema.
View attachment 1819473
IMG_20210612_121603_1.jpg
 
Back
Top Bottom