Naibu Waziri wa Mambo ya ndani asitisha Uraia wa Warundi 162,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani asitisha Uraia wa Warundi 162,000

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sagamawe, Sep 17, 2012.

 1. s

  sagamawe Senior Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesikia majuzi kuwa Naibu waziri wa mambo ya ndani amesitisha utoaji wa uraia wa watu 162,000 ambao hapo awali Lawrence Masha alikuwa ametangaza kuwapatia uraia wakati akiwa bado waziri. Mwenye habari zaidi naomba anijuze. Aksante
   
 2. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mabo=mambo
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Hili suala la utoaji wa uraia kwa wageni yafaa litafutiwe utarabu mzuri katika katiba mpya,utaratibu wa sasa unawapa wanasiasa mwanya wa kutuchezea namna watakavyo.
   
 4. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  wiki chache zilizopita niliona watu zaidi ya 100 (website ya uhamiaji) wenye majina ya kisomali wamefutiwa uraia wa tz kwasababu walijipatia uraia kwa njia zisizo halali na ninavyofahamu anayeidhinisha uraia ni waziri pekee... ni swala la kuhoji ilikuwa vipi mpaka waziri kutoa uraia kwa watu wasiostaili?
   
 5. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Safi sana!
   
 6. E

  Escherichia Coli Senior Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amesimamisha zoezi la utoaji uraia(baadhi walishapatiwa) ili kupata maoni ya wanaodaiwa kuwa wadau ambao inatamkwa kuwa hawakushirikishwa ktk mchakato huo.Hata hvyo kama wewe ni mmoja wao au jamaa yako yumo,usiwe na hofu kabisa.Makambi yote ya wakimbizi yalishafungwa(mwezi wa nane tumefunga kambi ya mwisho) na kwa mjibu wa mapatano ya TZ na UNHCR,tanzania hakuna mkimbizi tena.Wakimbizi waliochaguwa kubaki tz( 162,000) ni lazima watambuliwe kama jamii ya tz lkn utaratibu wa kuwatambua ndio bado unajadiliwa upya.Leo kuna kikao cha wawakilishi wao(vijana wasomi),ujumbe wa wizara na mwakilishi wa UNHCR.Nikirudi ofsini after a week ninaweza kukuhabarisha kama maamuzi yao hayatakuwa confidential!
   
 7. D

  Dido Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kambi ya mtabila itafungwa mwishoni mwa mwaka huu na ya Nyarugusu bado haijafungwa. Kambi ipi ya mwisho iliyofungwa?
   
 8. E

  Escherichia Coli Senior Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwezi wa nane ulikuwa mwezi wa mwisho kutambua uwepo wa kambi ya Nyarugusu.Kama bado kuna wakimbizi hawajaondolewa ni matokeo ya udhaifu ktk utaratibu wa kuwasafirisha.
   
 9. D

  Dido Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unamaanisha Mtabila? Maana wakimbizi wa kutoka Burundi waliokuwa wakiishi mtabila ndio walioondolewa hadhi ya ukimbizi mwezi wa nane, na si wakimbizi wa kutoka DRC waliopo kambo ya Nyarugusu.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naomba mwenye kujual hili atufafanulie; kisheria nani mwenye mamlaka ya 'kusitisha' au kutoa uraia? waziri au naibu waziri, au katibu au nani?
   
 11. Root

  Root JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,274
  Likes Received: 12,989
  Trophy Points: 280
  warudi kwao then wafate Wachina na Wahindi
   
 12. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,867
  Likes Received: 2,807
  Trophy Points: 280
  Mkuu uko ofisi gani wewe?

