Naibu Waziri wa Kilimo Mh Omary Mgumba azindua Cassava for life Kilindi Mkoani Tanga

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Campaign kubwa ya Kitaifa ya Cassava for life yazinduliwa Kilindi Mkoani Tanga.

Naibu wa Waziri wa Kilimo Mh Omary Mgumba amezindua kampeni kubwa sana Nchini ya Cassava for life Kilindi Mkoani Tanga.

Campaign hiyo iliandaliwa na taasisi ya Progress Center chini ya mkurugenzi wake Madam Rose Urio kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo,Wilaya ya Kilindi na wadau mbalimbali.

Miaka mingi tumekuwa tukishuhudia campiagn nyingi zikifanyika mijini hasa Dar es salaam na kutumia pesa nyingi ambazo hazina tija kwa mkulima wa Muhugo lakini hii imekuwa ya mfano sababu imefanyika moja kwa moja maeneo ya mashambani Kilindi Mkoani Tanga,

Naibu Waziri Mh Mgumba na Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh Martin Shigela wamepongeza hatua hiyo na ubunifu mkubwa uliofanywa na Madam Rose Urio.

Cassava for life imekuwa chachu kwa wakulima wote wa Mihogo Nchini hasa kuchangamkia fursa hii ambayo tayari nchi ya China iko tayari kununua muhogo wa Tanzania,

Rose alisisitiza kua soko kubwa liko nchini Tanzania ambapo ni pamoja na starch ya muhogo inayotumika viwandani ikiwemo viwanda vya nguo(textile industries), makaratasi, vyakula vya mifugo, bia na sukari za viwanda Naibu Waziri Mh Mgumba alitoa agizo kwa halmashauri zote nchini zinazostawi zao la muhogo kufungua mashamba darasa na kuja kujifunza kilindi kwa lengo la kungeza tija na ufanisi katika zao la muhogo.

Kwa mujibu wa Madam Rose Urio shamba darasa litakalo funguliwa wilayani humu lengo kubwa ni kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo cha muhogo na kufikia tija ya tani 20-25 kwa hekari tofauti na ilivyo sasa tani 5-7 kwa hekari.

Pia cassava for life na wadau wengine wameiomba Serikali kupitia Bank ya Kilimo ili isaidie ktk kilimo hiki biashara kwa kutoa mikopo na taratibu za rafiki.

Wakulima wameonyesha kuchangamkia hii fulsa.la mwisho madam rose urio Mkurugenzi Mkuu wa Cassava for life madam rose urio ameipongeza wizara ya kilimo,

Mkoa wa Tanga,wilaya ya kilindi na wilaya zingine zote zilishoshiriki bila kumsahau Mh Rc wa mkoa Tanga Martin Shigela ambaye akitoka maagizo kwa maafisa Ugani wote Mkoani Tanga kutembelea watengenezaji wa zana za kuchakata na kukaushia mihogo jambo ambalo liliungwa mkono na washiriki wengi na tayari kuna baadhi ya Taasisi zipo tayari kusambaza hizo machine ,

Pia wadau wingine kama world vision,Agra , Pass , Nmb na Utt na zingine zingine kwa mchango wao mkubwa walioutoa kuweza kufanikisha kampeini hiyo.

Rose alisisitiza kuwa kazi ni kipimo cha utu kwa hiyo watanzania tufanye kazi kwa bidii.
 
Huu ni ujinga mwingine. Kiimo hakihitaji kampeni kama ya nyumba ni choo. Kilimo kinatakiwa kiwe endelevu, kampeni ni shangwe za muda mfupi tu.
Kweli kabisa mkuu.

Ndio maana nikauliza lengo la kampeni
 
Back
Top Bottom