Naibu waziri wa maji akiri kuwepo udhaifu usomaji wa mita za maji unaowalipisha bili kubwa watumiaji

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
BILI.jpg

Dodoma. Kilio cha wananchi wanaozidishiwa bili za maji kwa mwezi tofauti na matumizi halisi, imebainika kinatokana na makosa ya wataalamu wa kusoma mita na kuingiza taarifa kwenye mfumo wa kompyuta.

Kero hii iliyopo maeneo mengi nchini huenda ikapata suluhu siku za karibuni baada ya wakurugenzi wa mamlaka za maji kufahamishwa juu ya hilo na kutakiwa kuchukua hatua.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaac Kamwere alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama aliyewasilisha kero ya wananchi wake kubambikiwa gharama kubwa zisizoendana na uhalisia.

Akieleza taarifa zilizopo wizarani, Waziri huyo alisema makosa mawili yamegundulika na yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

"Kuna service charge, wataalamu hawa walikuwa wanatoza gharama za kuwa na mita hata kama mteja hajapata maji. Hii tumeona si sawa. Waziri amewaita wakurugenzi wote na kuwaagiza kurekebisha suala hili," amesema.

Amefafanua pia kuhusu usomaji wa mita kwamba: "Walikuwa (wanaingiza) wana-punch kwenye kompyuta zaidi ya maramoja hivyo kuzidisha gharama hizo mara mbili."

Chanzo: Mwananchi
 
BUNGENI: Naibu waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Injinia Isac Kamwelwe, amekiri kuwepo kwa udhaifu katika usomaji wa mita za maji na kumsababishia mtumiaji wa huduma hiyo, kutakiwa kulipa bili kubwa tofauti na matumizi yake.

Injinia Kamwelwe, amesema mfumo wa usomaji mita unaudhaifu ambapo msomaji anapomaliza kusoma mita, huipeleka kwenye kompyuta, ambayo wakati mwingine hujizidisha mara mbili, na kufanya bili kuwa kubwa

19424113_861993703966872_3238146163260138021_n.jpg
 
Kwahiyo wataturudishia pesa zetu
1.maana hizi.mita ni vimeo balaa zinakimbia kuliko.matumizi
 
JE WAHUSIKA WATACHUKULIWA HATUA GANI??!!
JE WAATHIRIKA WA UZEMBE HUU WATAFIDIWA VIPI HASARA YAO??!!!
 
Serikali itoe kauli kuhusu Dawasco wanapokuja Kurekebisha Miundombinu yao hasa mabomba ambayo yanakuwa yanavujisha maji, nani anapaswa kulipa gharama??

Ni mteja ambae bomba limeharibika au Dawasco??

Maana unakuta unawapa taarifa Dawasco kuwa bomba lako linavujisha maji somewhere barabarani wakija wanakupa list ya vifaa (mara kwa mara unakuta vingine vya uongo) ili uwape hela wakanunue halafu fundi wao akisharekebisha bomba wanataka pesa.

Mchezo huu upo sana kwa wafanyakazi wa Dawasco ofisi ya Kimara.
 
sina hata hamu nao mimi hawa waliwahi kusoma usomaji wa unit 356 ukasomwa 833 na sasa wamekuja wameghoa na bomba ,,,,.............????
 
Back
Top Bottom