  Nakubaliana na wewe kuhusu kutoa uraia lakini sikubaliani na wewe kuhusu kufungwa makambi kwamba mwezi wa nane mmefunga kambi ya mwisho. Siyo kweli mkuu! Kambi iliyofungwa ni ile ya Warundi (Mtabila) lakini bado tuna kambi moja ilyobaki ambayo ina wakimbizi zaidi ya 60,000 (Nyarugusu) ambayo inahifadhi wakimbizi wa kutoka Congo. Hivyo kwa wale wa Mtabila ambao wameonekana sababu zao ni za msingi kuendelea na ukimbizi (hii inatokana na mambo ya usalama) watahamishiwa Nyarugusu, hayo ndo makubaliano yaliyopo kwenye Tripartite Commision (Burundi, Tanzania na UNHCR).

  Kwa wale 162,000 siyo rahisi kuwafutia uraia maana yalikuwa makubaliano ya hayo makundi matatu. Hapo wakuu tulishaumia lazima tukubali kwamba imeshakula kwetu!
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,867
  Likes Received: 2,807
  Trophy Points: 280
  Mkuu usichanganye madawa!

  Naona hapa unataka kutuchanganyia taarifa. Kambi ya Nyarugusu bado inatambuliwa kama kambi rasmi, hii ni kutokana na hali ilivyo DRC kwa sasa. Kati ya 2010 na 2011 kulikuwa na exchange visits nyingi zilizokuwa zinafanyika ili kuona kama hali ni shwari lakini ilikuja kuonekana kwamba isingekuwa busara kuwarudisha kwao wakati bado kuna mapigano kule kwao. Hivyo zoezi la kuwarudisha likawa limekwamba. Kwa hiyo Nyarugusu itaendelea kuwepo na baadhi ya wakimbizi wa Mtabila (wenye matatizo ya kiusalama), haya nia maamuzi yaliyotolewa baada ya indepth interview iliyofanyika kati ya Oktoba na Novemba 2011, watahamishiwa huko mara tu Mtabila itakapofungwa rasmi mwishoni mwa Disemba 2012.
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  Strongly kwa sababu za kiusalama warundii warwanda wote waliopewa uraia na watakaopewa uraia ....wewe relocated Hadi maeneo yenye Nafasi Kati Kati mwa nchi ....au kusini hata kaskazini ...,historian imeonyesha kuwa kawaacha hawa maeneo Yetu ya magharibi au ziwa ...lake zone miaka 20 ijayo watamega Eneo Letu kuwa nchi Hizo ambazo zinawatumia Hao waliambizi kimkakati ili kumega Eneo Letu ...na kutuletea usumbufu Kama wa Banyamulenge wanaompaa Kabila sasa Ambapo Eneo la mashariki limegeuka kama Jimbo la Rwanda....
  Kwa walio serekalini hasa usalama wa Taifa na usalama wa Jeshi (MI) ...wanaujuwa Huu mikakati wa majirani zetu wa kujitwalia Kagera,Kigoma na sehemu ya Rukwa....Wazo la kuwahamishia maeneo Mbali na mpaka warundii na warwanda wanaopewa uraia lilianza toka Enzi ya utawaka wa Mwalimu ,,,ambapo aliwapa vijiji mkoani Tabora waliambizi wa mwanzo wa Rwanda wa miaka ya 60 ......
  karibuni makosa yanacanyika kawaacha hawa tunaowapa uraia mikoa ya mipakanii tutakuja kuwaachia watoto wetu matatizo ......hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Kagera amelalamika kitendo cha majirani zetu kujipenyeza na wengine hata kupata uongozi wa mitaaa...na Kashiria uchaguzi Ujao kwa wingi wao wanaweza hata Kuamua Mbunge.......Ameomba pesa za kuwahamisha wahamiaji haramu kuwarudisha makwao....ni vema akapewa.....
  pia inashaauriwa ianzishwe security strip Kuanzia Kagera ...Hadi Kigoma usawa wa mipakanii tuweke mashamba ..makubwa ya kilimo yamilikiwe na Jeshi ..JkT ...hata Kama wataweka wawekezaji ....but this area is vulnerable need to be owned by defence..hawa raia wanarubuniwa wanauzia wageni maeneo ya mipakanii ni hatari...na wanaonunua wanfadhiliwa na agencies za majirani ...Kama sehemu ya mikakati
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Kuna wakimbizii wa Somalia wamepewa Eneo Soni ,Tanga...hawa inasadikika kuwa hawa Hilo lilikuwa eneo Lao la Asili na walihamia Somalia miaka 150 iliyopita ....na wanatambulika Kama jamii ya waswahili Somali .....at least Somali ni Mbali but strongly tutafute vijiji Mbali na mikoa ya pembezoni tuwahamiashie hawa wakimbizii 162'000 ....kwani hawa miaka 20 ..ijayo watafikia hata millions 5.....na wanafanya Ukanda wote huo uungane na Hao majirani....na mwisho wataanza kuchukua maagizo ya kiutawala toka huko....time bomb!!!!
   
