Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani apiga mkwara Jeshi la Zimamoto

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Yusuf Masauni amepiga marufuku askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji kwenda sehemu zenye majanga ya moto bila kuwa na uhakika kwamba vitendea kazi pamoja na magari yenye maji ya kutosha, vinaweza kuhimili na kudhibiti maafa ya moto na kuonya kwamba ofisa wa jeshi hilo atakayeruhusu uzembe huo serikali haitasita kumuajibisha.

Naibu waziri huyo wa mambo ya ndani ya nchi, ameyasema hayo wakati akizungumza na askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji wa wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza.

Baadhi ya viongozi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mwanza wamemweleza naibu waziri Hamad Yusuf Masauni baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo.

Jumla ya matukio 38 ya moto na mengine 23 ya uokozi yametokea katika mkoa wa Mwanza.

Wizara ya mambo ya ndani imeajiri askari 800 wa jeshi la zimamoto na uokoaji katika mwaka huu wa fedha ulioanza julai mosi ambao wanasubiri kupangwa katika vituo vyao vya kazi ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto za uhaba wa askari na vitendea kazi yakiwemo magari.
 
Yuko sahihi, wanaenda na magari yakifika eneo la tukio mara waseme maji hayatoki pampu imegoma mara maji gari haina maji, hiyo sio bongo muvi kweli?
 
Kuna kitu hakipo sahihi hapa, ikumbukwe gari ya zimamoto inahitaji kujaza maji maara tuu baada ya maji iliyokuja nayo kumaliza, maji haya huisha haraka sana kutokana na high pressure inayotumika, hivyo dv/dt inakwenda haraka zaidi.

Miundo mbinu ya miji/mitaa inatakiwa iwe na facility maalum ambazo zishajengwa ili kujaza maji katika magari haya mara tu baada ya kumalizika (kama inavyoonyeshwa katika picha) , badala ya kurudi kituoni kujaza, ambapo kwanza ni mbali, pili foleni, tatu uhakika wa kuwepo maji.
PHO-09Aug21-175168.jpg
Kutokana na kukosekana kwa huduma hii , ndipo pale gari la zimamoto linaposemwa limekuja bila maji.

Tamko la naibu waziri ni zuri, lakini kwanza tuanze kujenga miundo mbinu yetu, vinginevyo tuwe na magari mengi zaidi ili yote yatumike kwa wakati mmoja pindipo tukio limetokea ili maji yakiisha gari moja, gari la pili linatumika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom