Naibu waziri wa madini Dotto Biteko ameitaka menejimenti ya STAMICO kujitathimini kama ina sifa ya kuliongoza shirika

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497
NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Biteko amelitaka Shirika la Taifa la Madini (Stamico) kujitathini kuhusu utendaji wao wa kazi kwa Taifa kutokana na kuwa deni kubwa kuliko uzalishaji wa shirika hilo.

Biteko ametoa kauli hiyo alipotembelea Shirika la Taifa la Madini (Stamico) leo, Dar es Salaam,ambapo amesema Stamico imekuwa na madeni yanayofanya kudidimiza shirika kutokana na miradi wanayoiendesha ya uchimbaji kushindwa kuzalisha faida.

Amesema baada ya watu kujua changamoto sasa ndio wameona sehemu kujengea hoja katika taarifa mbalimbali.Biteko amesema Stamico ilitakiwa kuwa sehemu ya kujifunzia kwa wachimbaji wadogo lakini wachimbaji wadogo hawawezi kufika Stamico kwa sababu hakuna cha kujifunza.

Stamico inadeni zaidi ya Sh.bilioni moja pamoja na deni la Stamigold la Sh.bilioni 54 na Serikali inatakiwa kulipa deni hilo na kuacha kununua madawati katika shule.Biteko amesema kuwa kunahitajika kuwepo ubunifu kwa Stamico kwa kujiona wana kazi ya ziada ya kusaidia Taifa kupiga hatua.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Alex Rutagwelela amesema kuwa maagizo watayafanyia kazi katika uendeshaji wa shirika hilo.


Chanzo: Michuzi.


 
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa Nishati alipoitembelea STAMICO.

Kawambia live kwamba ni mlinzi wa getini ndo anayepiga kazi, wengine hakuna kitu.

Kawavua nguo vibaya.

Nadhani naibu waziri huyo kaanza vizuri sana. Kuna mijamaa inakaa tu ofisini na inalalamikia serikali kila kukicha lakini ukiiuliza imefanya nini hakuna output yoyote.


Nawasilisha
 
Back
Top Bottom