 16. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Escherichia Coli jamaa yangu msije mkatutia hasira bure humu yaani wote 162,000 mnataka kuwapa Uraia wakati Zanzibar wameahidi kutoa vitambulisho vya ufanyaji kazi tu kwa wanaotoka Bara na sio vya Uraia au makazi na ina maana wafanyabiashara hawatatambuliwa Ninyi mnataka kutuingizia wengine kwanini wasipewe vya ukimbizi?
  Kumbuka walikuwepo tele maofisini lakini baada ya ile ndege ya Rais wao (Habyarimana na Kagame kuchukua Nchi) walirudisha uraia na kukimbilia kwao (kuna afisa wa MAPATO enzi hizo alioa msukuma alimuacha na leo yuko kwao na Cheo kikubwa tu na kaoa Mtutsi mwenzake
  Acheni kujipendekeza nampa Hongera huyo Naibu Waziri km kavifutilia mbali
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Nyarugusu na Mtabila zote waliongeza muda.Mtabila sasa ni official mwisho mwezi wa 12.Nyarugusu Bado kwani wengi wanatoka East Kongo na huko bado kuna mcharuko.
   
 18. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  You are damn right!
   
 19. B

  Bi Mashavu Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amesimamisha zoezi la utoaji uraia(baadhi walishapatiwa) ili kupata maoni ya wanaodaiwa kuwa wadau ambao inatamkwa kuwa hawakushirikishwa ktk mchakato huo.Hata hvyo kama wewe ni mmoja wao au jamaa yako yumo,usiwe na hofu kabisa.Makambi yote ya wakimbizi yalishafungwa(mwezi wa nane tumefunga kambi ya mwisho) na kwa mjibu wa mapatano ya TZ na UNHCR,tanzania hakuna mkimbizi tena.Wakimbizi waliochaguwa kubaki tz( 162,000) ni lazima watambuliwe kama jamii ya tz lkn utaratibu wa kuwatambua ndio bado unajadiliwa upya.Leo kuna kikao cha wawakilishi wao(vijana wasomi),ujumbe wa wizara na mwakilishi wa UNHCR.Nikirudi ofsini after a week ninaweza kukuhabarisha kama maamuzi yao hayatakuwa confidential!

  Hivi Maagizo ya Waziri aliemaliza muda wake huweza kutenguliwa na Naibu Waziri Mpya? Nadhani hapa tunarudi katika siasa zetu uchwara (kama alivyosema mheshimiwa mmoja aliejiuzulu nafasi yake). Taratibu na kanuni za msingi za kutoa uraia zipo tena kwa mujibu wa sheria, na endapo suala litaonekana si la kawaida (kwa mfano kutoa uraia kwa watu 162,000 +++) mijadala ya wazi iwepo na kuwajumuisha wadau mbalimbali kabla ya kufikia hitimisho la kuutangazia Umma. Hili suala limekuwepo tokea 2007, leo ni 2012 na bado linapelekwa kwa wadau (what for?) ina maana ikikataliwa watu hao watanyang'anywa uraia ambao tayari wameshapewa? Ikikubalika uanzishwe tena mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kwamba wasambazwe nchi nzima au la? Itakuwa mwaka gani?
   
Loading...